Mosi:Ndio chaweza fanyiwa hujuma hasa kama kuna mambo ya uhasama hasa umafia kwa mamlaka husika "mfano nchi husika na nchi nyingine " mfano mzuri kuna ndege kadhaa za viongozi wakubwa wa nchi au watu maalufu zisha anguka na hicho kibox kinachotegemewa kiwe na taarifa husika juu ya mwendo wa ajali husika huwekwa kapuni na wahusika ili kukidhi matakwa yao kwa kisingizio cha mambo ya usalam wa Taifa, n.k hasa kwa zile ndege za kimataifa, na pia kama wahusika wanataka kuficha taarifa flani flani kuhusu chanzo halisi cha ndege husika.
Pili:Utafutaji wa hicho kibox cheusi ni kwa kutumia "signals" maalumu ambazo huonesha maala kilipo angukia . Yaani kina "signal detectors" kama ambavyo askari au wanajeshi wanavyoweza kwenda msituni au maala flani kusaka bomuau mlipuko uliotokea sehemu flani ulikuwa ni wa kitu gani , utakuta hapo ni lazima kuwe kuna vifaa vinavyoweza ku detect uwepo wa kitu husika kinachotafutwa.
Tatu: Ndio , taarifa huanza kuchukuliwa punde ndege inapoanza maandalizi ya safari husika mpaka ilipo pata ajali husika.
Nne: Ndio wanaweza shindwa kukipata kama muda mrefu umepita toka ndege husika ipate ajali , mfano miezi 3 au zaidi tokea ajali itokee, kwani na chenyewe huweza kuishiwa chaji yake iliyowekwa kukitunza, mfano ndege ya malaysia ilivyopotea mazima hapo juzi kati au zile ndege ambazo huanguka maeneo ya "Bermuda Triangle" n.k au maeneo ya uhasama mfano katika uwanja wa vita.