Hiki kidonda nateseka sana nikienda haja, mwenye kujua dawa ya kuharisha

kalanga1

JF-Expert Member
Apr 10, 2017
318
424
A.alaykum wakuu, ninaomba msaada wenu jamani kwani ninapitia magumu sana, niende moja kwa moja kwenye mada
.
Kama mwezi mmoja umepita kuna siku nilienda haja kubwa, wakati najikamua nikapata maumivu kama nimechanika na kweli kinyesi kikatoka na damu kidogo... Nilirudi nyumbani kujichunguza vizuri nikakuta kweli nimechanika kidonda ni kikubwa kimetokeza kwa nje kimeingia hadi ndani, halafu kuzunguka kidonda pamevimba kiasi kwamba kuna kama linyama limening'inia chini likubwa, yaaani utaweza useme ni uvimbe umepasuka nashindwa hata kuelewa

Siku inayofata Nilienda RABININSIA HOSPITAL tegeta, doctor akaniangalia pamoja na maelezo yangu (maana hili tatizo limeanza muda, mwanzo nilikuwa napata vidonda kwa nje kuzunguka eneo la haja kubwa, siku naamka asubuhi nakuta tu kidonda, nakiuguza siku ingine nakuta tu, kila siku ni vidonda tu kuzunguka eneo la haja kubwa, nikatumia dawa hiyo hali ya nje ikapona sasa tatizo likawa ndani ) ko kwa maelezo yangu haya dr akanambia nina tatizo la anal fiscure sijui, kwa kiswahili mipasuko ya m.kundu akanipa tu dawa za kutumia ila kisipopona niende wanifanyie upasuaji.

Sasa kilichonifanya niwaombe msaada ndugu zangu hichi kidonda nateseka sana nikienda haja, yaaani napata maumivu makali mnoo pamoja na damu nadhani choo kinakwangua, naombeni mnisaidie mwenye kujua dawa ambayo nikibanwa haja nakunywa then niwe naharisha tu, yaaani maumivu yake acha kbs, nisaidieni jamani
 
Polee kwa ugonjwa huo.

Nadhani dawa yake ni ku-trim hiyo sehemu ya utumbo/rectum iliyojitokeza.

Epuka kula vyakula vitakavyokusababishia kupata choo kigumu, kunywa maji mengi, vyakula vyenye fibers na maji maji. Usikae chooni muda mrefu au kujikamua kwaajili ya kusukuma choo, acha Bowel movement ifanye yake.

Sio mtaalamu wa afya, maoni ya kimtaa mtaa baada ya kusikia sikia haya matatizo.
 
Pole sana mkuu. Pole sana.

Ngoja waje wajuvi wa mambo kwenye hili eneo.

By the way, wewe ni ME au KE? I am just curious..
 
Duuh poleee, jitahidi kunywa mtindi na mapapai ili upate choo kilaini
Asante ndugu yangu, yaaani choo sio kama kigumu kwa sasa. Lakini ni kidonda tu. Maji kwa siku nakunywa lita 3. Yaaani natamani niwe naharisha tu yawe yanapita maji tu
 
Polee kwa ugonjwa huo.

Nadhani dawa yake ni ku-trim hiyo sehemu ya utumbo/rectum iliyojitokeza...
Kadri siku zinavyokwenda kidonda kinapona na hiyo nyama inarudi ndani, na kidonda kwa nje kinapona kabisaaa, saiv hata kunawa nanawa fresh maana nyuma hata kujisafisha nilikuwa siwezi kutokana na maumivu. So nina imani kinapona
 
Me nakushauri rudi ufanyiwe upasuaji kama daktari alivyokushauri. Humu utapata kusikia mengi na mwisho utashindwa umsikilize nani
Kadri siku zinavyokwenda kidonda kinapona na hiyo nyama inarudi ndani, na kidonda kwa nje kinapona kabisaaa, sahivi hata kunawa nanawa fresh maana nyuma hata kujisafisha nilikuwa siwezi kutokana na maumivu. So nina imani kinapona.. Ila napata tu tabu wakati wa kujisaidia maana kipo kwenye njia kbs
 
Mkuu hiyo ni BAWASIRI.

Zipo za aina 3.

Bawasiri ya nje, kinatoka kama kijipu uchungu.

Bawasiri ya ndani- inatoka nyama ambayo huwa inajitokeza nje na kurudi unapoenda haya.

Bawasiri ya ndani- ila kunakua na mpasuko fulani wa mishipa,hii huepelekea kutokwa na damu haawa ukienda haja na ikiwa chronic basi hata bila kwenda haja.

Pole sana Mkuuu, I can imagine mawazo na mvurugiko wa fikra ulionao. Utapona ila pata daktari mzuri mwenye uzoefu. Pia zipo dawa za asili, jitahidi mapema kujitibu.
 
Kwa maelezo yako nilidhani bawasiri. Anyway, data maelekezo ya dokta, tumia hiyo dawa then uangalie matokeo.

Pia inaonekana shughuli zako zinakufanya muda mrefu sana unakuwa umekaa.
Hata mimi mwanzo nilijua ni Bawasiri, kila ninaemwambia ananambia bawasiri, nikatumia dawa za kienyeji. Sasa juzi nikaamua kwenda hosp nikaambiwa anal fiscure
 
Mkuu hiyo ni BAWASIRI.

Zipo za aina 3.

Bawasiri ya nje,kinatoka kama kijipu uchungu...
Asante.

Nimetumia nyingi sana dawa za bawasiri hata mimi mwanzo nilijua ni bawasiri. Yaaan sina raha
 
Hilo tatizo haliwezi kukuisha bila ya kunywa dawa za kulainisha choo, nakushauri unywe dawa za kienyeji ambazo zimethibitishwa na mamlaka husika vilevile utumie dawa ile ya kuponesha bawasiri, ipo ya kujipaka sehemu yenye jeraha, dawa za asili ndio zinaponesha hilo tatizo kwa uhakika japo ni gharama, kwa ushauri wa harakaharaka tembelea matawi ya dk Mwaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom