Msaada: Atakayefanikisha hili namlipa USD 100

protogonist

Senior Member
Feb 27, 2018
179
226
Habari wakuu,

Nimepata tatizo ambalo kimsingi sio kubwa sana na pia sio dogo sana, ni la wastani. Lakini kwa wahusika ni jepesi sana, linaweza tumia dakika 1 kuwa solved.

Ipo hivi: Nina Gmail account yangu ambayo huwa naitumia katika shughuli zangu muhimu sana siku moja nikatumiwa verification code za kureset password bila ya Mimi kureset password nikashtuka nilichofanya nika-change password haraka haraka, tatizo ndipo liliponikuta.

Nikaitumia kama week moja mbele jambo la kushangaza siku moja naingia nikakuta imeji-logout yenyewe nikajisemea haina shida nita-login upya, sasa mzozo ukaja kwenye password -- niliyoiweka mpya siikumbuki.

Ikumbukwe hii account ina recovery phone number yangu ambayo ninayo. Nikajaribu kureset verification code zinafika lakini inagoma ku-reset. Wananiambia niweke Gmail ambayo wata-contact na mimi later na nikiweka Gmail wananiambia wanashindwa ku-verify kama account ni yangu

Tatizo hili limenitokea toka October lakini hadi leo nimeshindwa kuirejesha na naihitaji sana. Nimejaribu kufatilia kwa Wana IT wa Tz lakini wapi; na katika pitapita zangu katika support forum yao wanasema account kila ikiendelea kujaribiwa ku-reset ni sawa sawa pingu kila unavyojaribu kuitoa ndio inazidi kukaza.

Nimeshajiunga vifurushi vya kimataifa kama vya USA,Canada, UK na vya nchi nyingine ili niweze kuwapigia customer care katika nchi hizo lakini hawapokei; nimeambulia hola! Leo pia nimejiunga na vifurushi vya Kenya kupiga customer service ya Kenya lakini hawapokei.

Jambo nililofikiria kutembelea Google House kwa East Africa ipo Kenya na Kenya kwenda ndio hadi passport hizi mpya za kielectroniki na mimi nina zile za zamani. Nikifikiria kuanza ku-apply passport muda unazidi kwenda sana nahitaji kwa siku mbili tatu hizi.

Ombi langu kwa mtu yoyote ambaye yupo Kenya au nchi nyingine ambaye anaweza kunisaidoa kutembelea tawi la Google na kuniwakilisha nitampa kiasi tajwa hapo juu kama Asante njia za malipo PayPal, Bitcoin au Payoneer.

NOTE: SIHITAJI MTU WA KUIRESET YEYE MWENYEWE BILA KUTEMBELEA GOOGLE AU KAMA KUNA MTU AMBAYE AMEWAHI KUWASILIANA NA GOOGLE UNAWEZA NISAIDIA NJIA ULIYOTUMIA KUWASILIANA NAO PIA KAMA KUNA MTU AMBAYE AMEPATA TATIZO KAMA LANGU NA KULISOLVE NAOMBA MSAADA





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiini cha tatizo la account yako ni "hackers" ambao baada ya kukupa link ya kureset password uliingia chaka na kuwapa full access ya account yako. Huyo mtu bila shaka is behind all these na anajaribu kuextract every resources at his disposal using your account. The solution hipo na tena ni simple sana huitaji kuwahusisha personnel wa google physically.

Google kwani hata response yao ni online hawataki physical contact. Kwahiyo hayo mambo sijui ya kutembelea office zao unajipotezea muda. Niliwahi kuwatatulia wengi shida kama hiyo and trust me on this. Mimi Niko Dar Tanzania. Njoo PM!
 
Kiini cha tatizo la account yako ni "hackers" ambao baada ya kukupa link ya kureset password uliingia chaka na kuwapa full access ya account yako. Huyo mtu bila shaka is behind all these na anajaribu kuextract every resources at his disposal using your account. The solution hipo na tena ni simple sana huitaji kuwahusisha personnel wa google physically. Google kwani hata response yao ni online hawataki physical contact. Kwahiyo hayo mambo sijui ya kutembelea office zao unajipotezea muda. Niliwahi kuwatatulia wengi shida kama hiyo and trust me on this. Mimi Niko Dar Tanzania. Njoo PM!
Mkuu nimekuelewa na Asante kwa ushauri labda niongeze kuwa nilichange password kwenye my account kule hlf pia nikijaribu kureset recovery phone number yangu bado ipo kwenye account....
Nakuja PM

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NOTE:SIHITAJI MTU WA KUIRESET YEYE MWENYEWE BILA KUTEMBELEA GOOGLE AU KAMA KUNA MTU AMBAYE AMEWAHI KUWASILIANA NA GOOGLE UNAWEZA NISAIDIA NJIA ULIYOTUMIA KUWASILIANA NAO PIA KAMA KUNA MTU AMBAYE AMEPATA TATIZO KAMA LANGU NA KULISOLVE NAOMBA MSAADA

Hiyo imenikatisha tamaa sana, ngoja nikuache, ila nime hack sana Gmail hizi, hiyo kurudi ni rahisi tu ingawa hutaki mtu unataka wa kwenda Google house okay kila la kheri pia dau lako dogo Fanya 250.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom