Mrisho Ngassa apandishwa kizimbani

Mrisho Ngassa apandishwa kizimbani

attachment.php

mshambuliaji nyota wa yanga na timu ya taifa, taifa stars, mrisho khalfan ngassa.

mshambuliaji nyota wa yanga na timu ya taifa, taifa stars, mrisho khalfan ngassa, amefunguliwa kesi ya madai ya talaka namba 30/2014, katika mahakama ya wilaya ya temeke jijini dar es salaam na mkewe latifa abdul fundi.

Ngassa amefunguliwa kesi hiyo akidaiwa kumtelekeza na kumnyima matunzo ya ndoa mke wake tangu juni mwaka 2011, migogoro ilipoanzia.

Kesi hiyo iliyoanza kuunguruma baraza kuu la waislamu nchini (bakwata), kitengo cha mashauri ya ndoa, mambo yalikwenda ndivyo sivyo kufuatia ngassa kutotoa ushirikiano katika baraza hilo.

Baada ya baraza hilo kushindwa kesi hiyo, liliihamishia mahakamani hapo ambapo juzi (jumatatu), mchezaji huyo na mkewe walitakiwa kupanda kizimbani mbele ya hakimu waliyepangiwa, timothy lyon, lakini ngassa alishindwa kutokea kutokana na majukumu aliyokuwanayo kwenye timu ya taifa iliyokuwa nchini burundi.

Kufuatia udhuru huo, hakimu lyon aliiahirisha kesi hiyo mpaka septemba 30, mwaka huu ambapo ngassa na latifa wanatakiwa kupanda kizimbani katika shauri hilo.

Katika kesi hiyo, latifa anamdai, ngassa talaka pamoja na mgawanyo wa mali walizochuma wakiwa katika ndoa yao ikiwemo nyumba mbili, moja iliyopo yombo na nyingine tegeta basihaya jijini dar es salaam.

Kiwanja kimoja kilichopo tegeta basihaya jijini, gari aina ya toyota cresta, vitanda viwili, kabati dogo la vipodozi, seti ya masofa, meza, pasi ya umeme, majiko mawili ya kupikia, televisheni, redio kaseti, brenda na draya.

Pamoja na mali hizo, latifa anamdai ngassa ampe pesa taslimu shilingi laki mbili na nusu (250,000/) kila mwezi, tangu juni 2011, mpaka siku ya hukumu ambazo ni kwa ajili ya matunzo tangu alipositisha kumhudumia.

Jalada la kesi hiyo liliambatanishwa na cheti cha ndoa kinachoonyesha wawili hao walifunga ndoa mei mosi, mwaka 2009, mashahidi wakiwa imani madega na saidy rashid.


chanzo: globalpublishers

hiiii itakuwa fundisho kwa wale wachezaji wanaohisi kuzaa ni kitu kidogo tu

kuoa utaoa lakini ukizaa kutunza jukumu lako wangu ngassa

mbaya zaiidi alipomwocha src ni kademu kalichomgombanisha mwimbaji flora ngasa noo flora mbasha na mumewe ..aka mdogo wake flora

hako kalibadilisha maisha ya ngassa kabisa na hata flora alikuwa akijua mdogo wake huyu wa hiari akitembea na mrisho halfan ngassa wakati ni mume wa mtu

nahisi ukimyaa hu huu ndio umemzawadia yale yanayotokea kwenye ndoa yake ..ngassa ni shahidi wa hili na mkewe ....

Tubadilike turekebishe maisha yetu hata kama una ka stigma pembeni

lazima nyumbani uwaheshimu ati
 
Du noma sana demu wa kimakonde ni shida amepiga vizuri hesabu zake? Laki 2 na nusu kwa miaka mi3 ni 9m tu labda apiganie hizo nyumba achukue hiyo ya yombo ye amwachie ya tegeta,maana nakumbuka alisema ana nyumba nne mbili dsm na nyingine 2 mwanza na za dsm zina thamani ya milioni 100 mia @.
 
Kwa picha zile...nilisitisha ushabiki kwa yanga....na nilisusia kuishangilia stars kila alipokuwa anapangwa.
 
Wanawake wengine jamani, kwenda kudai hadi kabati la vipodozi ndiyo nini?
Wakati mwingine na sisi tuwe wajasiliamali vinginevyo hawa wanaume watatunyanyasa sana.

umenena mkuu,mwanamke mwenye sikio kamemuingia!!
 
Du noma sana demu wa kimakonde ni shida amepiga vizuri hesabu zake? .

Ngassa kashakua Kama mamwinyi.babaake alimwoza kule Mwanza,Madega akamwoza,akaongeza wa 3.achilia vicheche...anasema ana umri gani tena?
 
Haya boss ngasa..nkeo anadai mpaka pasi
 
matunzo? angedai huduma muhimu ya kimwili, tangu 2011 hajafanya tendo la ndoa! pole na ukipata taraka katafute mume mungine 'man U'
 
Ndoa na masupastaa ni majanga,mnao oa au kuolewa mkae mkijua hivyo.labda nawe uwe kicheche
 
Hakuna uswahili hapo wacha adai haki yake, tena kamhurumia, mswahili ni huyo Ngasa mwenyewe anayeoa oa bila mpangilio
 
Ngassa kashakua Kama mamwinyi.babaake alimwoza kule Mwanza,Madega akamwoza,akaongeza wa 3.achilia vicheche...anasema ana umri gani tena?

toka nimejua mwaka 2006 ana sema ana miaka 17 mpaka leo umri wake umegoma kabisa kwenda mbele umeganda palepale ulipo
 
Wangekuwa na mahakama yao ya KADHI inayoendeshwa na wao wenyewe si wangepelekana huko..??
 
Back
Top Bottom