Msaada: Basi zuri Moshi - Dar

Msaada: Basi zuri Moshi - Dar

Kaka Joni

Member
Joined
Oct 1, 2013
Posts
25
Reaction score
16
Kwa wale ambao huwa mnasafiri mara kwa mara kati ya moshi/arusha - dar hebu nisaidieni ni basi gani zuri kwa sasa kusafiria? Nimesafiri safiri na kilimanjaro exp na dar exp naona kama yameanza kuchokachoka hivi.. Nategemea kusafiri wikiendi hii na familia yangu na nataka gari comfortable / luxury maana nimechoka kweli hapa nilipo. Ntashukuru wadau..
 
Yapo mengi mkuu. Dar exp, KLM, mtei....yote safi hayo
 
Mi sitaki basi linalotimua mbio. Nataka basi tulivu la starehe ambalo linajali usalama wa raia.

Nakushauri upande Fastjet kwani barabara toka Korogwe hadi Himo ina diversion na lami imechoka utafika umekoma
 
panda Ngorika ya kwanza, tunaiita kiberiti

Mkuu MUSSOLIN naona unataka kumpandisha ndugu yetu kwenye B-52Bombers kinguvu,ungempa kwanza pre-conditions za kupanda hilo Dege la Kaskazini a.k.a Mfalme na Mwamba wa Kaskazini. Kuna Mzee mmoja alilipanda hilo tulipofika Njia Panda Segera aliomba poo mwenyewe akashuka,Chezea Ngorika Dume weye....
 
Mkuu hao wanaokushairi kupanda Fastjet hawana hoja na wanataka kukuongezea gharama zisizo na ulazima,kuna usafiri wa ardhini ni nafuu na unaokoa muda kuliko hiyo FastJet,kamata zile Hiace zinazopeleka Magazeti Moshi na Arusha ni nafuu,comfortable na zinajali muda sana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom