Msaada hatua za kufuata kabla sijaanzisha biashara

senzoside

Senior Member
Mar 13, 2012
183
31
Habari wanajukwaa hili la biashara!

Nimekuja kwenu mnisaidie hatua za kufuata kabla sijafungua biashara nataka nifungue duka ambalo nitauza bidhaa zifuatazo Vipondozi aina zote, vitenge, madera, na kwa baadae nifumgue huduma zote za kifedha (M-pesa, Tigo pesa, Airtel money, Halopesa na wakaka wa NMB, CRDB pamoja na NBC)

Sasa sijui nianzie wapi...Kwakuwa huku kuna wataalamu mbalimbali na wazoefu nimatumaini yangu nitabata muongozo stahiki. Aksanteni na Mungu awabariki.
 
Habari wanajukwaa hili la biashara!
Nimekuja kwenu mnisaidie hatua za kufuata kabla sijafungua biashara nataka nifumgue duka ambalo nitauza bidhaa zifuatazo Vipondozi aina zote, vitenge, madera, na kwa baadae nifumgue huduma zote za kifedha (M-pesa, tigo pesa, Airtel money, halopesa na wakaka wa nmb, cradb pamoja na nbc) sasa sijui nianzie wapi...Kwakuwa huku kuna wataalamu mbalimbali na wazoefu nimatumaini yangu nitabata muongozo stahiki. Aksanteni na Mungu awabariki.
Tafuta TIN namba kwanza,
Mengine watakuja wajuvi kukuelekeza.
 
Habari wanajukwaa hili la biashara!
Nimekuja kwenu mnisaidie hatua za kufuata kabla sijafungua biashara nataka nifumgue duka ambalo nitauza bidhaa zifuatazo Vipondozi aina zote, vitenge, madera, na kwa baadae nifumgue huduma zote za kifedha (M-pesa, tigo pesa, Airtel money, halopesa na wakaka wa nmb, cradb pamoja na nbc) sasa sijui nianzie wapi...Kwakuwa huku kuna wataalamu mbalimbali na wazoefu nimatumaini yangu nitabata muongozo stahiki. Aksanteni na Mungu awabariki.
Jambo la kwanza tafuta TIN ya biashara pamoja na vibali vyote vya biashara kama manispaa na TFDA

Tafuta location nzuri ambayo ina movement kubwa ya watu maana hiyo biashara haihitsji sehemu ambazo zimejificha.

Fanya research ni bidhaa zipi huwa zinauzwa kwa wingi na wapi pa kuzipata kwa urahisi.

Line zako zote za biashara zinasoma majina yako iwe nmb,crddb na hata tigo pesa kuepusha kupigwa kwa line hizi za watu

Hakikisha una record trend yako ya biashara kila mwez kwa bidhaa zinazopendwa na kama unapanda au unashuka wengine wataendelea
 
Tafuta sehemu ambayo unadhani wateja wengi wanaishi/wanapita. Bila shaka Una mtaji tayari na umeishafanya forecast ya biashara ukaiona ni endelevu.

Tafuta duka/suppliers utakaponunua bidhaa kwa bei nafuu na ujue jinsi ya kufikisha dukani kwako hizo bidhaa kwa bei nafuu. Bei nafuu i dont mean substandard stuff.

Bahati nzuri biashara yako haihitaji kuwa na leseni zaidi ya leseni ya biashara from halmashauri/Manispaa. Pata TIN ya Biashara na ufanyiwe makadirio TRA ambayo utaanza kulipa baada ya miezi sita. Kama mauzo yako kwa mwaka (gross) yanazidi 11m, nunua machine ya efd, kama hayazidi hapo nenda stationery tengeneza cash sales zinazoonyesha TIN yako na jina.

Oh sorry vipodozi vinahitaji leseni pia from TMDA
You are ready for the business
 
Tafuta wafanyabiashara kadhaa wanaofanya unachotaka kufanya,uongee nao(ana kwa ana) kuhusu hiyo biashara unayofanya,lengo ni kupata picha hiyo biashara inafanywaje,changamoto za biashara na wanavyozikabili na mbinu kadhaa za kuuza vizuri zaidi.Ujue bidhaa wanatoa wapi,faida ya bidhaa ipoje na mengine mengi utajifunza kama utauliza maswali muhimu.Kila mmoja ataeleza atakachotaka kukuambia,ni muhimu kuongea na zaidi ya mmoja upate picha pana ya unachotaka kufanya.Wengine hawatotoa ushirikiano mzuri,lakini nimejifunza watu wengi ni wema na wapo kutoa ushirikiano kwa wengine kama utaonesha una nia ya kujifunza.

Chagua location sahihi ya biashara,hata kama itakuchukua muda lakini location inamatter sana kwenye biashara,katika kuongea na hao wafanyabiashara,dadisi ni location zipi zinafanya vizuri zaidi kwa biashara unayotaka kufanya.Then utafute location ambayo angalau itakupa advantage uanze kwa ufanisi kwa asilimia kubwa.

Jua ni bidhaa gani muhimu ambazo ni lazima uanze nazo,hii unaweza kujua kutoka kwa mahojiano na watu wanaofanya biashara hiyo.Nyingine utaongeza kadiri ya uhitaji,maana mahitaji ya location mbili tofauti,hutofautiana pia.Biashara ni mzunguko wa pesa,usikubali kuweka bidhaa ili mradi ujaze duka tu,jitahidi uweke bidhaa zenye kuhitajika,zinazotoka.

Kwa mtaji utakaanza nao wowote ule,jitahidi sehemu yako ya biashara ivutie.Chagua design nzuri ya kupangilia muonekano wa sehemu yako ya biashara,hutokamilika..mengine unaweza kufanya baadae.

Ukishaanza biashara yako,kuwa mvumilivu,ondoa mategemeo ya mafanikio ya haraka,ipe muda na wekeza mapato katika kukuza biashara katika bidhaa zenye uhitaji na ambazo huna.Wahudumie vizuri wateja wako na kama utaweka mtu mwingine kama muuzaji hakikisha anahudumia vizuri wateja wako.Itakusaidia kuwa na wateja maalumu ambao watakuwa wakirudi mara kwa mara wakihitaji bidhaa fulani.

Hakikisha unaijua biashara yako vizuri ikiwezekana kuliko hata anayekuuzia,kama utaweka mtu,kuwa karibu na biashara,ujue kwa asilimia kubwa kila kinachotokea kwenye ofisi yako.

Kwa yote utakayojifunza kabla ya kuanza biashara hayototosha,jitahidi uwe na utulivu wa kusuluhisha kila changamoto mpya itakayojitokeza na ujiongeze pale itakapobidi ili kuhakikisha biashara yako inaenda vizuri.
 
Tafuta wafanyabiashara kadhaa wanaofanya unachotaka kufanya,uongee nao(ana kwa ana) kuhusu hiyo biashara unayofanya,lengo ni kupata picha hiyo biashara inafanywaje,changamoto za biashara na wanavyozikabili na mbinu kadhaa
Wazo zuri sana
 
  • Natumaini mtaji unao
  • Tafuta fremu ya duka, na lipia miezi 3 au 6
  • Tafuta TIN TRA
  • Lipa kodi
  • Tafuta leseni kwa halmashauri/manispaa/jiji
  • Weka mzigo dukani
  • Weka binti mrembo auze
  • Anza kuhesabu mapato
 
Habari wanajukwaa hili la biashara!

Nimekuja kwenu mnisaidie hatua za kufuata kabla sijafungua biashara nataka nifungue duka ambalo nitauza bidhaa zifuatazo Vipondozi aina zote, vitenge, madera, na kwa baadae nifumgue huduma zote za kifedha (M-pesa, Tigo pesa, Airtel money, Halopesa na wakaka wa NMB, CRDB pamoja na NBC)

Sasa sijui nianzie wapi...Kwakuwa huku kuna wataalamu mbalimbali na wazoefu nimatumaini yangu nitabata muongozo stahiki. Aksanteni na Mungu awabariki.
TAFUTA PIA MSHAURI WA KIBIASHARA AKUPE BUSINESS PLAN
 
Habari wanajukwaa hili la biashara!

Nimekuja kwenu mnisaidie hatua za kufuata kabla sijafungua biashara nataka nifungue duka ambalo nitauza bidhaa zifuatazo Vipondozi aina zote, vitenge, madera, na kwa baadae nifumgue huduma zote za kifedha (M-pesa, Tigo pesa, Airtel money, Halopesa na wakaka wa NMB, CRDB pamoja na NBC)

Sasa sijui nianzie wapi...Kwakuwa huku kuna wataalamu mbalimbali na wazoefu nimatumaini yangu nitabata muongozo stahiki. Aksanteni na Mungu awabariki.
Naomba kufaham yafuatayo kabda sijashauri chochote.

1: Mtaji wa kufungua biashara hiyo umeupataje?

2: Vitenge na vipodozi aina zote unaviweka flame Moja au office tofauti.

3: Unafanya au umewahi fanya kazi/shughuli gani kabda?

4: Eneo/mji unao plan kufungua biashara zako.

5: Utasmama mwenyewe au utamuweka mtu?
 
Back
Top Bottom