Msaada: Held by customs (import clearance failure)

Msaada: Held by customs (import clearance failure)

STUNTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
13,077
Reaction score
17,260
Habari za muda huu, hii ni mara yangu ya kwanza kuagiza mzigo na nimekumbana na tatizo hilo baada ya mzigo kufika nchini.

Mzigo wenyewe sio mkubwa sana nilinunua kwa Ali Express. Carrier ni AliExpress Standard Shipping.

Chini nimeambatanisha na screenshots.
Wadau wenye uzoefu naombeni msaada wenu kipi ninatakiwa kufanya.
Asante.


Adjustments.JPG
 

Attachments

  • IMG_1110.JPG
    IMG_1110.JPG
    37.3 KB · Views: 25
Wapigie courier wako..yawezekana wamedeclare pesa ndogo sana kuliko uhalisia..au umeagiza kitu kisichoruhusiwa
 
Na mm Kuna mzigo wangu walikaa nao Sana hao custom inawezekana wameamua kutupia macho waagizaji wa mizigo..huemda wsmeona Kuna pesa nyingi huko
 
fuatilia huko posta,utapelekwa kwa bwana TRA,,
lakini hapo nimeona muda haujachange kivile subiri kama siku 2 hivi,then check tena,,,,, muda mwingine custom wanachelewesha...
 
Mzigo sio mkubwa kwa maana ya UKUBWA. yaani volume, yaani urefu x upana x unene/pai mara nusu kipenyo kipeo cha pili mara urefu/n.k au sio mkubwa kwa maana ya thamani yake?!

Ninachoona hapo ni issue ya kodi ambayo haijalishi ukubwa wa mzigo bali thamani ya mzigo!
 
Nenda posta,mi pia nishawahi kukutana na huo ujumbe,kufka posta nikapewa mzgo wangu bila kodi yoyote
 
Asante, nitafanya hivyo na kuleta mrejesho.
No hurry... kama uliweka namba ya simu, utapigiwa na ukifika pale, kabla hujapewa mzigo wako utaambiwa ukalipie kama issue yenyewe ni kulipia!
 
Mimi naye yamenikuta aisee mpaka leo sijapata mzigo wangu.


Sent from my cupboard using mug
Screenshot_20210416-200225.jpg
 
Niliagiza tws earphones wakaniwekea hivyo. Nilipoenda posta wakaniambia lazima nilipie kodi. Nikawadanganya earphones nimenunua 40 badala ya 110 nikapigwa kodi ya kama 20000 hivi. Sasa sijui kama kudanganya ilisaidia au vipi. Kwasababu nilijua labda nikidanganya itakuwa kama 5000 hivi lakini inaonekana wanaangalia bei halisi.
 
Back
Top Bottom