MSAADA: Betri ya simu inasumbua.

worms

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
839
1,000
Habari Jukwaa la Tech.

Ndugu zangu nina tatizo la betri katika simu yangu Samsung Note 3 kila baada ya miezi minne betri linakuwa limechoka mbaya halikai kabisa na chaji... nimenunua betri mpaka nimechoka hali ni tete hadi nimeanza ichukia hii simu...

Nitapataje betri nzuri? Naomba mnisaidie hata kama betri hilo itahitajika kununuliwa mtandaoni hamna shida ilimradi nipate betri imara na linalotunza sana chaji..

Kwa sasa simu yangu haimalizi masaa matatu inazima...

Mara zote nikinunua betri mpya inakuwa vema mwanzoni lakini baada ya miezi miwili inakuwa ishaanza poromoka katika ufanisi na ikifika miezi minne inakuwa sawa na kuwa na Laptop desktop( haikai kabisa na chaji).

Nisaidieni ndugu zangu najua wadau wengi pia wa samsung watakuwa wanapitia haya kwani ni kama ugonjwa wa samsung zote upande wa betri.

Karibuni sana wadau...!
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
35,462
2,000
Karibu TECNO mkuu.


Naelekea mwaka wa pili tangu niinunue mambo swafii kabisa
 

worms

JF-Expert Member
Jul 29, 2017
839
1,000
Karibu TECNO mkuu.


Naelekea mwaka wa pili tangu niinunue mambo swafii kabisa
Asante ndugu nilikuwa huko nikahamia Samsung changamoto ni hiyo ya betri hasa vitu vingine vipo poa kabisa.............

Nataka nipate njia kwanza ya kutibu hili tatizo ikishindikana nitarudi huko.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
35,462
2,000
Asante ndugu nilikuwa huko nikahamia Samsung changamoto ni hiyo ya betri hasa vitu vingine vipo poa kabisa.............

Nataka nipate njia kwanza ya kutibu hili tatizo ikishindikana nitarudi huko.
Poapoa mkuu.

Karibu tena!

Ila ukumbuke kuwa kiungo kimoja kikipata jeraha maumivu ni mwili wote
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom