Msaada: Atakayefanikisha hili namlipa USD 100

mkuu mimi naweza kukusaidia lakini ndo hvyo sio kimasiliano kama unavyosema mpaka uwasiliane na google,tunakaa pamoja kwenye computer yako na kuanza mambo ya ku reset gmail yako kwasababu hata mi nishawahi kukumbana na tatzo kama lako,lakn niliweza kulifanikisha kuna process unatakiwa uifuate.
Mkuu unaweza kunifanikishia hili?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu mimi naweza kukusaidia lakini ndo hvyo sio kimasiliano kama unavyosema mpaka uwasiliane na google,tunakaa pamoja kwenye computer yako na kuanza mambo ya ku reset gmail yako kwasababu hata mi nishawahi kukumbana na tatzo kama lako,lakn niliweza kulifanikisha kuna process unatakiwa uifuate.
Mkuu naweza kuja PM
 
MastaKiraka, Nikiweka hiyo Gmail ya kucontact wanachofanya wanatuma code kwenye ile Gmail halafu nikija nikiingiza kwenye acc yenye tatzo wanasema wanashindwa kuverify kama account ni yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
hii ilisha nikuta tena mimi recovery options zilikuwa tatu. Namba moja ya simu, email moja ya google na nyingine yahoo. Kote huko walikuw wanatuma codes zao kwa ajili ya kuveryfy ila ukiziingiza wanakupa ujumne huo uliouandika hapo. Nilisubiri sana kwa matumaini kuwa system huwenda ikakaa sawa lakibi hakuna kilichobadilika. HAKUNA NJIA NILIYOTUMIA KUPATA ACCYTENA KWENYE ACC YANGU ZAIDI YA KUKUMBUKA PASSWORDS. THANK GOD SIKUKUTA MALICIOUS activity KWENYE ACCOUNT YANGU. Kila la kheri mkuu
 
Hiyo kazi yako si ngumu sana but umeshaweka angalizo kuwa mtu lazima aende Google center . Kwa hapo Mimi siwezi kukusaidia
 
Nitakusaidia.

Naomba vitu vifuatavyo email yako na password uliyokuwa unatumia kabla ya kubadilisha, namba ya simu na email uliyokuwa umeunganisha kama recovery, naomba na aina ya simu yako uliyokuwa umesign in nayo, naomba na tarehe uliyofungulia hiyo gmail kama una kumbuka, NiPM hivyo vitu faster uandae na hiyo hela faster siku moja itakuwa tayari.
 
Sijafanikiwa kusolve hili tatzo hadi leo
 
Habari wakuu,

Nimepata tatizo ambalo kimsingi sio kubwa sana na pia sio dogo sana, ni la wastani. Lakini kwa wahusika ni jepesi sana, linaweza tumia dakika 1 kuwa solved.

Ipo hivi: Nina Gmail account yangu ambayo huwa naitumia katika shughuli zangu muhimu sana siku moja nikatumiwa verification code za kureset password bila ya Mimi kureset password nikashtuka nilichofanya nika-change password haraka haraka, tatizo ndipo liliponikuta.

Nikaitumia kama week moja mbele jambo la kushangaza siku moja naingia nikakuta imeji-logout yenyewe nikajisemea haina shida nita-login upya, sasa mzozo ukaja kwenye password -- niliyoiweka mpya siikumbuki.

Ikumbukwe hii account ina recovery phone number yangu ambayo ninayo. Nikajaribu kureset verification code zinafika lakini inagoma ku-reset. Wananiambia niweke Gmail ambayo wata-contact na mimi later na nikiweka Gmail wananiambia wanashindwa ku-verify kama account ni yangu

Tatizo hili limenitokea toka October lakini hadi leo nimeshindwa kuirejesha na naihitaji sana. Nimejaribu kufatilia kwa Wana IT wa Tz lakini wapi; na katika pitapita zangu katika support forum yao wanasema account kila ikiendelea kujaribiwa ku-reset ni sawa sawa pingu kila unavyojaribu kuitoa ndio inazidi kukaza.

Nimeshajiunga vifurushi vya kimataifa kama vya USA,Canada, UK na vya nchi nyingine ili niweze kuwapigia customer care katika nchi hizo lakini hawapokei; nimeambulia hola! Leo pia nimejiunga na vifurushi vya Kenya kupiga customer service ya Kenya lakini hawapokei.

Jambo nililofikiria kutembelea Google House kwa East Africa ipo Kenya na Kenya kwenda ndio hadi passport hizi mpya za kielectroniki na mimi nina zile za zamani. Nikifikiria kuanza ku-apply passport muda unazidi kwenda sana nahitaji kwa siku mbili tatu hizi.

Ombi langu kwa mtu yoyote ambaye yupo Kenya au nchi nyingine ambaye anaweza kunisaidoa kutembelea tawi la Google na kuniwakilisha nitampa kiasi tajwa hapo juu kama Asante njia za malipo PayPal, Bitcoin au Payoneer.

NOTE: SIHITAJI MTU WA KUIRESET YEYE MWENYEWE BILA KUTEMBELEA GOOGLE AU KAMA KUNA MTU AMBAYE AMEWAHI KUWASILIANA NA GOOGLE UNAWEZA NISAIDIA NJIA ULIYOTUMIA KUWASILIANA NAO PIA KAMA KUNA MTU AMBAYE AMEPATA TATIZO KAMA LANGU NA KULISOLVE NAOMBA MSAADA

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna email yangu nilikuwa nimesahau password tangu mwaka 2015 na wakaniambia hivyo wameshindwa kuverify account yangu, lakini mwezi Agosti mwaka huu (2020) nikaijaribu kulogin ikakubali.
 
Hili tatizo nalijua na nimeshawahi kulisove kabla.

Nikutoe hofu inawezekana ku-solve, hackers huwa wana gain access ya email yako kisha wanaweza kui-delete na pia wanachukua access ya YouTube channel yako. Wanabadilisha jina na content.

Kama tatizo ni hilo ni PM.
 
Back
Top Bottom