Msaada: Biashara ya Nyumba ya Wageni (Guest House) imekaaje?

mkuu acha kuwatisha wenzako. Biashara ya gest ni moja ya biashara yenye faida sana kama ikiwa sehem nzuri na wafanyakazi waaminifu na wachapakazi.
 
LOCATION; LOCATION; LOCATION......

Huwezi ukaiweka kijijini ambapo wakazi wote ni wenyeji na wageni wao wakija wanarudi makwao hivyo wanazo sehemu za kufikia...

Ila kama ipo karibu na sehemu zenye mizunguko ya watu na karibu na sehemu kama Stand za Basi n.k. lazima italipa. Pia inabidi ujue unalenga watu wa aina gani ili uweze kuweka bei kulingana na watu unaowalenga, pia customer service ni muhimu, usafi na security kwa watu wanaokuja.., kwahio kuwa na kiwanja sehemu fulani huenda hio sehemu ikawa bora zaidi kwa shughuli nyingine, fanya research kuangalia hapo ulipo karibu kama kuna nyumba kama hizo au huitaji wa hizo nyumba
 
Hii biashara ni nzuri,unaweza jaribu kuwekeza nje ya mji katika barabara kuu,ukilenga wateja wa malori,kwa mfano utafanya mahesabu kwa wastani lori kutoka dar kwenda nyanda za juu dereva atahitaji kulala mfano ruaha mbuyuni nenda kawekeza hapo,au kwa njia ya kati ikungi,vivyo hivyo unaweza kucheki njia ya arusha labda hedaru,muhimu katika hili kuwe na parking;hutajuta kuwekeza hela yako na fursa nyingi zitajitokeza,utapata hela ya parking.car wash,kuziba pancha,na baadae utafungua hoteli,kama ikiwa safi na watu wa mabasi watakuunga mkono
 
Ni kweli hiyo pesa ni ndogo kwa kujenga g.house ya kisasa.unaweza kukwama kwenye finishing na ununuzi wa vifaa vya g.house.ila ni biashara ambayo huwezi kulala njaa bali si rahisi pia kutajirika.
 
tofali elf 10=10m
nondo pc 200=3m
mchanga lori 15=1.5m
kokoto lori 5=1m
cement mifuko 500=6m
mbao pc 1000= 7m
bati pc 400=6m
fundi hadi kupaua na plasta =10m
haya ni makadirio ya dsm, pwani na tanga mm cjui uko wapi. jumla ni 45m. hapo ni guest ya vyumba 10. nenda benk kachukue mkopo wa 70m umalizie kila k2 na baadh ya vyumba unaweka AC. Marejesho approx 6.5m kwa mwezi kwa mwaka 1. hakikisha kila cku unapata takriban laki 2.5 ili upate 7.5m kwa mwezi. jitahd wafanyakaz wawe wanalipwa kwa pesa itakayotokana na biashara ndogondogo za hapo kv vinywaj na misosi ili na ww ubaki na angalao 1m ya kukupoza ktk huo mwaka mmoja wa maumivu ya marejesho. angalizo: inatakiwa eneo lako liwe na mzunguko wa wasafiri na wachepukaji
 
Mzawa JF..mbona umesahau vitu kibao..milango na fremu zake..madirisha...vifaa vya umeme..mabomba ya maji..rangi..vitasa vya milango..gharama za kuunganisha maji na umeme..ceiling board/gypsum board..hiyo gest ya vyumba kumi vya aina gani self contained au vyoo vya nje..
 
Siku hizi watu wanasafiri sana, ukiwa mkoa wowote unaona mabasi mengi yanaingia yakiwa na abiria kibao. Hivi hawa wote ni mafusca, majambazi wezi? Je mashehe na mapadri huwa hawasafiri? Acheni kutisha wenzenu biashara ya guest ni nzuri. Otherwise ni kama vile biashara ya zahanati inatibu kila mtu na sio kosa.
 
wakubwa nisaidie mimi nataka kujikita kwenye biashara ya gest je? Biashara hii imekaaje kwa wale wazoefu
plani zangu ni kwamba iwe ya kisasa kama chakula,vinywaji,malazi bila kukosa m-pesa .
Kwasasa hela ambayo nimeisha kukusanya haizidi tsh. 50.ml
kiwanja kipotayari.
unatafuta watu wagombane
 
tofali elf 10=10m
nondo pc 200=3m
mchanga lori 15=1.5m
kokoto lori 5=1m
cement mifuko 500=6m
mbao pc 1000= 7m
bati pc 400=6m
fundi hadi kupaua na plasta =10m
haya ni makadirio ya dsm, pwani na tanga mm cjui uko wapi. jumla ni 45m. hapo ni guest ya vyumba 10. nenda benk kachukue mkopo wa 70m umalizie kila k2 na baadh ya vyumba unaweka AC. Marejesho approx 6.5m kwa mwezi kwa mwaka 1. hakikisha kila cku unapata takriban laki 2.5 ili upate 7.5m kwa mwezi. jitahd wafanyakaz wawe wanalipwa kwa pesa itakayotokana na biashara ndogondogo za hapo kv vinywaj na misosi ili na ww ubaki na angalao 1m ya kukupoza ktk huo mwaka mmoja wa maumivu ya marejesho. angalizo: inatakiwa eneo lako liwe na mzunguko wa wasafiri na wachepukaji

Mkuu biashara ni rahisi kiasi hicho? kulipa 6.5M Kwa mwezi atafilisiwa tu na bank, haiwezekani uwe unajaza room zote kila siku labda kama itakuwa karibu na stendi ya mabasi
  • vipi hotel levy atalipaje?maana hapo ni palefu kidogo manispaa wasumbufu.
  • Bill za umeme kama itakuwa na Ac na heater
  • Maji safi kama yatakuwa yakununua kwenye maroli
  • Maji machafu je kuvuta kila week
Ni rahisi kukadilia kuwa kila siku utapata kiasi fulani lakini kiuhalisia siku nyingine utakosa watu kabisa hapo ndo utaona ugumu wa kulipa mkopo Bank.
Hii biashara kama huna mtaji unategemea mkopo bank haifai garama za uendeshaji ni kubwa na ushindani wa biashara pia mkubwa usitegemee ukope bank biashara hii ikutoe fasta ujue umeumia.
 
Habari wana jamvi....
Nina nyumba ambayo wakati naendelea na michakato nikapata wazo la kuibadilisha matumizi iwe lodge. Ningependa tupeane mawazo mbalimbali jinsi biashara hii inavyofanyika,hasa mapato yapatikanayo kila siku. Kwa mfano kama kwa mfano napata 50,000 per day je natakiwa nizichukue nizi bank mwenyewe au vizuri ni kusubiri baada ya siku 2 au 3 au 7? Na vp naweza kudhibiti wizi na udanganyifu wa wafanyakazi na mengineyo. Na vp kuhusu idadi ya wafanyakazi wanaohitajika kwa lodge ya vyumba 7 mpaka 8? Tushauriane
 
ni nayo yangu lah! inanipasua ubongo! balaa ispokuwa mara utakapoianzisha sahau kukosa elfu 10/20/30 mfukoni pia ni jinsi gani utaweza kudhibiti wafanyakazi wako,maana vitanda havisemi kaka! sio kama utaweza fanya stocking kama bia/tatizo kuibiwa au ukae hapo ambacho ni kitu kigumu sana! kwa mwangaikaji!
 
Back
Top Bottom