Habar wana jf, tatizo langu n computer yangu inachelewa kuwaka na kuzima kuna maneno fulan huwa yanapenda kutokea( window update ) sielew nifanye nn na mm sio mtaalam wa maswala haya ya IT msaada tafadhal.
Inapochelewa kuwaka mimina mafuta ya taa,diseli au petroli alafu uwe na kiberiti. Inapochelewa kuzima, chukua ndoo ya maji au maziwa na uimiminie.Itazima hapo hapo, in fact, itakufa.
Usijali ikifa, kuna mbinu za kuifufua.....wataalamu watakuja kukusaidia hapa.
Usijaribu kutekeleza ushauri huu kama wewe sio fundi wa computer.
Wasaidie wataalamu wa hayo madudus kwa kujieleza vizuri ili wakupe msaada stahiki.
Unatumia Computer ya aina gani? model, system inayotumia, windows version ipi? ukubwa wa disc, na wewe umeshatumia asilimia ngapi ya disc?
Program zipi,ngapi zinajianzisha zenyewe wakati unapowasha computer yako.
Je unatumia anti-virus? moja,mbili, tatu kwa wakati mmoja?.
Ukijieleza vizuri utapata msaada unaouhitaji,dugu.