Msaada: Anatumia kiwanja changu kuweza kufika kwake

Msaada: Anatumia kiwanja changu kuweza kufika kwake

Wkt najenga Kuna jirani yangu alinizibia njia kwa kulima,
Mungu saidia kuna kiwanja kilikuwa na upenyo uliokuwa umefichwa na vichaka ,
nikaibua njia ujenzi ukaendelea,
baadae nikambembeleza mwenye hicho kiwanja akakubali kuniuzia kwa bei mkasi,
sasa nimeunganika brbrn kuliko jiran roho mbaya,
nishahamia,
jiran roho mbaya bado hajakamilisha na bado amepanga,
nishachimba kisima,
na kuvuta umeme tyr,
hayo yote jirn roho mbaya hana,
na akihamia ....
Pia kwa ss anatakiwa apite kwangu ndo njia ya karb kw miguu,
pia kuna jiran ambaye ndoo walikuwa wakishirikiana naye keshazibwa huwa anapita uwanjan kwangu na anategemea apite kwangu,
Suala hilo litafakari kwa umakini sana, ingawa majiran wengi ni washari sana.
 
Huyu jamaa atakuwa muhaya maana hao.kwa ardhi.ni balaa Mm Nina Jirani yangu alinipeleka hadi.kwa mjumbe kisa gari LA mchanga lilipita kwenye kiwanja chake na ambacha hata hajaanza kujenga looh
 
Tatizo ni kuvunja sheria wakati wa kujenga hata kama sehemu haijapimwa inabidi kistaarabu /kisheria kila mtu kuacha mita moja na nusu kutoka kwenye mpaka ndio ajenge hii inaacha barabara na hata moto ukitokea fire inaweza kufika ila sehemu nyingi hilo halifuatwi kwahiyo kisheria haruhusiwi kupita kwako ila je na wewe ulivyojenga umeacha mita moja na nusu (hio ndio njia)
 
Saitot

Mkuu pole, ila kumbuka kuwa ni jambo la kheri sana kuishi kwa amani,furaha na upendo na jiranì zako. Inavo onekana kujenga mazingira ya uhasama ama amani viko mikononi mwako. Kama kuna uwezekano wa kumwachia jirani yako njia bila ya wewe kuathirika sana ni jambo Mungu anapenda, fikiria ni wewe umezibiwa njia. Naongea kwa uzoefu ktk hili, Binafsi nimewahi kumkatia jirani yangu kipandn cha mbele ya kiwanja changu jirani kwa ajili ya kupitisha gari lake bila malipo yoyote na sijawahi jutia uamuzi wangu. Gombana na ndugu sio jirani. Majirani ni muhimu ndo maana hatununui na kujenga maporini japo ardhi ni ya kutosha huko. Ongea vizuri na majirani zako mtatue kero zenu na huo ndo ukokamavu.
 
Last edited by a moderator:
Uwe mpole tu Mkuu! Ardhi ni mali ya Rais wa Tanzania ambaye anaweza kubadilisha matumizi ya hicho kiwanja na kuweka mradi wowote ule.
 
Saitot

Jisikie fahari kumuwezesha binadamu mwenzako kufanikiwa kwa jambo lolote lile, na MUNGU atakubariki kwa kujitoa kwako,nibora kutoa kuliko kupokea.

Ongea nae, ukiona anauwezo wa kununua muuzie kama hanauwezo muachie kiasikidogo cha ardhi yako atumie kufika kwake hauta pungukiwa na chochote.
 
Last edited by a moderator:
Kuweka ukuta wa uzio pekee si suluhu ya kudumu bali utakuwa mbuni aliechimbia kichwa chini akidhani amejificha.
Navaa viatu vya muhusika kwa kuwa nami hali kama hiyo imenikuta wakati nikiendelea na hatua za ujenzi japo maeneo ninayopita kwa jirani zangu hayajaendelezwa bado.
Ufumbuzi ni kuongea na jirani yako,tafuteni uongozi wa mtaa wenu wekeni taratibu za kila mtu kuacha ile 1.5 M kila mtu na jirani yake mbona mtapa 3 M ambayo ni barabara ya kutosha na mtakuwa mmetafuta ufumbuzi wa kudumu.
Wasalaam
 
Mimi kuna jirani alinitenda kwa kweli sina mswalie mtume tena na jirani katika ardhi. Huyo mama baada ya mimi kuhamia kwangu niliishi vizuri sana na familia yake. Hawakuwana umeme na walikuwa na wagonjwa ambao dawa zinatakiwa zikae katika friji, maji hawakuwa nayo hata mikingio ya mvua hawana. Wao ni sare za shughuli na kujipamba, vyote walinitegemea mimi ikiwamo msaada wa fedha.

Hivi karibuni wakamuuzia mtu kipande cha ardhi wakamuona ana pesa sana wakasahau fadhila zote wanamwambia ajenge ukuta hadi ugote ktk ukuta wangu. Nikapeleka suala kwa mjumbe kumbe ni wana "chama lao" wenzake, wakaanza kunikandamiza. Ikabidi nitumie ubabe wakabomoa. Nimemchukia yeye hilo lijumbe letu na hilo lichama lao nikiona rangi zake nabanwa mafua. Jirani wengine utatamani ubebe nyumba kwa greda uhame...
 
Mkuu pole, ila kumbuka kuwa ni jambo la kheri sana kuishi kwa amani,furaha na upendo na jiranì zako. Inavo onekana kujenga mazingira ya uhasama ama amani viko mikononi mwako. Kama kuna uwezekano wa kumwachia jirani yako njia bila ya wewe kuathirika sana ni jambo Mungu anapenda, fikiria ni wewe umezibiwa njia. Naongea kwa uzoefu ktk hili, Binafsi nimewahi kumkatia jirani yangu kipandn cha mbele ya kiwanja changu jirani kwa ajili ya kupitisha gari lake bila malipo yoyote na sijawahi jutia uamuzi wangu. Gombana na ndugu sio jirani. Majirani ni muhimu ndo maana hatununui na kujenga maporini japo ardhi ni ya kutosha huko. Ongea vizuri na majirani zako mtatue kero zenu na huo ndo ukokamavu.

Well said. Na kwa hicho ulicho mfanyia huyo jirani naamini huwa anakuombea mazuri kila siku kwa Mungu. UTAJIRI NI KUTOA NA SIO KUONGEZA.
Ukiona wewe una mali nyingi halafu bado huridhiki basi ujue wewe bado masikini.
 
Back
Top Bottom