Msaada: Aliyewahi kufikia hatua hii- Alitokaje?

Msaada: Aliyewahi kufikia hatua hii- Alitokaje?

Mkuu nimepitia hicho kipindi, kuna wakati nikashawishiwa na mama mmoja ambaye ni marehemu
kwa sasa niende nchi fulani kufuata mzigo (unga) kwa ahadi ya kitita cha tsh milioni 11, nilikuwa
nakaribia kukubali lakini wakati nikitafakari yule mama akakumbwa na umauti.

Nilitamani kuuza maji barabarani lakini aibu kilikuwa kikwazo kwangu, hatimaye nikapata mbinu
ambayo namshukuru Mungu ilinitoa sana, tena sana. Nilirudi kijijini nikaonana na wataalamu wa
tiba za asili..... naomba unielewe hapa ili kuweka mambo sawa sio waganga wa kienyeji ni wataalamu
wa tiba za asili. Ndiyo.... nikajikuta mpango wangu huo ukiniwezesha kununua kiwanja hapa Dar.
. hadi
kufanikiwa kujenga.
Utumie vizuri muda wa asubuhi kwa kutafakari nini cha kufanya..... usichoke kila kitu kinaanzia
kwenye fikra hata ukiiona ghorofa kubwa vipi lazima itakuwa imetoka kwenye fikra za mtu mmoja kwanza
hata kama ni ghorofa ya serikali, jumuiya n.k.
hapo kwenye blue..ilianza uza dawa ama walikufanyia dawa sijakupata mkuu
 
mpe ushauri wako kafikia mwisho wa uwezo wake!

Soma vizuri palagraph ya pili mstari wa kwanza "Anything u mention, nimejaribu bila mafanikio", HE NEEDS TO THINK POSITIVE, idea inaweza isifail, anaweza kufail mtekelezaji, ukianguka mara moja au mia haimaanishi kuwa usiamke, you get up and PUSH ON!
 
hapo kwenye blue..ilianza uza dawa ama walikufanyia dawa sijakupata mkuu

Hahahaha, GAZETI naona hataki kufunguka kwa faida ya wengi, labda ni moja ya masharti!
 
Last edited by a moderator:
pole sana mkuu. ni biashara gani umefanya, na umetumia njia gani? kuomba tu bila kuweka juhudi hutofanikiwa.
 
Pole sana Mkuu hasa hapo kwenye suala la ndugu kushangilia problems zako. Nakushauri uongee na Headmasters wa shule za private unaweza pata dili ndogo ya kupiga chaki (kufundisha) huku ukiangalia ustaarabu mwingine kuliko kuendelea kujifungia ndani. Hiyo itakukeep bize maana ukikaa sehemu moja lonely halafu una mawazo ya maisha magumu unaweza fika hatua ya kuchukua maamuzi magumu.

ikibidi anaweza hata "kupiga chaki" kwa kujitolea mfano mara mbili kwa wiki. akifanya kazi yake vizuri anaweza pata ajira ya kuanzia. pia katika kazi hiyo anaweza pata contacts muhimu zenye msaada kwake.
 
Pole mkuu....maisha mara nyingine hayako fair...ila komaa tu...ONE DAY YES
 
I feel sorry for you
Endelea kuomba tu mungu ni wawote leo nitakuweka kwenye maombi
 
Ujue..kuna watu humu hawajui shida. Wamezaliwa kwenye mapiza na masoseji. Huwezi elewa ninachosema au nilichoandika.
 
Mkuu,sasa wewe unamuomba MUNGU then unashinda ndani huku ukitarajia life linyooke! Are you serious?

Kama hujichanganyi utamaliza wachungaji tu.There's no miracles under the sun mkuu,halafu unadegree!
USHAIRI WANGU;Sio lazima ufanye kazi uliosomea mkuu mf teaching kunafursa za kuanzia kujipanga kimaisha.

Kila la kheri!
 
Mkuu nimepitia hicho kipindi, kuna wakati nikashawishiwa na mama mmoja ambaye ni marehemu
kwa sasa niende nchi fulani kufuata mzigo (unga) kwa ahadi ya kitita cha tsh milioni 11, nilikuwa
nakaribia kukubali lakini wakati nikitafakari yule mama akakumbwa na umauti.

Nilitamani kuuza maji barabarani lakini aibu kilikuwa kikwazo kwangu, hatimaye nikapata mbinu
ambayo namshukuru Mungu ilinitoa sana, tena sana. Nilirudi kijijini nikaonana na wataalamu wa
tiba za asili..... naomba unielewe hapa ili kuweka mambo sawa sio waganga wa kienyeji ni wataalamu
wa tiba za asili. Ndiyo.... nikajikuta mpango wangu huo ukiniwezesha kununua kiwanja hapa Dar.. hadi
kufanikiwa kujenga.
Utumie vizuri muda wa asubuhi kwa kutafakari nini cha kufanya..... usichoke kila kitu kinaanzia
kwenye fikra hata ukiiona ghorofa kubwa vipi lazima itakuwa imetoka kwenye fikra za mtu mmoja kwanza
hata kama ni ghorofa ya serikali, jumuiya n.k.

kweli mdau, muda wa asubuhi ni mzuri sana kupata ufumbuzi wa matatizo ikiwa tu hujaamka na mning'inio.
 
Nipo Ng'wanuzi, Shinyanga

Pole sn Mkuu!

Mkuu Km utaweza jitahidi kupata nguvu ya pesa uende Dar, huko fulsa ni nyingi na mzunguko Wa pesa ni mkubwa kuliko huku kwetu bara! Km unaweza ukapata makazi Dar ni vema ukaenda huko na ukifika usichague kazi Km unatafuta. Kwani Ukipata kz yeyote ile kwanza itakupa uwezo Wa kukaa mjini Na pia itakupa connection mbalimbali. Kikubwa uweke malengo na uyatekeleze na uwajibike. Angalia kwa huko Dar starehe ni nyingi sn Km utapitiwa utashindwa kutimiza malengo yako!

Km ukifika Dar kwa lengo moja na ukawajibika vizuri. Ni miaka mitatu tu utakua umepata msingi Kiasi!

Kwa mikoani Mkuu ni kugumu!

Mzunguko Wa pesa uko chini, nafasi za ajira sio nyingi Na ata mikopo sio mingi!
 
Pole ndugu, kwanza nakuomba katika kipindi hiki usijishughulishe na mambo ya ulevi kwani utaharibikiwa zaidi, pili kazana kumwomba Mungu utapata njia ya kutokea. Mimi nilipitia njia kama yako utafikiri umecopy, ilifika wakati hata nikiona mtu anatoa noti ya elfu moja nashangaa amepataje ila nilipoamua kumtegemea Mungu nilipata kazi na sasa hivi nina biashara zangu binafsi. Mtegemee sana Mungu.
 
Ntuzu. ..ushauri wako ni mzuri. Ila dar sio kwepesi namna hiyo. Nimekaa huko kwa mwaka mzima...mpaka nikaamua kubeba tofali ili niwe napata pesa ya kula na nauli. Maisha yalikua magumu sana. Ndugu wa Dar wengi ni wachoyo....vyakula wanaona kama unamaliza. Ndugu wa Dar hawapendi wageni kama mimi tegemezi. Wanataka ukienda kwao...ufanye shughuli na ue unarudi usiku sio kukaa kaa tu ovyo. Na ue na uwezo wa kula mtaani.
 
Back
Top Bottom