Msaada: Dawa nzuri ya kuua nzi

Kuna mtu kamya ndani nini?
dawa ni usafi tuh asikudanganye mtu
 
Kuna mtu kamya ndani nini?
dawa ni usafi tuh asikudanganye mtu
Soma Maelezo vizuri!Nzi wanavamia kutoka kusikojulikana wanafikia nje ya paa,ukifungua mlango tu au dirisha wanaingia ndani!!!
 
Mkuu achana na imam potofu mm mwenyew mwenyeji wa Mbeya japo Sjawah ona nzi maeneo yang lakin cha kufanya nenda duka LA mifugo apo mbaliz au popote Karibu na wew kuna dawa za Aina zote ila jaribu kuondoa vitu au sehem wanapopenda kutua Kama kamba hivi zingatia hiyo dawa ya ingita ina packet ya yellow inachenga chenga
 
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
ASANTENI WANA JF KWA USHAURI WENU!!NILIJARIBU KUUFANYIA KAZI LAKINI KILA NILIPOTUMIA DAWA KESHO YAKE NZI WALIONGEZEKA!NILIKUWA NIKIKUSANYA WANAJAA KWENYE NUSU KILO!NIKIRI SASA NIMESHINDWA.NIMEJARIBU KUMSHIRIKISHA MWENYE NYUMBA ANATOA MAJIBU YASIYOELEWEKA ETI NI MSIMU WAKE NDIYO WAJAE KWANGU TUUU??NIMESALIMU AMRI NINAFUNGASHA VIRAGO.ABAKI NA NZI WAKE
 
Hiyo nyumba haifai, Kuna mapepo wabaya wa huyo mwenye nyumba
 
Iko Dawa inaitwa ingita nadhani pkt yake ya yellow, na Dawa in chengachenga za yellow, ni balaaa wanakufa.
Nimejaribu lakini wapi!Wanakufa leo halafu kesho wanakuja mara mbili yake
 
Duh[emoji23]
Nacheka kama mazuri..

Dawa nzuri Ni jina lako "umunyu" yaani "chumvi"
Tafuta chumvi ya mawe,iombee kwa Imani na inyunyize kila sehemu..
Unaweza ukawa unanyunyiza huku ukitamka na kukemea.

Nyingine iloweke itumie kudeki na kufuta madirisha na sehemu mbalimbali.

Kama kuna uhusiano wa hao nzi na nguvu za Giza basi vyote vitapotea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nacheka japo sio mazuri, nyumba za watu zina mambo sana....

Kama ni nzi wa kawaida nunua dawa ya pakti inaitwa green leaf unachanganya na maji lita 1 unamwaga tu chini wanakufa sana.

Kama ni nzi wa mtu hilo sijui, pole.
 
Nacheka japo sio mazuri, nyumba za watu zina mambo sana....

Kama ni nzi wa kawaida nunua dawa ya pakti inaitwa green leaf unachanganya na maji lita 1 unamwaga tu chini wanakufa sana.

Kama ni nzi wa mtu hilo sijui, pole.
Asante kwa ushauri Ila kwa nilipofikishwa na hawa nzi nimesalimu amri ninaikimbia hii nyumba
 
Asante kwa ushauri Ila kwa nilipofikishwa na hawa nzi nimesalimu amri ninaikimbia hii nyumba
July hadi leo September bado unatishia tu kuhama?😁
Kodi inaisha lini kwani?
 
Jamani hii chumvi mi naiogopa niliwahi kuinyunyizia kwenye nyumba ya watu mmh naona niliamsha yaliolala.... kesho yake nilibeba pochi na nguo za kazini nikaacha nyumba, nilirudi baada ya miezi miwili kurudia vitu vyangu.
 
Inaisha Desemba 31
Mwenye nyumba anakutingisha uhame hilo ndio lengo, ukiondoka leo anaingia mwingine analipa kodi baada ya mwezi matukio yanaanza anakimbia.

Kuna uzi humu unaeleza wenye nyumba wanafanya hayo ili wapate hela, utafute usome.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…