Kuna Tatizo gani benki ya CRDB?

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
17,287
10,698
Wiki kadhaa zilizopita nilienda CRDB kuomba Mkopo binafsi.

CRDB wakasema lazima mshahara wangu upite kwao. Nikahamisha mshahara kutoka NMB kwenda CRDB ndipo nikajaza form za mkopo na kuzirudisha CRDB Bank.

Nilivyorudisha tu fomu loan officer akaniambia sasa hivi mfumo unasumbua kidogo huenda ukawa tayari after two weeks. Mie nikadhani yule afisa anataka kitu kidogo na kwa vile hizo wiki mbili kwangu hazikuwa nyingi sikutaka kuanza kuwaza habari za kitu kidogo.

Lakini baada ya kuanza kupita pita katika mitandao hasa page za CRDB naona kuna msururu wa watu wanalalamika kuwa huenda CRDB imefulia maana kuna watu wamerejesha fom toka December mpaka leo hawajapewa mkopo. Na wengine wameanza kukatwa rejesho bila kupewa mkopo. Ukiwapigia Simu CRDB au ukiwaandikia wanakwambia tunafanyia kazi suala lako.

Hapa najiuliza ina maana kweli mfumo unasumbua,au ni benki imeyumba haina fungu la kutosha kukopesha au kuna kitu gani kimewakumba CRDB?
 
Kufuatilia mkopo wapo, nadhani unajua anapata commision kwa kila mkopo unao kamilika.. so anakuona mtu muhimu sana.

Hutakiwi kumpa hata cent 5.
Ndugu yanyu wenyewe wana kitu kinaitwa system. Kila mwenye kutaka mkopo bila kupitia system file litakaa haliendi popote. Kila ukienda utambiwa leo system haifanyi kesho system haipo basi shida tu. Watu wazima mmenielewa. Jitume tu kuitia charge system mambo yako yaende😏😏
 
Eti unaenda kukopa halafu utoe kitu kidogo kwa loan officer. Sifanyi huo ujinga hata siku moja. Biashara kuu ya benki ni kukopesha. Mkopaji ni mteja muhimu sana kwa benki. Tusiendekeze kutoa hata senti kwa loan officers, hiyo ni kazi yao walipwa mishahara na marupurupu
 
Benki ya kifala sana hii kwa sasa, wapo na huduma yao ya e-banking wanahimiza watu kujiunga ila bado wako zama za mawe hawa jamaa. Wiki jana nilitoka nje ya nchi kidogo nikataka kutuma chochote kwa familia hii "system"yao inagoma haitoi password, kutafta msaada kwao zaidi ya wiki mbili hakuna solution wafanyakazi hawajielewi mpaka mameneja wao kwenye hiki kitengo cha e-banking, non-proffessional kabisa sijui wanawaokota wapi. Well, safari bado ni ndefu.
 
Back
Top Bottom