Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,293
- 2,623
๐ฏ๏ธ Leo nakupa taarifa kuhusu simu hii ya Samsung Galaxy s25 Edge ni simu ambayo kama utaniambia ni kwanini usinunue basi nakupa taarifa zake sio kwamba haifai kuitumia hapana ila hii simu ina changamoto kadhaa.
๐ฏ๏ธ Najua watu wengi wanapenda kutumia simu ambayo ni nzuri Yani ukitoa pesa yako basi unataka simu ambayo kamera yake ni nzuri, storage ya kutosha, betri imara nk lakini kwanini usinunue hii simu ๐.
๐ Simu hii imetoka miezi kadhaa iloyopita lakini changamoto ya kwanza Betri lake ni dhaifu sana sijui kwanini, yani ina 3900mah lakini haikai na chaji ripoti inaonyesha watu wengi wanalalamika betri lake ni dhaifu sana halikai na chaji ๐.
๐ Kamera yake sio tuliotegemea , Samsung ni wazuri kwenye kamera lakini kwenye S25 Edge kamera yake sio tuliotegemea kabisa haitoa picha nzuri kama tulivyotarajia yani ile ubora wa picha kwa bei ya hii simu sio nzuri kabisa.
๐ Inapeleka chaji pole pole wengi watu wanalalamika unapochaji hii simu inapeleka chaji pole pole kwani simu hii kwa gharama inayouzwa hatujategemea spidi ya uingizaji chaji wake hiko slow ๐.
๐ฏ๏ธ Samsung ni brand nzuri lakini kwenye hii toleo la Samsung Galaxy s25 Edge sio nzuri kutumia haswa gharama yake ni dola $1,100 sawa na tanzania shilingi 2.7milioni ni bora ununue s25 ultra tu kuliko kutumia Edge๐.