Msaada: Hili wazo likoje wakuu?

Baba ilumba

Member
Apr 18, 2020
37
49
Nikiwa bado niko quarantine nimepata wazo kuwa baada ya corona kupita ninataka nianzishe kipindi changu
YouTube

Lengo la kipindi hicho ni nini

Nimezamiria kutembea karibu kila chocho ya Tanzania yaani nataka nitembelee karibia kila kona ya nchi yangu pendwa na yakuvutia niwaoneshe watu was dunia hii jinsi nchi yetu ilivyonzuri,ilivyobarikiwa kuwa na vivutio vya kila aina

Pia nikafikiria kama kipindi kikifanikiwa vizuri kwa hapa Tanzania basi nianze kuzunguka chocho mbalimbali za Africa

Naombeni ushari wenu. Je, hili wazo ni zuri au la?
 
Kesho asubuhi niamshe unikumbushe ntakushauri

Najua ni nje ya mada lakini umeicheki avatar yangu mkuu?
 
Duuuh watu mnakatisha sana tamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sijamkatisha Tamaa mkuu, nimejaribu kumueleza kua kuna watu wanfanya kazi Kama anayoigikiria kuifanya , chamsingi ni yeye kwenda kuangalia wanafanyaje kazi zao na wanamapungufu yapi? Na yy kuboresha zaidi ili afanye kazi zake kwa ufanisi zaidi.

Tatizo wabongo hatupendi kukutana na changamoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo zuri, Ila haujaonyesha namna gani uta monetize,Kama ni kwa kutegemea YouTube unaweza chukua muda mrefu kufikia malengo ya kipesa
 
Wazo zuri sana;ila kwa mwanzo itakugharimu asilimia 100% ujihudumie mpaka pale channel yako itakapoanza kutengeneza fedha,kama unaweza kujihudumia miezi sita kwa safari na video nzuri.....utapiga hela baada ya hapo.
 
[QUOTE="Equation x, post: 35229707, member: 452082


Wazo zuri sana;ila kwa mwanzo itakugharimu asilimia 100% ujihudumie mpaka pale channel yako itakapoanza kutengeneza fedha,kama unaweza kujihudumia miezi sita kwa safari na video nzuri.....utapiga hela baada ya hapo.
[/QUOTE]

Sawa mkuu gharama kwangu sio issue kwa miez 6 ya mwanzo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom