Iceberg9
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 26,659
- 50,947
- Thread starter
- #41
Ahsante sana mkuu, hilo mimi pia nililliona wenzetu wajanja sana, kwao kuna masoko yani demand is very high tena sana na kama hawapeleki kwao wanapeleka nchi za jirani tatizo sisi hatuwazi nje ya box, mkuu yani my bro ambaye yupo UK amenitia hamasa sana hii kitu lazima niifanye, hapa nipo kukusanya tafiti mpaka kieleweke,Mkuu,
Kuna mambo mengi ya kuendelea kujiuliza na kufanya utafiti wa kutosha.
Mfano: Kuna kampuni/jamaa wanakuja nchini kutokea nje ya nchi na sanasana ni Wahindi, wanaweka kambi humu nchini na hasa mashambani huko, wananunua mazao kama Ufuta, Choroko, Mbaazi, Dengu na mazao mengine ya jamii ya Mikundekunde, wanapopeleka huwa hatupajui na hakuna anayejishughulisha kujua huwa wanayapeleka wapi, kwa kifupi hapa namaanisha MASOKO.
Kama bidhaa hizi zipo hapa nchini kwetu kwanini sisi tunaishia tu kuwauzia hawa wanaotulangua, ina maana sisi hatuwezi kupeleka huko wanapopeleka wao.
Hebu tufunguke vijana. Na kwa sasa nina imani na serikali tulonayo.
Kwa ufupi nimeanza kutafuta namna ya kufanya packaging na nimeshazingatia viwango vinavyohitajika ISO, hao wahindi, wachina mkuu tena wananunua kwa bei ya chini sana kwa mkulima yani ni walanguzi hatari