Msaada: Hatari kulipishwa zaidi kwenye mkopo CRDB

Kama alikopa mkopo wamiaka 5 atalipa m.22,854,000.na kila mwezi anakatwa 380,901.happ riba ni 18%
 
Kweli kuna usanii sana, walimwambia riba ya chini( kati ya 20-30) hakumbuki, akakopa 15,000,000 atalipa 22,000,000.Kimsingi sio wakweli.
Njooni mkope kwenye benki za Kiislamu...hakuna riba huku. Riba ni haram..inadhulumu watu badala ya kuwasaidia.

Uislam umeweka utaratibu mzuri sana wa kukopesha ambapo wote wawili mnafaidika sawa sawa.
 
principal Amount ni kianzio
final maturity date ni tarehe ya mwisho
first drawdown date ni tarehe ya kupunguza deni(akiba) ya kwanza
total facility ni Wenda alichukua pesa nyingi,au aliweka kiasi maalumu cha kukata au makubaliano ya mkopo.
Hizo form za mkopo halijaziwa au kajaza mwenyewe kwa ufahamu wake wende kuna misteki kafanya
Principal amount ni kiasi cha mkopo alichopokea ambacho kulingana na maelezo yake ni Tshs. 15m. Na total facility ni jumla ya kiasi ambacho atakuwa amelipa pamoja na riba yake hadi tarehe ya mwisho ya kurudisha mkopo baada ya hiyo miaka mitano (yaani principal amount + interest) ambacho kwa case yake huyu mwenzetu ni Tshs. 22,854,060.
 
Hapo nadhan kosa sio la bank ila mwajiri wake, awasiliane na maafsa utumish wanajua kila kitu.
 
Yap alikopa kwa miaka mitano,na kiasi hicho ndio anachokatwa, mkuu inaonesha unayafahamu vizuri.
Hivi huwa wanakata vipi?,maana alikopa m15 atarudisha m22.8 naona ongezeko ni m7.8
Ambayo ni zaidi ya 18%.
Iko sawa .unajua jinsi unavyo ongeza muda wa kulipa ndo riba inaongezeka.kama una android nenda kwenye playstore download multculculator.alafu tafuta sehemu inaitwa loan calculation
 
Mimi nadhani kitu cha msingi ni kuurudia kuusoma mkataba ili kujiridhisha mkopo ulitakiwa kulipwa kwa Muda Gani.

Suala jingine ni vizuri wewe na mkeo mkaenda benki pamoja ili kupata maelezo ya kina na kwa lugha yetu adhimu ya kiswahili. Wakichanganya kiingereza unasema bayana huelewi.
Chukua "bank statement" kuanzia mwezi wa kwanza kurejesha hadi sasa.
 
Walimu mnapenda sana kukopa,usilie vumilia! Hayo maswali ungemwuliza bepari tangu Mwanzo wakati mnachukua mkopo
 
Back
Top Bottom