Mrisho Ngassa: Nimeshindwa kuperformance!

Mrisho Ngassa: Nimeshindwa kuperformance!

acha akatwe tu yeye c anaipenda yanga anaacha kufanya mpira kazi anajifanya yanga damu TEGETE tu ndo yanga damu
 
Hiki ni kingereza cha soccer . Soccer ina lugha yake na huwa hatu-edit ni kawaida kusikia tumefungwa kwa kushindwa kudeffence
 
Ndiyo maana alifurushwa kwenye majaribio West Ham United, pia aliogopa kwenda Sudan maana hakipandi, angeishije huko maana hata mademu anaopenda angetokeaje.
Hahahaaaaaaaa.... Kuperfomance....Yanga bhana ndio maana Ngasa haondoki pale kuna wenzake wengi wanaoelewana....
 
Tevez,Sanchez,Paulista na Ramires ni baadhi kati ya wachezaji wengi wanaongea kiingereza kibovu ila hakuna anaejali muhimu ujumbe umefika hata Ngasa kiingereza sio lugha ya kwanza sioni tatizo akifanya makosa.
Wakongo na wazungu wakikosea kiswahili tunaona kawaida tu duh sijui utumwa wa akili utatuacha lini,hongera kwake kwa kujaribu ipo siku ataimuda hiyo lugha hata kwa 50%.

naongezea hata Van Gaal kingereza kwake chenga kunawakati hadi anawauliza watu wa press hiki kwa kingereza mnasemaje
 
Ngasa kadai ameshindwa 'kuperformance' sababu sababu alikua anakatwa hela zote.
Sasa najiuliza kulikua na ulazima gani wa kutumia kiingereza?!
Afu mademu,iv kweli Ngasa angekua ka mimi tu mngemshobokea?!

Mi nadhani alikosea kama mtu mwingine anavyoweza kukosea. Hata wewe umekosea kuandika 'sababu sababu' hapo juu baada ya 'kuperformance' ulimaanisha nini?
Kingereza ni lugha kama ilivyo lugha nyingine. Kutoijua vizuri hakupunguzi wala kuongeza kitu. Lakini pia tunajifunza kutokana na makosa. Kama akikosolewa anajifunza ila si kukejeli kama vile ni kosa kubwa kihivyo. Hata wazungu nao wanakosea kiswahili mbona hatuwalaumu kwa kukosea ila tunawarekebisha!
 
Mkuu umesababisha nielekee kwa Mangi nikachukue "8.6 made from Holland" zangu 2 na embassy za jero ili niweze kulala vyema.
CC KakaJambazi

Njoo soma muumini mwenzangu wa kitu murua anavyomwaga matirio ya kunyakulia PhD.
 
Last edited by a moderator:
perfomance ni noun jamani,perfom ni verb,sasa yeye kashindwa kuperfomance,hajakosea jamani,hahahahaha

Alitakiwa aseme nimeshindwa "performance" au nimeshindwa " ku-perform" ku haiungiki na performance
 
Sikutegemea kama watu wazima wanaweza kutetea ujinga.Eti mbona mcheza flan na flan hawajui lugha ya Kiingereza.Je unajua uchumi wa nchi wanazotoka hao wachezaji?Je unafanana na tz?.Tatizo la wachezaji hawa ni shule ndogo sana...sijui hata kama darasa la 7 wanakuwa wamemaliza.Lakin hata kama kulikuwa na sababu flan flan bado kwa nafasi wa walizonazo wanaweza kwenda english course na kumudu lugha hii.kisha kuwa na uwanja mpana wa kazi yake...huwezi kuacha fursa kubwa kisa lugha haipandi.
 
perfomance ni noun jamani,perfom ni verb,sasa yeye kashindwa kuperfomance,hajakosea jamani,hahahahaha

Dada una kingereza kigumu!
Performance ni noun,huh?
Huenda ikawa nimepotea njia..
 
Uvivu kingereza ukiamua kukivalia njuga ni chepesi sana,diamond platinum si huyo now anakigonga kwa kwenda mbele na shule hajasoma,english sio elimu ni lugha tu kama kihaya
 
Tevez,Sanchez,Paulista na Ramires ni baadhi kati ya wachezaji wengi wanaongea kiingereza kibovu ila hakuna anaejali muhimu ujumbe umefika hata Ngasa kiingereza sio lugha ya kwanza sioni tatizo akifanya makosa.
Wakongo na wazungu wakikosea kiswahili tunaona kawaida tu duh sijui utumwa wa akili utatuacha lini,hongera kwake kwa kujaribu ipo siku ataimuda hiyo lugha hata kwa 50%.
hao uliowataja wanalazimika kutumia kiingereza kwa sababu wanazungumza na watu wa mataifa mengine ambayo hiyo ni lugha wanayoifahamu, ngassa anaongea na waswahili wenzake, lugha ngeni ya nini?! Utumwa tu unamsumbua!
 
Ngasa kadai ameshindwa 'kuperformance' sababu sababu alikua anakatwa hela zote.
Sasa najiuliza kulikua na ulazima gani wa kutumia kiingereza?!
Afu mademu,iv kweli Ngasa angekua ka mimi tu mngemshobokea?!

Kushindwa kwakwe "kuperformance" kunaweza kuchangiwa na ile movie aliyocheza na mdogo wake Flora Mbasha.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom