Ndugu marafiki nahitaji ushauri wenu, nimefanikiwa kujenga nyumba yangu eneo fulani mkoani Mbeya.
Lakini kuna jirani yangu ambaye anatumia eneo la kiwanja changu ili aweze kufika kwake na ni mbele ya nyumba yangu.
Nimeshamwambia kwa mdomo na kwa maandishi kwamba natahitaji kutumia eneo hilo , hivyo atafute sehemu nyingine ya yeye kuweza kufika kwake, lakini naona kuna aina ya kiburi na uchonganishi kwa majirani wengine kwamba namzibia njia.
Kwa sasa ninapoandika na kuomba ushauri kwenu nipo masomoni Muhimbili, lakini kabla ya kuja hapa nilishamwandikia maelezo ya kutumia eneo hilo kwa mwaka 2016 mwaka ambao masomo yangu nitakuwa nimemaliza.
Lakini bado ninapokuwa likizo sioni jitihada anazozifanya kutafuta njia mbadala, ndugu zangu sitapenda kufanya jambo bila kuwa na maamuzi sahihi hivyo basi nalileta kwenu nipate ufumbuzi.
Ahsante