Rais Samia Mwanadiplomasia halisi

Rais Samia Mwanadiplomasia halisi

Joined
Jan 17, 2013
Posts
29
Reaction score
8
MAMA SAMIA SULUHU HASSAN [emoji1241]

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA MWANA DIPLOMASIA HALISI [emoji1241]

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anayo mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine tunaweza kumuelezea kwa ubora wa mambo anayo yafanya kwa ajili ya Taifa letu tukufu la Tanzania.

Katika eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mengi ameyafanya kwa juhudi kubwa hasa katika maeneo kadha wa akadha kama ifuatavyo japo kwa ufupi ila kwa uhalisia wake:

Katika sekta ya Elimu; Mh: Raisi ameweza kuboresha na kuhakikisha elimu Bure inatolewa kuanzia shule ya msingi hadi kidato cha sita. Pamoja na kuboresha miundombinu ya shule zetu ili kuzifanya shule zetu kuwa sehemu salama na maeneo sahihi ya kuwaandaa wataalamu wetu na wazalendo wa taifa letu kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Hili linaenda sambamba na wanafuzi wote wanao hitimu kutoka ngazi moja kwenda ngazi nyingine kuwa wanapata nafasi na stahiki zao kwa wakati ili kuondoka na athari zinazoweza kujitokeza na kuathiri taaluma mashuleni na vyuoni.

Sekta ya Afya,kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa kafanya jambo kubwa na lakuheshimika, kwa mapambano makali ameendelea kujenga na kusogeza huduma za afya karibu na wanchi kwa kujenga vituo vya afya, zahanati na hospitali Nchinzima.

Sekta ya Uchumi, Mh: Raisi yuko bize kuimarisha uchumi wa Nchi pamoja na kuhakikisha watanzania wanainuka kiuchumi na kuwa na taifa imara lenye watanzania imara na uchumi imara mwananchi mmoja mmoja, kwa kuendeleza nakubuni mikakati madhubuti ambayo itaendelea kuliongeza pato la Taifa. Na kusaidia mwananchi kwa kilahali ili kujipatia pesa kulingana na shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazo lenga mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Kitika Demokrasia, Mh: Raisi hapa yeye ni bingwa wa siasa na hana mbamba wala makuu kama wasemavyo waungwana, Wakosoaji wote wamaswala ya kidemokrasia sasahivi wako kutekeleza sharti lao la kisiasa na kidemokrasia. Wako bize kuzunguka Nchinzima kueneza sera na falsafa zao japo wakati mwingine waki kashifu hata mhimili wa uraisi na raisi mwenyewe (Sio desturi zetu)

Miradi ya Kimkakati, hili ni jambo ambalo lipo wazi kwani ‘site’ zote ilipo miradi ya kimkatati tunaona ni jinsi gani kandarasi wako bize kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati. Miradi mikubwa kama vile Bwawa la Mwalimu Nyerere, Mradiwa Reli ya Kisasa (SGR), Madaraja makubwa, Vivuko vya majini, kuunganisha mkoa na Mkoa, Wilaya kwa Wilaya na hatimaye Nchi nzima.

Sekta ya kilimo, Kashusha mbolea kwa kutiamkono juu ya ruzuku ya mbolea na mbolea inapatikana kwa wakati kwenye maeneo yote ya Nchi na wakulima wako bize mashambani huku wakipewa uhuru wa kuuza popote pasina kuwepo na kufungwa kwa mipaka.

Uhuru wa kutoa Maoni, Wanaharakati na wapazasauti katika Nyanja tofauti tofauti wako bize kunena na kupaza sauti katika kila eneo ambalo wanajiamini na kuona wana uwezo nalo kwa kulisemea. Lakini pia wako wanaojua kutokuutumia vyema uhuru wanaoupata kwani kila penye haki pana wajibu na haki ya mtu mmoja inapoishia ndipo inapoanzia haki ya mtu mwingine.

Sekta ya Utalii,Mh: Raisi bado yuko bize kuendelea pale alipoishia JPM kwa kuendelea kuitangaza Nchi Kimataifa juu ya vivutio tulivyo navyo katika Nchi na watalii wako bize kumiminika kwa Taifa na kuendelea kuliingizia Taifa pato la fedha za kigeni, Mh: Raisi kwenye hili hakuwa nyuma mpaka akaamua kutengeneza filamu ya kutangaza Nchi yetu na vivutio vyetu.(The royal tour).

Elimu ya vyuo vikuu na Kati,Mh: Raisi yuko bize kuongeza mikopo ya wanafunzi ili watoto wa Mtanzania mwenye maisha ya hali ya chini na kawaida waweze kusoma bila bhughudha yoyote, asilimia ya mikopo kila mwaka inaongezeka na wanapata wengi zaidi ya mwaka uliopita.

Ulinzi naUsalama, Bado Mh: Raisi wetu na Amiri Jeshi Mkuu hajawa nyuma katika maswala ya Ulinzi na Usalama wa Taifa letu, ziko program nyingi za kiulinzi na kiusalama kwa ajili ya Taifa letu pendwa zinaendelea kuratibiwa ili kuendeleza uimara wa Ulinzi na Usalama wa Taifa letu katika kila kada na kila eneo kwani Nchi haiwezi kwenda na kusonga mbele pasi na kuwepo kwa amani na Utulivu wa Taifa letu.

Umoja wa Kitaifa, Bado kama raia namba moja na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi yetu yote, ameamua kuleta umoja wa Kitaifa kwa kufanya vikao vya kimkakati na vya kimaridhiano ilituweze kuendelea kuongea lugha moja kama Taifa lenye haiba na hulka ya Taifa kulingana na dhima ya uasisi wa Tanzania yetu.

Ulimwengu wakiteknolojia,Nchi yetu kupitia kwa Mh.Raisi bado tume endelea kuto kujitenga na Dunia kwa kuingiza shughuli nyingi kwenye teknolojia ili kurahisisha na kusogeza huduma za kiserikali karibu na wananchi iliiwerahisi kuhudumiwa. Shughuli nyingi za serikali ziko kwenye tovuti za wizara husika ilikuongeza na kuchochea uharaka wakutatua mahitaji ya Wananchi kwa ujumla wetu.

Kama Nilivyosema yako mengi ambayo kwa namna moja ama nyingine Mh.Raisi anaendelea kuyatatua kupitia ilani ya Chama cha Mapinduzi, yako mengi na muda wangu hautoshi kuweza kuyaelezea kwani yako mengi. Kwa siku ya leo naweza kusema haya machache ambayo yako dhahiri wa watanzania wote wazalendo nawenye kuona ni namna gani Mh: Raisi halali na jinsi alivyo bize kuwa pambania Watanzania kwa ujumla wetu pasi na kujali Dini,Rangi,Kabila wala vinasaba vya mtu husika.

Muhimu Ikumbukwe:
Nchi ni kama familia, hakuna familia ambayo ilishawahi kumaliza changamoto za kimaendeleo ilikusaidia kabisa kukaa kwa utulivu kwamba kila jambo limeisha.

Nchi ni kama familia hatuwezi kuyamaliza yoote kwa wakati mmoja na maendeleo ni hatua na hatua inapimwa katika matokeo.

Ukilinganisha mwaka 1961December.9, maendeleo yalivyo kwa kipindi hicho toka tunapata Uhuru na Mwaka wa leo 2023, nihatua kubwa zimepigwa chini ya Chama chetu cha Mapinduzi na kwakuwa maendeleo ni hatua bado tuko bize kuendelea kuwaletea Watanzania na kutatua change moto za muda mfupi na muda mrefu.

Na:
Mr Sheja Rb
Robert H Shejamabu
Katibu Idara ya Hamasa na Chipukizi UVCCM Wilaya ya Njombe.

UVCC%20HATUNA%20JAMBO%20DOGO.jpg
 
Back
Top Bottom