Msaada: Anayejua darasa zuri la Kichina jijini Arusha

raslimali

JF-Expert Member
Nov 4, 2014
1,344
1,013
Habari wakuu,

Naomba msaada kwa anayejua lilipo darasa la lugha ya Kichina Arusha na mawasiliano ya simu ikiwezekana. Nataka nimpeleke mdogo wangu kwa miezi michache wakati anasubiri matokeo ya kidato cha sita.

Natanguliza shukrani.
 
Ilboru sekondari Wana SoMo la kichina, bila shaka Wana walimu pia. Jaribu kuuliza hpo utapewa mwongozo mkuu
 
Miezi michache haisaidii kabisa kichina ni kigumu angalau mwaka sio rahisi kabisa inahitaji mtoto awe serious hasa miezi 4 ya mwanzo baada ya miezi 6 ndio ataanza kuelewa kuandika na kujielezea kiasi.

Kwa wiki angalau afundishwe jumla ya masaa 9 na nyumbani kila siku atumie walau saa 1 kufanya exercise za book 1 nimeweka material nyingi za chinese tafuta huo uzi utazipata

Kama ni mfatiliaji pia ubalozi wa china wanatoaga fursa na mafunzo baadae unapata udhamini wa kwenda kujifunza lugha vyuo vya China.
 
shukrani mkuu ngoja niangalie huo uzi.
 
Back
Top Bottom