Msaada: hiki ni 'kitu' gani!?

lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,466
9,028
habari wana jf

sina uhakika sana na jukwaa nililoingia na naomba kama nimekosea mods ipeleke kunakostahili.

Nimepewa hii kitu kwenye daldala jana usiku kama 'change' ya nauli na sikuwa na mashaka juu yake kwa vile niliamini na mpaka sasa naamini kuwa ni Fedha Halali kwa Malipo ya Shiling Mia Tano, 500/-!

Leo asubuhi nilivyojaribu kumpatia konda kwenye daladala akanitolea matusi na kuikataa, ikanibidi nifanye maarifa ya ziada ili kufika nilikokuwa naenda.

Nilipofika nilikokuwa naenda nikaitoa kununua maandazi, wakakataa pia.

Ndipo nikaenda kwenye kibanda cha vocha ili angalau nipate uwezo wa 'kubeep' kwa bahati mbaya nako wameikataa.

Wote wanasema sio pesa, sasa wana jf nauliza ni kitu gani hiki!!??

attachment.php

Nawasilisha
 
Attachments

  • 5.jpg
    5.jpg
    398.6 KB · Views: 944
  • 5.jpg
    5.jpg
    156.5 KB · Views: 221
hicho kitu hata mie natamani kujuwa sana, wenzetu pesa zao wanatumia makaratasi tofauti na tunayotumia sisi? maana hizi pesa zetu ni balaa
 
hiyo ni hela sema tu labda kuna mama anayenyonyesha huenda aliiweka kwenye sidiria ili vibaka wasimuibie
 
..itakuwa fedha feki kwa malipo ya shilingi mia 5 ambayo kama wakiikubali itakula kwao kama ambavyo imekula kwako so far. Pole, itupe. Ukienda pengne utaitiwa mwizi.
 
ha! ha! haaaaaa nimefurahi sana mkuu coz nilishawahi kupiga bit konda baada ya kunidai hela nyengine. baada ya kuona mambo yamemzidia akaniomba nimpatie hivo hivo.
ila ukweli ni kwamba kuna hela nyengine kwa jinsi mtu alivyo na heshima haifai hata kuitoka mfukoni.
 
sasa mkuu huyu Lukindo yeye anadai amepewa pesa na kodakta kwenye daladala na ilivyo sheria ya pesa, zinazunguka miongoni mwa watu.
Sasa tatizo liko wapi, hela zetu ndio hazifai au tunazitunza vibaya!!?? Mara nyingi pia nimeona hata hizi 'coins' zilizochakaa.
Ni bora kuangalia chanzo cha tatizo badala ya matokeo.
ha! ha! haaaaaa nimefurahi sana mkuu coz nilishawahi kupiga bit konda baada ya kunidai hela nyengine. baada ya kuona mambo yamemzidia akaniomba nimpatie hivo hivo.
ila ukweli ni kwamba kuna hela nyengine kwa jinsi mtu alivyo na heshima haifai hata kuitoka mfukoni.
 
..itakuwa fedha feki kwa malipo ya shilingi mia 5 ambayo kama wakiikubali itakula kwao kama ambavyo imekula kwako so far. Pole, itupe. Ukienda pengne utaitiwa mwizi.

Kumbe Kunafedha Feki Hata Za Shilingi Mia Tano Itafika Wakati Watatengeneza Fedha Feki Za Shilingi 200
 
Mi nimeshayeyukiwa na hizo miatano kama kumi hivi.., tena mwaka huu huu na ilibidi nizitupe...
 
Back
Top Bottom