Msaada: Hivi kibox cheusi ni cha nini katika ndege

scatter

JF-Expert Member
Joined
Feb 15, 2013
Posts
1,673
Reaction score
952
Wakuu katika kitu kinacho nichanganyaga na kunifanya niwe na maswali mengi ni kuhusu hiki kidude kitwacho box nyeusi
Kwakweli mawazo yangu huenda mbali na kuanza kuwaza mambo ya kishirikina kuwa labda ni hirizi za wazungu au kinakuwa na roho za watu maana pindi ndege ikipinduka watu wapo maradhi kupoteza ma milioni ya fedha za madafu mpaka kipatikane
Je hiki ni kidude cha nini na kwanini watu wasitafute mabaki ya watu bali hukitafuta hiki kitu ...

scatter
 
Last edited by a moderator:
Black box hua inarekodi mwenendo wa ndege na maongezi ya marubani thusway ndege ikianguka kinatafutwa ili kujua chanzo cha ajali ni nini.
 
Mungai.... -> Mulugo -> Kawambwa

Elimu na Maarifa ya kizazi hiki vimeshuka sana...!
 
Black box hua inarekodi mwenendo wa ndege na maongezi ya marubani thusway ndege ikianguka kinatafutwa ili kujua chanzo cha ajali ni nini.
Ili iweje
 
Ili iweje
Mbona kila kitu kipo wazi, unapojua mwenendo wa ndege ni rahisi kujua chanzo cha ajali ni nini? Mathalani marubani wanalalamika hali ya hewa kuwa mbaya na control mpaka wanapoteza mawasiliano wanajua chanzo cha ajali ni hali ay hewa mbaya au kama ni engine failure wanajua ili wawajibishe wahusika n.k
 
Okkey nimekupata mkuu
 
Ili kuna umuhimu wa kutafuta miili kabla ya kibox
 
Huyo unayemuita "Mzungu", moja ya vitu anavyovipa kipaumbele katika maisha ni kujifunza kupitia historia. Kilichotokea jana ni muhimu sana katika kumfanya ajue leo aanzie wapi. Mfano, ukiingia katika "Museum" utaona wameweka hadi usafiri wao wa zamani, designing za nyumba walizoishi na takataka nyingine. Wakikupa huduma fulani tegemea kupewa na "survey" itakayokuuliza ubora na mapungufu ya hiyo huduma. Kwao kila jambo linahitaji "improvement". Kwa hiyo kuipata miili ni sawa na muhimu, lakini kubwa hasa ni jinsi ya kujifunza na kuangalia uwezekano wa kuzuia janga lisitokee tena; hapo ndipo umuhimu wa "black-box" unapoanzia.
Cheerz

Ili iweje
 
Wakuu katika kitu kinacho nichanganyaga na kunifanya niwe na maswali mengi ni kuhusu hiki kidude kitwacho box nyeusi
Kwakweli mawazo yangu huenda mbali na kuanza kuwaza mambo ya kishirikina kuwa labda ni hirizi za wazungu au kinakuwa na roho za watu maana pindi ndege ikipinduka watu wapo maradhi kupoteza ma milioni ya fedha za madafu mpaka kipatikane
Je hiki ni kidude cha nini na kwanini watu wasitafute mabaki ya watu bali hukitafuta hiki kitu ...

scatter

kiboksi chenyewe ni cha orange...black box zamani. kazi yake ni kuhifadhi mwenendo mzima wa ndege ikiwemo maongezi baina ya marubani, kwahio ajali ilkitokea wakikipata hiki ni rahisi kujua chanzo cha ajali....pia kinawekewa kifaa[transponder] ambacho kinatoa signal kuashiria kipo wapi ili iwe rahisi kukipata.
 
Ili kuna umuhimu wa kutafuta miili kabla ya kibox

ndio. ukipata hicho kiboksi utaweza kujua chanzo cha ajali na hivyo kuweza kuzuia isitokee in future[kwasababu za mwanzo] ila ukiipata miili haitakuwezesha kutatua tatizo lililoifanya ndege ianguke ili lisitokee tena....lakini mara nyingi huwa wanatafuta vyote kwa wakati mmoja wanagawana majukumu tu hao waokoaji.
 
Priority ya kwanza kabisa ni kuokoa maisha!
Mda ukipita kiasi cha wataalam kuamini kuwa uwezekano wa kuokoa maisha haupo tena bali ni kutafuta na kuokota maiti tu, hapo ndipo wanagawana majukumu na kuanza kutafuta mabaki ya ndege na hizo visanduku vyeusi.

Hizo "black boxes" ziko mbili.
Moja ina record mitambo, na hali ya kiufundi ya ndege, na jinsi ilivyo endeshwa. (DFDR)
Cha pili hurekodi sauti na mawasiliano kati yamarubani na controllers, na sauti zozote za chumbani mwa kuendeshe (cockpit), Inaitwa Cockpit Voice Recorder (CVR).
Vimetengenezwa kwa kutumia chuma cha pua, hivyo vinaweza kuhimili moto mkali, kuvunjika na maji baharini.
 
sababu nyingine ambayo huwafanya waokoaji kukimbilia kutafuta black box hasa inapotokea ajali kama hiyo ya kuanguka ndege baharini,ni kuwahi mlio wa tahadhari usiwapote maana betri za kusaidia kutoa mlio huo hupoteza nguvu takriban baada ya mwezi mmoja
 
Majibu ndio hayo mkuu na kingine chakuongezea ni kua black box haiharibiki na haiungui, kwaio ajali yyte black box itakua salama
 
Ahsante mgosani na matembele kwa kuongeza kitu kichwani mwangu ndio maana naipenda JF, napata vitu vingi sana
 
Hizo "black boxes" ziko mbili.
Moja ina record mitambo, na hali ya kiufundi ya
Vimetengenezwa kwa kutumia chuma cha pua, hivyo vinaweza kuhimili moto mkali, kuvunjika na maji baharini.

Nilikuwa nataka hapa hapa kwenye mtls zake maana naona hata kama ndege imeungua kinatafutwa sana sasa mm huwa najiuliza chenyewe hakiungui au kuharibika?
 
Back
Top Bottom