Kuna mkasa ulitokea nikaamini Tanzania hii bado Kuna watu waaminifu

Mr mutuu

JF-Expert Member
Jan 27, 2023
2,510
12,409
Huu mkasa ulitokea kama miaka miwili imepita, dogo wangu alivyomaliza chuo akapata kazi shirika Moja binafsi, akafanya huko kama miaka minne akaanza mazoea ya kunipiga vizinga Tabia ambayo alikua Hana, nikapigwa vizinga weeee mpaka nikachoka, mawazo yakanijia huyu dogo kaajiriwa na Kuna kipindi aliniambia mshahara ni 1.something, nikasema hapana huyo dogo atakua amepata jini(mwanamke) chuma ulete labda anahudumia ukoo wao mzima, nikatafuta siku nikamuita kumhoji ndo akaniambia taasisi Yao imeyumba muda tu yaani mishahara Wana kama miez 6 hawajalipwa Kila siku ahadi... Nikafatilia hili swala nikagundua ni ukweli nikamshauri atafute kazi sehemu nyingine au serikalini akaniambia sawa

Sasa kuna kipindi nafasi serikali zikatoka kada Yao, nikamshtua nikamwambia apply haraka haraka akasema poa, ikapita muda katika mihangaiko na story za hapa na pale nikaunganishwa na mtu flani alikua mkubwa kiasi serikalini kwenye Hio kada aliyokua anafanya kazi dogo, nikamuomba amsaidie dogo apate kazi, Jamaa bila kupepesa macho akaniambia live nimtafutie milioni cash ndo amsaidie( sipendi mambo ya rushwa ila sasa ndo nchi yetu hii Kila mtu anaelewa mkono mtupu haulambwi)

Dogo nikamshirikisha, akaniambia Kuna hela wamepewa anaweza kua na hio M lakini akawa anasema bro huo ni utapeli tutaibiwa tu acha kama ni riziki ntapata tu, nikamsihi sana atoe Hio hela maana aliyeni connect nae mbona ni mtu wangu wa nguvu sidhani kama anaweza kunifanyia ujinga, kishingo upande dogo akamtumia Hio hela jamaa....tena jamaa akatuaminisha mpaka akamwambia dogo achague kituo Cha kazi kabisa😃😃Post zinatoka hola, dogo hajapata, aisee huyu dogo ananiheshimu ila alikuja kua mbogo mpaka akanivunjia heshima, akawa ananituhumu tumempiga milioni yake😃,kuanza kufatilia jamaa nae ananiambia mbona sielewi nilishachombeza jina la huyu apate kazi sijui Nini kimetokea, nikasema hapa tushaingizwa town, nikalalamika tu kwa jamaa aliyeniunganisha na huyu mtu lakini nae akawa ananiambia mbona huyo hayupo ivo, dogo sasa, ikawa usumbufu mpaka home akawa ananisema nimempiga hela nikaona Shari za Nini ikapita muda nikamtumia Hio milioni yake.....

Nimekaa kama wiki 3 mbele, jamaa aliyepewa milioni akanipigia akaniambia anaenda Dodoma kikazi akifika huko atafatilia kwanini dogo hazapata post, akaniambia bro nipe tu akaunti yako nikupe hizo hela umpe mdogo wako asione kama tumemdhulumu wakati na yeye anatafuta bado hajajipata.... Kumbuka hapo mi nilishapotezea hii ishu na dogo nilishamlipa, nikatuma Hio acc kishingo upande nikajua hapa hakuna lolote

Kweli baada ya muda naona muamula umesoma aisee nilishangaa sana(kumbuka sikuwahi kumsumbua arudishe hiyo pesa).... Nimekaa kama siku 2 jamaa ananipigia ananiambia muulize dogo kama alishawahi kuomba kazi serikalini, nikampigia dogo akaniambia baada ya kumaliza tu internship aliomba kazi serikalini..... Nikamrudia jamaa akaniambia huyo mdogo wako ni mjinga sana ametupotezea muda bure....Kumbe huyu mbwiga(dogo) alishawahi kuomba kazi serikalini akapata, akaona kituo kipo Kijijini huko hakwenda kuripoti, kwa maelezo ya jamaa akadai system ilikua bado inasoma kama dogo alishapata kazi, nikamuuliza kwa io hawafanyi confirmation baada ya watu kuripoti ili hao ambao hawajareport system iwaondoe akaniambia haelewi kwanini imekua ivo, kumbe walivyoingiza jina la dogo likasoma kama tayari alishapangiwa kituo

Nikamuelezea dogo akaniambia ni kweli alipangwa mbali sasa akaona bado ana kazi hakuenda, jamaa akanishauri mwambie mdogo wako afatilie huku hili jina lake litoke huku la sivyo hatakaa apate kazi huku, dogo ananiambia bro nisaidie sasa , nikamwambia ushakua mtu mzima fatilia mambo yako mwenyewe maana ushafanya familia wajue mi ni tapeli

Jamaa nikaja mtumia laki 2 kiuungwana nikamwambia bro najua ulitumia hata na vocha, nimekumbuka hilo tukio maana dogo alikua ananiomba namba ya huyo jamaa ( ambayo kimsingi Sina nilishapoteza) na rafiki yangu aliyenipa ile connection na jamaa tumemzika mwaka huu mwanzoni(RIP).... Dogo namuelesha kua Sina namba zake naona ishakua lawama anahisi kama bado nimemind nambania
 
IAtafanya usaili sana na hata akipita, ikiingizwa namba ya CHETI chake Cha form IV taarifa zake zinakuja kwenye mfumo...atasota sana kupata kazi serikalini. Automatically mfumo utam-reject. Labda atafute private. Technolojia haiongopi mkuu.

Aende Utumishi wamshauri cha kufanya kuondoa hiyo kadhia.
 
IAtafanya usaili sana na hata akipita, kiingizwa namba ya CHETI chake Cha form IV taarifa zake zinakuja kwenye mfumo...atasota sana kupata kazi serikalini. Automatically mfumo utam-reject. Labda atafute private. Technolojia haiongopi mkuu.
Ndo jamaa aliniambia mwambie mdogo wako afatilie system itoe jina lake ila akaniambia hapo lazima atapigwa hela, na jamaa ni kama alikua hataki tena kufanya ishu za dogo maana aliniambia wote walionipa hela wamepangiwa vituo walivyoniomba kasoro huyu mdogo wako mjinga😃😃😃
 
Huyo jamaa haikuwa tabia yake lakini pengine aliheshimu connection iliyowakutanisha.

Ila namshukuru Mungu sijawahi kuhonga kwa sababu ya kazi japo katika harakati nishakutana na watu baadhi waliopewa upendeleo wa wazi..
Hivyo, Dear HR's, jueni mna moto wenu special wa kuwachomea maana kumnyima mtu nafasi anayostahili kwa ajili ya 500k au tamaa za ngono, ni ushetani uliopitiliza
 
Bongo nyoso mkuu, tunakua na mabosi ambao tunawafundisha kazi, niliwahi fanya kazi sehemu bosi mweupe kabisa walikuja wazungu kufanya project Fulani jamaa Kila akiulizwa kitu inabidi sisi ndo tutoe ufafanuzi, jioni mkiwa nae anacheka tu anawaambia vijana siwezi teseka na nyinyi mpo bado damu inachemka😃😃
 
Huu mkasa ulitokea kama miaka miwili imepita, dogo wangu alivyomaliza chuo akapata kazi shirika Moja binafsi, akafanya huko kama miaka minne akaanza mazoea ya kunipiga vizinga Tabia ambayo alikua Hana, nikapigwa vizinga weeee mpaka nikachoka, mawazo yakanijia huyu dogo kaajiriwa na Kuna kipindi aliniambia mshahara ni 1.something, nikasema hapana huyo dogo atakua amepata jini(mwanamke) chuma ulete labda anahudumia ukoo wao mzima, nikatafuta siku nikamuita kumhoji ndo akaniambia taasisi Yao imeyumba muda tu yaani mishahara Wana kama miez 6 hawajalipwa Kila siku ahadi... Nikafatilia hili swala nikagundua ni ukweli nikamshauri atafute kazi sehemu nyingine au serikalini akaniambia sawa

Sasa kuna kipindi nafasi serikali zikatoka kada Yao, nikamshtua nikamwambia apply haraka haraka akasema poa, ikapita muda katika mihangaiko na story za hapa na pale nikaunganishwa na mtu flani alikua mkubwa kiasi serikalini kwenye Hio kada aliyokua anafanya kazi dogo, nikamuomba amsaidie dogo apate kazi, Jamaa bila kupepesa macho akaniambia live nimtafutie milioni cash ndo amsaidie( sipendi mambo ya rushwa ila sasa ndo nchi yetu hii Kila mtu anaelewa mkono mtupu haulambwi)

Dogo nikamshirikisha, akaniambia Kuna hela wamepewa anaweza kua na hio M lakini akawa anasema bro huo ni utapeli tutaibiwa tu acha kama ni riziki ntapata tu, nikamsihi sana atoe Hio hela maana aliyeni connect nae mbona ni mtu wangu wa nguvu sidhani kama anaweza kunifanyia ujinga, kishingo upande dogo akamtumia Hio hela jamaa....tena jamaa akatuaminisha mpaka akamwambia dogo achague kituo Cha kazi kabisa😃😃Post zinatoka hola, dogo hajapata, aisee huyu dogo ananiheshimu ila alikuja kua mbogo mpaka akanivunjia heshima, akawa ananituhumu tumempiga milioni yake😃,kuanza kufatilia jamaa nae ananiambia mbona sielewi nilishachombeza jina la huyu apate kazi sijui Nini kimetokea, nikasema hapa tushaingizwa town, nikalalamika tu kwa jamaa aliyeniunganisha na huyu mtu lakini nae akawa ananiambia mbona huyo hayupo ivo, dogo sasa, ikawa usumbufu mpaka home akawa ananisema nimempiga hela nikaona Shari za Nini ikapita muda nikamtumia Hio milioni yake.....

Nimekaa kama wiki 3 mbele, jamaa aliyepewa milioni akanipigia akaniambia anaenda Dodoma kikazi akifika huko atafatilia kwanini dogo hazapata post, akaniambia bro nipe tu akaunti yako nikupe hizo hela umpe mdogo wako asione kama tumemdhulumu wakati na yeye anatafuta bado hajajipata.... Kumbuka hapo mi nilishapotezea hii ishu na dogo nilishamlipa, nikatuma Hio acc kishingo upande nikajua hapa hakuna lolote

Kweli baada ya muda naona muamula umesoma aisee nilishangaa sana(kumbuka sikuwahi kumsumbua arudishe hiyo pesa).... Nimekaa kama siku 2 jamaa ananipigia ananiambia muulize dogo kama alishawahi kuomba kazi serikalini, nikampigia dogo akaniambia baada ya kumaliza tu internship aliomba kazi serikalini..... Nikamrudia jamaa akaniambia huyo mdogo wako ni mjinga sana ametupotezea muda bure....Kumbe huyu mbwiga(dogo) alishawahi kuomba kazi serikalini akapata, akaona kituo kipo Kijijini huko hakwenda kuripoti, kwa maelezo ya jamaa akadai system ilikua bado inasoma kama dogo alishapata kazi, nikamuuliza kwa io hawafanyi confirmation baada ya watu kuripoti ili hao ambao hawajareport system iwaondoe akaniambia haelewi kwanini imekua ivo, kumbe walivyoingiza jina la dogo likasoma kama tayari alishapangiwa kituo

Nikamuelezea dogo akaniambia ni kweli alipangwa mbali sasa akaona bado ana kazi hakuenda, jamaa akanishauri mwambie mdogo wako afatilie huku hili jina lake litoke huku la sivyo hatakaa apate kazi huku, dogo ananiambia bro nisaidie sasa , nikamwambia ushakua mtu mzima fatilia mambo yako mwenyewe maana ushafanya familia wajue mi ni tapeli

Jamaa nikaja mtumia laki 2 kiuungwana nikamwambia bro najua ulitumia hata na vocha, nimekumbuka hilo tukio maana dogo alikua ananiomba namba ya huyo jamaa ( ambayo kimsingi Sina nilishapoteza) na rafiki yangu aliyenipa ile connection na jamaa tumemzika mwaka huu mwanzoni(RIP).... Dogo namuelesha kua Sina namba zake naona ishakua lawama anahisi kama bado nimemind nambania
Sasa hapo mtu muaminifu ni nani, huyo aliyeomba rushwa kuwaunganishia kazi?
 
Ndo jamaa aliniambia mwambie mdogo wako afatilie system itoe jina lake ila akaniambia hapo lazima atapigwa hela, na jamaa ni kama alikua hataki tena kufanya ishu za dogo maana aliniambia wote walionipa hela wamepangiwa vituo walivyoniomba kasoro huyu mdogo wako mjinga😃😃😃
Em lete connection hiyo kuna mshkaji wangu anasota nimfanyie hata mpango kwa jamaa
 
Samaki anaishi katuka maji mpaka hajui kwamba kuna maji.

Mtu anayeomba rushwa anaonekana muaminifu.
Only If!
Kama atakamilisha huo mchakato wa kutoa hio huduma baada ya kupokea rushwa, sasa imefikia mpaka unatoa rushwa halafu na hio huduma au favour pia hauipati, na unakuwa hauna opa kwenda,
Kwa sasa malalamiko mengi ukifatilia ni mtu amekula hela ya watu na hao watu hawakupata walichotaka.
A double whammy!
 
Hata akikamilisha huo mchakato bado si muaminifu. Muaminifu hachukui rushwa.

Ukishachukua rushwa, wewe si muaminifu.
 
Sasa hapo mtu muaminifu ni nani, huyo aliyeomba rushwa kuwaunganishia kazi?
Kiranga nimeona tu notification yako umeni quote akili ikanituma tu 'this ain't good' najua ligi zako tunaweza bishana mwezi

Ume experience another 'ride' huko huku kwetu hata huyu anayerudisha rushwa ambayo hajaifanyia kazi tunamuona muungwana

Kiufupi bila rushwa huku kwetu huwezi ku survive ndo mfumo wa maisha na tunaishi nao
 
Back
Top Bottom