Haikuwa dhamira yangu kumsaliti Uncle wangu, namuheshim sana,
lakini kutokana na vituko vya Aunt kunizidia ndipo nikajikuta nimetenda naye tendo.
Ikawa ngumu kuuacha mchezo huo kutokana na kile nilichokikuta kwake, nikajiona mshamba wa mapenzi kwa upya wa huba zake kwangu kila wakati.
Mwisho sikuutambua, mpaka ilipofika wiki iliyopita aliponiambia kwamba ana mimba yangu, na ni hakika na kweli kwamba yaweza kuwa yangu,
Anataka kuitoa, jambo ambalo naliona ni dhambi kubwa zaid kwa Mungu, yatosha dhambi ya kwanza,
Lakini pia nahofia ndoa yake na Mjomba wangu, itakuwaje atapojua kwamba mtoto si wake,
naombeni ushauri wenu tafadhari,
Jamani! Hivi nini maana ya heshima? Unasema unamuheshimu sana huyo mjomba then how come umezini na mkewe?
Listen to me very careful. Maandiko yanasemaje kwa dhambi kama yako. Maana hapa Jf naona mara nimetembea na mama mkwe, mara shemeji katembea na mke wangu nk
Maandiko yanasema hivi:
Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, naam, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mtu mume aziniye, na mwanamke aziniye,hakika watauawa.
Na mtu mume atakaye lala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauwawa; damu yao itakuwa juu yao
Na mtu mume akilala na mkwewe mwanamke wote wawili hakika watauawa, wamefanya yaliyo machafuko, damu yao itakuwa juu yao
Tena mtu mume akilala na mtu mume, kama alalavyo na mtu mke, wote wawili wamefanya machukizo, hakika watauawa damu yao itakuwa juu yao
Tena mtu mume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu,watachomwa moto yeye mume na hao wanawake pia.
Tena mtu mume akilala na mnyama hakika atauawa, nanyi mtamuua huyo mnyama
Tena mtu mume akimwoa binti ya babaye au binti ya ***** na kuuona utupu wake na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mume ni jambo la aibu. Watakatiliwa mbali mbele ya macho ya wana wa watu wao
Tena tu mume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake, watauchukua uovu wao, watakufa bila kuzaa mwana
Tena mtu mume akimtwaa mke wa nduguye, ni uchafu, ameufunua utupu wa nduguye, hao wztakuwa hawana wana. Basi zishikeni amri zangu zote na hukumu zangu zote na kuzifanya, ili lwamba nchi ninayowapeleka ninyi kukaa isiwatapike. ( mambo ya walawi 20:11-22)
Umefunua utupu wa mjomba then unasema unamuheshimu! Nimesikitika.
Wacha nilale maana sijui dunia inaenda wapi. Dear God have mercy on us.