MBUZI MWENYE BUSARA
Senior Member
- Nov 24, 2019
- 143
- 151
Sasa nimeongea na mke wangu kuhusu nyumba ambayo nimejenga kwenye kiwanja chake kuhusu umiliki kwasababu yeye alitaka kuandika jina lake tena kwa siri. Nimemuuliza kwanza kwamba tangu tuoane hatujawahi kuongelea kuhusu hicho kiwanja chake.
Akanikumbusha kwamba wakati tunaoana mimi nilimshauri akiuze na ilituletea mtafaruku kweli. Na ni kweli nilisita sana kujenga kwenye kiwanja cha mke wangu kwasababu nilishaona ni mtu mpenda vyake na asiye na muda na vyangu ilihali tayari sisi ni mke na mume.
Na niwarudishe kidogo kilichonifanya nimuone wa tofauti kidogo baada ya kuhamia pale, siku moja mwisho wa mwezi nilienda kuitembelea familia. Asubuhi tukiwa mimi na watoto akaleta mada kwamba Joyce (siyo jina halisi) ambaye yeye ni shangazi kwa Joyce. Joyce ameniomba Jack (siyo jina halisi) yaani mtoto wa Joyce aje aishi hapa na aende shule akikaa kwetu.
Sasa Joyce tuliwahi kukaa naye kama ndugu yake mke wangu, akawa anatusaidia kazi lakini alikuja kuondoka kwa ugomvi na mke wangu. Aliponipa hizo stori akili yangu iliyafanya mrejeo haraka sana nikakumbuka jinsi Joyce alivyoondoka kwa shangazi yake kwa maneno.
Nikamwambia mke hilo kwasasa haitawezekana na sababu niliyompa ni kwamba mtoto wetu kwasasa anasoma 'English Medium' halafu huyu Jack akija aende shule ya kawaida (serikali) mimi sitajisikia vizuri na haitakuwa sawa hata kwa tafsiri za watu wengi.
Nikamshauri kwamba, kama ni kwa ajili ya kwenda shule basi aende kwa shemeji (kaka yake mke) ambaye kimsingi yupo karibu na shule hiyo ya serikali na ni baba mdogo wake Joyce. Mke wangu alikuja juu sana na kuzua ugomvi kidogo nimpige.
Lakini maneno yaliyonikera sana ni kwamba, mimi siwataki ndugu zake na huwa nakuja hapa kuleta vurugu na kwamba anajuta kuolewa na mimi na akakimbilia nje. Baadaye nilimuita, akaja tukaongea, nikaamua kutulia ili nione maisha yanaendaje baada ya pale.
Na hapa wiki moja kabla alinijulisha swala la kuwekewa 'bcone' kwenye like eneo, kwamba inahitahijika 100,000 akanipa na ukomo wa muda, sikutaka maneno nikampa ile hela akalipa. Niliporudi akanionesha risiti, nikamwambia wafuatilie waweke.
Wiki inayofuata akanitaarifu kwamba wameshaweka 'bcone' lakini wanahitaji paspoti saba kwa maandalizi ya hati nikamwambia sawa. Nilipoenda nikamwambia ebu nenda idara ya maji ukaulizie utaratibu wa kupata maji kwa bomba binafsi, yaani kufungiwa mita ya maji kwenye hiyo nyumba.
Alienda baadaye akaniambia wanahitaji tujaze fomu na paspoti mbili, na fomu hurusiwi kuchukua unajazia kule idara ya maji, nikamwambia sawa. Jioni akaniambia kesho nataka nikapige zile picha ajaze hizo fomu na kupeleka zile picha saba kwa ajili ya hati, mimi nikaitikia sawa.
Asubuhi kulipokucha nikamwambia simamisha hilo zoezi hadi nije. Lakini nilimpigia simu jamaa yangu ambaye naye amejaza hiyo fomu, nikamuulizi hivi hizi fomu hurusiwi kutokana nazo ukajazie nyumbani? Jamaa akasema mbona mimi nilijazie nyumbani nikarudisha?!
Nikamwambia sawa, mimi nilikuwa naendelea kukusanya taarifa zangu. Jana nikafanya ziara ya kustukiza, nikafika nyumba lakini nikiwa njiani niliandika ujumbe kumjulia hali yeye na watoto nikamwambia nipo njiani nakuja huko.
Basi nikafika yeye alikuwa ametoka na watoto, nikafungua nikaingia nikampigia akasema anakuja na kweli wakawasili na watoto, watoto wangu wananipenda sana wakafurahi stori mbili tatu.
Mimi sikutaka kikao kichukue muda, nikaanza kikao na yeye nikamwambia mimi nimekuja kwa mazungumzo na wewe, akastuka sana. Nikamwambia mazungumzo ni ya kawaida ya kifamilia. Tukaongea nikamwambia hiki kiwanja si unajua ni chako, akasema ndiyo.
Nikamwambia lakini bahati nzuri tumejaliwa kujenga nyumba ya familia, akasema ndiyo. Nikamwambia kuna vitu tusipoviweka sawa huko mbeleni vitatuletea shida, akashangaa. Nikamwambia kwasasa tunaelekea kwenye swala la umiliki sasa tuamue mimi na wewe mmliki wa nyumba ya familia yetu kwenye kiwanja chako kitakuwa na umiliki wa nani? Hana jibu!
Nikamuuliza je maji na hilo suala la picha za hati mmiliki ungeandika? Akasema mimi nilijua ni vitu vya kawaida wala sikufikiria yote hayo! Nikamuuliza kwa mkuu wa familia ni nani akasema ni wewe (mimi). Nikamuuliza sasa mbona siku ile ulifanya tu kunipa taarifa tu unataka kwenda kupiga picha bila kuuliza tuandike jina la nani? Akasema mimi niliona hata nikiandika jina langu ni sawa tu na kwasababu nilikupa taarifa niliona hakuna shida.
Nikamwambia sasa mimi natambua kwamba kiwanja ni chako lakini nimejenga nyumba ya familia yangu ambayo ni sisi sote. Nimekuja tupate mwafaka wa hicho kiwanja na mimi nipo kwa ajili kuidhamini familia yangu na katika hii familia tunaojielewa kwasasa ni mimi na wewe vijana wetu bado wadogo.
Nikamwambia mimi nina majibu yangu lakini nahitaji majibu yako juu ya kiwanja hiki. Nikamkumbusha, kwamba siku ile ulivyoongea maneno ya kwamba mimi huwa nakuja kukuletea vurugu na kwamba unajuta kuolewa na mimi nilizingatia na hivyo sitakubaki kuiweka rehani familia kwa kuruhusu mambo yaende kiholela.
Akahamaki na kudai kwanini namkumbusha mambo ya zamani, nikamwambia haikuwa sehemu ya mada lakini nimeona nikukumbushe ili ujirekebishe kimawazo, kauli na kimtazamo na ufahamu mipaka yake kama mke. Akasema yale alitamka kwa hasira kwasababu ulinikemea mbele ya watoto n.k, nikamwambia mimi uliniletea mada yako mbele ya watoto na nilipopinga wewe ndiyo ukaleta ugomvi.
Akasema tuyamalize kwanza haya ndiyo tuje swala la umiliki wa nyumba. Ila nikamwambia mimi siwezi tena kukuruhusu kumiliki hii nyumba kwasababu hustahili, utashindwa kuzuia hisia zako na utaendelea kuropoka zaidi na huenda hata kuna siku utamleta mwanaume humu na sitaweza kuzuia. Naye akasema na wewe unaweza kumleta mwanamke halafu unitoe mimi.
Mwisho akasema nimpe muda atafakari swala la umiliki wa hii nyumba halafu atanipa jibu kwamba hawezi kupata jibu la haraka. Lakini nimemwambia mimi ndiye nina wajibu na jukumu la kulinda, kuhifadhi na kutunza mali za familia hivyo yeye ni mtu wa pili kutoka kwangu na akaona ugumu nipo tayari kumpa pesa yenye thamani ya kiwanja chake, yeye atajua atazifanyaje hizo hela lakini kiwanja kiwe chini ya familia na chini yangu kama mwenyewe dhamana ya familia namba moja.
Kwa hiyo namsubiri aamue halafu nami nitaweka msimamo wa kiti. Japo sasa amenuna lakini mgonjwa haulizwi dawa. Mimi kiukweli sina mpango B ya hilo, nahitaji heshima iwepo kwangu kama mwenye nyumba na siwezi kuwa mtalii kwenye familia yangu. Lazima kiti kiheshimiwe bila hivyo panya watatawala.
Naomba kuwasilisha kwa ajili yenu kujifunza na kutoa ushauri.
Asanteni.
Pia soma: Mke wangu anataka kuandika jina lake nyumba niliyoijenga