Itambue biashara ya Export Tanzania

Itambue biashara ya Export Tanzania

BARADIGE

Member
Joined
May 22, 2014
Posts
74
Reaction score
36
Habarini Wana jukwaa na poleni na majukuku ya kila siku.

Leo ningependa tujadili kuhusu biashara ya export ambayo kwa namna Moja au nyingine ni biashara inayo fanywa na watu wachache na hii hutokana na kukosa maarifa ya dhati katika biashara hii.

Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zina export bidhaa mbalimbali lakini kwa kiwango kikubwa ni bidhaa za agriculture na madini kwani nchi Bado ipo katika stage ya ukuaji.
Tanzania katika soko la Dunia hutambulika katika uuzaji wa bidhaa mbalimbali ambazo ni pamoja na

•madini ( Dhahabu ,almasi pamoja na madini mengine
•Kahawa,karanga,korosho,Chai pamoja na mazao mengine.

Kama unahitaji kujifunza na kuanza biashara hii unapaswa kujua mambo kadhaa; ambayo ni
•unahitaji kusafirisha zao Gani au bidhaa Gani

°Vibali vipi vinahitajika na uanze wapi; Tuchukulie mfano
kama unahitaji kusafirisha kahawa unahitaji kufanya yafuatayo
Kwanza upate kibali Cha ununuzi wa zao hili kibali hiki utapata katika bodi inayo simamia zao husika

Ukisha nunua utafanya process za kukusanya katika warehouse au ma ghala yanayo tambulia na mamlaka ya mapato TRA
Kisha utafalitilia vibali kadhaa ambavyo ni Export permit yan kibali ya kusafirisha bidhaa yako nje na Kisha utafatilia vibali vingine ambavyo hutolewa na mamlaka ya chakula
,Atomic,pamoja na mazingira
Baada ya hapo utalipia Kodi katika mamlaka ya mapato na hii ni baada ya mamlaka kufanya ukaguzi wa docoment zote kama ziko sawa na kutathmini Kodi husika

Kimsingi biashara hii ni biashara iliyo fanywa kuonekana ni watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi lakini

Biashara hii unahitaji maarifa ya soko pamoja na kujua wateja wako

Maarifa ndo msingi mkubwa wa mafanikio ya biashara hii
Mifumo ya mafanikio sehem yoyote ukikosa maarifa utakuwa gizani

Njooni wadau tujadili tujikwamue kwa pamoja

tea eport permit.jpg
Radioactivity analysis Certificate.jpeg
ASSESSMENT_DOCUMENT_TZDL-18-1382638-page-001_1.jpg
 

Attachments

Hii biashara ni nzuri sana na inataka uwe sharp na smart sana ili utoboe,
Mojawapo ya changamoto ya biashara ya Export ni kuwa inataka uwe na uhitaji wa uhakika kabisaa wa unachokiuza na uwajue hasa wanunuzi vinginevyo kupoteza hela ni nje nje, na pia kuna complinces nyingi kwenye hii biashara na ni ukweli ulio wazi kuwa mara nyingi sana kuwa tayari kuna magwiji wanaokuwa washaestablish mizizi ambayo si rahisi sana mtu mpya kutoboa kirahisi.
 
Mojawapo ya changamoto ya biashara ya Export ni kuwa inataka uwe na uhitaji wa uhakika kabisaa wa unachokiuza na uwajue hasa wanunuzi vinginevyo kupoteza hela ni nje nje, na pia kuna complinces nyingi kwenye hii biashara na ni ukweli ulio wazi kuwa mara nyingi sana kuwa tayari kuna magwiji wanaokuwa washaestablish mizizi ambayo si rahisi sana mtu mpya kutoboa kirahisi.
Yupo mzee mmoja hapo bandarini anaexport mchele kukunja B kila mwezi ni kawaida sana kwa sababu ana mizizi ya biashara muda mrefu.
 
Unajua wafanyabiashara wengine wa Tanzania Bado upande wa export hawana maarifa sana kutokana na
Biashara hii kwa kipindi kirefu imekuwa ikimilikiwa na watu wachache Tena wenye vipato vikubwa
Mfano ukisema madini ya copa kwa Tanzania utakuta muuzaji mkubwa ni Bravo
Ukija kwenye zao la katani unamkuta Mo Dewji kaliteka soko
Hii inasababishwa hasa na nini?
Moja watu hawana maarifa ya je akitaka kuuza nje nani ni mnunuzi na anataka nini hasa
PILI
Mamlaka husika mfano Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA)
Ambao kwa kiwango kikubwa ndiyo
Inatoa taarifa ya masoko ya nje na kusimamia utaratibu wa biashara hii
Kushindwa kuwapa watu Taarifa ili wafanya biashara wapambanie fursa
Ukitaka kufahamu watu wapi gizani
Huwez kujua hata sasa je kama nimelima labda karanga je nawezaje kuuza nje ya Tanzania? Utakuta wengine hawafaham
Pia Taasisi nyingi zipo kwaajili ya kusimamia wale waliobahatika kujua fursa siyo kutengeneza wafanya biashara wapya
Kimsingi Kuna haja ya kufukua upande huu wa export business ili tupate matajiri wengine zaidi.
Nchi zilizo endelea zimepata mafanikio kwakuwa kiwango kikubwa bidhaa huenda nje ili kufanya fedha yao ipande thamani.
 
Back
Top Bottom