Msaada: Hawala anataka tugawane mali

Adolph Jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
5,552
8,620
Ni muda Wa miaka mitatu sasa umepita tangu tukutane na huyu binti yaani mwaka 2017 akiwa Single mother yaani ameisha zalishwa mtoto mmoja. Tukabebana hapa sokoni bila kwenda kwao tukayajenga tukakubaliana nikamchukua yeye na mtoto wake tukaanza maisha.

Alinikuta nina nyumba moja na Kiwanja hivi sasa kile Kiwanja nimejenga na tumehamia huko.

Sasa mtafaruku unaanzia pale tulipo kwazana na anataka kuondoka na Mimi ninataka kuachana naye maana visanga vimezidi na yeye anadai tugawane Mali tulizovuna wote kwa muda huo jamani wanasheria Msaada hapo kisheria imekaaje?
 
Kisheria, Dhana ya ndoa inasema hivii:

1. Kama mmeishi pamoja miaka 2 na kuendelea;
2. Majirani wanawajua nyie kama ni mume na mke.

Basi hiyo ni ndoa kamili na kila mwanandoa ana haki kamili za mirathi pindi kikitokea chochote.

Sasa nyie mmekaa pamoja toka 2017, tena mmejenga pamoja (haijalishi pesa katoa nani), mpaka hapo huyo hakuwa hawara bali mke wako kabisa.

Ushauri: Muite myajenge kistaarabu, mpooze kidogo ili kuepusha milolongo na fedheha zitakazokupata huko mbeleni.
Unforgetable
 
Si mwana sheria ila nakumbuka sheria ya ndoa inamtambua mtu kuwa mke wa mtu kama watakuwa wanakaa pamoja kwa muda wa miezi sita hata kama hujafunga nae ndoa maadamu tu jamii inakuona unakaa nae.

Hapo mkikwaruzana chochote kilichopatikana since mnaanza kuishi pamoja ni cha wote na kitagawanywa sawa
 
Si mwana sheria ila nakumbuka sheria ya ndoa inamtambua mtu kuwa mke wa mtu kama watakuwa wanakaa pamoja kwa muda wa miezi sita hata kama hujafunga nae ndoa maadamu tu jamii inakuona unakaa nae...hapo mkikwaruzana chochote kilichopatikana since mnaanza kuishi pamoja ni cha wote na kitagawanywa sawa
Duuuuuh
 
Hwa watu wanaoitwa single mother hawa!!! natambua wako wema waliozalishwa tu na wakaachwa bila sababu isipokua %85 ni wanawake washenzi sana sana sana. hawakuachwa hivi hivi tu na baada ya kuachwa hua wako tayali kupora wanaume wa watu,watalenga mali na vitu kadhaa,hua wanatazama mpaka tunafanya kazi gani inayoweza kuleta manufaa ya maisha baadae na ukiingia kichwa kichwa baadae anakutibua makusudi ili abebe mlicho vuna.

Ni kama wako kwenye ajira na hua wanafanya kusudi kabisa bila sisi wanaume kujua,mbaya zaidi sheria zetu na jamii ya kiTanzania hua inaamini wanawake wanasingiziwa na kuonewa lakini ni kwa sababu ya aibu tu ya wanaume au kubeba msalaba kwa wanaume tunakaaga kimya

Lakini wako wanawake washenzi sana na ninakwambia kwa uso mkavu kabisa komesha huyo mwanamke ili asije kurudia kwa mwingine,namaanisha vaa uhalisia wa MWANAUME na umfunze adabu maana huwezi kushindwa,hawajaumbiwa kukushinda hao ila wapende na kuwatunza iwapo wana adabu.
 
Back
Top Bottom