Msaada hichi kidonda sehemu ya siri nitumie dawa gani?

Unahitajika kusafisha damu, kuna kitu watu hawaja note huwa kinaweza kukauka kwa njee alfu ndani kikavima na ukikigusa unaweza sema unajipu na ukikikamua kunatoka damu, sio ishu ya cream ni damu chafu mkuu. Dawa ya kusafisha damu ninayo na ukitaka kufanya diet mwenyewe tumia mbogamboga zenye iron Florine kwa wingi mfano, Mchunga, mnavu na matunda na kuachana na vyakula vyenye mafuta kwa wingi na vyenye cholesterol nyingi.
Ni lazima kutibu source ya ugonjwa na sio symptoms. Jitahidi kufunga fasting inasaidia hata mara mbili kwa wiki ukishindwa waweza kufunga ukanjwa maji tu hii itakusaidia kusafisha mwili mzima.

Nake Truth.
Could be true....this one is hidden Truth
 
Mrejesho:Nilichelewa kuja kutoa mrejesho humu ndani kuhusu kidonda changu Lakini baada ya kutoka hapa niliuchukua ushauri nikaenda hospital ambapo kwa bahati mbaya niliambiwa Bima yangu haijawa activated hivyo nikakosa huduma..

Halaf hichi kidonda hakikuwa na association yoyote au uhusiano na history yangu ya kuugua kabisa maana kuna watu walikua wanafukua thread zangu sijawah kuugua magonjwa ya zinaa kabisa maishani mwangu na wala sio mtu wa kujiachia sana, ni muangalifu sana nina mpenzi mmoja tu mwaka wa 8 huu

Nikamcheki dr mmoja nguli mwenye hospital yake kupitia watsaap nikamuelezea akanambia niende matibabu yake ni elfu 75 kwa kuanzia..Nikaona ngoja nisubiri kwanza

Nilishauriwa niende duka la dawa pia lakini wakati nikiwa kwenye kuwaza nichague chaguo lipi maana kilikua kimevimbia damu, nikasoma kitabu kimoja hivi ambacho nilikua nacho cha anti bacteria and anti viral herbals ambacho nilikua nimekinunua nikawa nimekipuuza tu muda mrefu kujisomea ndo nikakuta kwamba aloevera na kitunguu swaumu kwa pamoja vinakausha vidonda na ni antiviral na antibacterial pia...

Nikatafuta aloevera maana nimepanda nyumbani, nikaikata ule utomvu wake nikaukamua nikakoroga pamoja na kitunguu swaumu kilichosagwa nikapaka then nikapafunga na bandeji ili hiyo dawa isitoke nikafanya hivyo kwa kuweka aloevera na kitunguu swaumu asubuhi na jioni

You can't believe kidonda kimekauka ndani ya siku 2 tu
Baada ya kukauka nikawa naendelea kupaka kama siku 7 hivi kimepona kabisa uvimbe umekwisha yaani ukiambiwa nilikuaga na kidonda kikubwa hapo mahali huwezi amini panavyoonekana utadhani hapajawahi kuwa na uvimbe na kidonda..
Mkuu kwa maana hiyo aloe vera na kitunguu swaumu ndo tiba uliotumia hadi kupona.??
 
Usiache kwenda hospital.
Unasumbuliwa na jipu ambalo linatokana na damu kuchafuka.
Nenda kwa Wauza dawa wa Kimasai, uliza Gamba la "SUKU". Chemsha katika Lita moja ya Maji mpaka maji yawe kama chai rangi, kisha liondoe hilo gamba lianike utalitumia tena baadaye.
Kunywa robo au nusu kikombe cha chai Mara tatu mpaka yatakapoisha.
Kidonda kitakauka au kitatengeneza mdomo wa jipu tayari kukamuliwa.
Dawa hii, inapatikana kwa Wamasai itakusaidia na haina matatizo yoyote inapotumika na dawa za hospital.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom