Gowima
Member
- Jul 13, 2020
- 31
- 63
Mim nimekuja kugundua kumbe mambo mazuri yamejificha VETA hukooo! Madegree haya ya UDSM, SAUT, MZUMBE kilio kitupuuuu. But it too late to catch the morning bus.MUHIMU: MAADA INALENGA KUTEGEMEA KOZI ILI KUAJIRIWA (SIO KUJIAJIRI)
Kozi hizi ni
-ualimu (education)
-Procurement na Logistics
-Marketing
-Petroleum Chemistry
-Business Administration
- Marketing
Vyuo vinapodahili wanafunzi wawe wanaangalia hali ya idadi za ajira na wahitimu wa hizi fani, Kozi tajwa hapo juu ni nadra sana kutangazwa ajira na hapo hapo kuna wahitimu wengi ambao bado wanasubiri ajira zinazotoka chache kwa spidi ya kobe.
Kwa mfano, Kozi ya procurement kila mwaka wahitimu wanaweza kufikia elfu 5 ila ni ajira 10 tu mwaka mzima hutolwa na serikali. Kutoka mwaka 2015 hadi sasa panaweza kuwa na wahitimu wa fani hii elfu 15 ambao bado hawajapata ajira hizi chache zinaotoka taratibu.
Ningependa serikali iwe na mkakati mzuri wa kuvielekeza chuo kwamba idadi Fulani ya wahitimu ikifikia basi kozi inabidi zisimame kwa kipindi Fulani hivi.
Hakika ukisoma VETA Ni wazi utakuwa na ARI na position nzuri ya kujiajiri.