Msaada: Biashara ya Nyumba ya Wageni (Guest House) imekaaje?

Niliwahi Kufanya Kazi Guest Moja Hapa Dar Kabla Sijajishikiza Huju Mkoani:

Yule Mama Alikuwa Anatubana Hivi.

1. Asubuhi Saa 12 Kamiki Anataka Umtumie Report Yenye IDADI YA VYUMBA NA NAMBA ZAKE, IDADI YA MASHUKA MACHAFU, IDADI YA SABUNI ZIKIZOBAKI NA UNIT ZA UMEME ZILIZOBAKI.

2. Anampigia Mlinzi Akitoka Anamuuliza Kama Kuna Mtu Aliingia Usiku.

3. Anampigia Mfua Mashuka Anamuulza Kafua Mangapi

4. Anapiga Surprise Kama Zote, Unashangaa Anakupigia Mchana Anakuuliza Umeuza Vyumba Vingapi.

5. Anamtuma Snitch Aje Apange Chumba Then Anakuulizia Kama Hicho Chumba Kilitoka.

ALL IN ALL NILIKUWA NAMPIGA VIZURI, YEYE AKIPATA 150K MIMI NINA 50K

Baadae Ndio Akapata Mbinu Ambayo Ilimsaidia Kuziba Kabisa Mianya Ya Sisi Kupiga Ndio Nikaamua Kusepa Pale

Aliweka CCTV Camera Milango Yote Na Kwenye Korrido, Halafu Zikawa Connected Kwenye Router So Zipo Live Moja Moja Kwenye Screen Take, So Hakuna Tena Utapeli, Yaani Yupo Live Masaa 24 Anaona Guest Yake Kutokea Nyumban Kwake Gomz.

NA HII NDIO NJIA PEKEE YA KUZUIA KUPIGWA KWENYE BIASHARA YA GUEST.

Kwa uzoefu wako,watumiaji wengi wako interested na aina gani ya vyumba (self au vya kawaida) au mradi chumba kipo basi.

Nafikiria kuinvest uswahilini ambako hakuna wageni bali wachepukaji tu,self or vya kawaida ndo vitafaa?
 
Watu wanataka SELF Na Viwe Cheap, Usalama Wao Na Privacy I Mean Milango Ya Nyuma Iwepo Ili Wasionekane Sana Na Pia Customer Care Inatakiwa Iwe Nzuri Umpate Mtu Mchangamfu Mwenye Lugha Nzuri.
 
Hata wakij n cheti cha ndoa utathibitishaje kuwa ni chai wakati cheti hakina picha za wanandoa.
 
Mwambie muhudumu kila tukio arekodi kwenye kitabu afu mzoeshe kumshitukiza na mwambie kila tukio utakalolikuta halijarekodiwa hata la fasta litamfukuzisha kazi
 
Achana nayo haikufai hiyo biashara.
Ili upate hela ni mpaka iendeshwe kihunihuni ndio utapata hela yaani namaanisha wale wanaopata hela huwa wanamezea tu kila wakionacho,yaani hata akiona mke wa jirani yake anaingizwa kwenye hiyo guest ananyamaza tu ili asiikose hela.
Ingekuwa ni hotel tena ambayo iko maeneo ya mjini hapo sawa ungepata wateja sahihi ambao ni halali.
 
Niambie ni Biashara gani Halali ambayo hakuna unyonyaji ?

Mfano lile nanasi unalonunua kwa mkulima kwa Tshs 1000/= au shambani mtu ana-bargain kwa Tshs 400/= Je ni halali kumpa huyu mkulima hivyo visenti kwa shughuli aliyofanya kwa miezi kadhaa....

In short dunia ni dog eat dog..., bora huyu ana-provide mandhari ya watu ku-enjoy kitu natural kuliko yule anayewanyangaya nyuki chakula chao na malkia wao na watoto wao tena..., kwa kuwauwa baadhi (eti anajiita mfugaji..., kwani angewaacha wangekufa)!!???
 
Mbali na overheads za kawaida (ambao nadhani unazijua) moja ya gharama kubwa sana nyingine ni ya wadau wa TRA..., ngoja nikupe pdf hapo chini ya hao wadau
 
Attachments

  • The Hotels Act.pdf
    121.3 KB · Views: 32
Back
Top Bottom