Mrisho Gambo: Suala la wamachinga si la mchezo, ni kuhusu maisha ya watu tena wanyonge kabisa. Tusisukumwe na Wafanyabiasha Wakubwa

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Suala la Machinga si jambo jepesi hata kidogo. Hakuna mtu anayependa kuwa mmachinga bali maisha ndio yamewafikisha hapo. Hakuna anayependa kupanga vitu vyake barabarani apigwe na jua au anyeshewe na mvua au agongwe na gari.

Changamoto kubwa ni ukosefu wa ajira na Kazi ya Machinga imekuwa ni sehemu ya kupumulia.

Hili si suala la mchezo ni kuhusu maisha ya watu tena watu wanyonge kabisa. Hapa tusisukumwe na Wafanyabiasha Wakubwa wakati tunashughulikia suala la MACHINGA.

Ni jambo linalohitaji utulivu na kuangalia mustakabali wa maisha ya watu.

Mrisho Gambo
Mbunge-Arusha Mjini

images (6).jpeg
 
Ni jambo linalohitaji utulivu na kuangalia mustakabali wa maisha ya watu."
Huyu ni
giphy.gif
 
Suala la Machinga si jambo jepesi hata kidogo. Hakuna mtu anayependa kuwa mmachinga bali maisha ndio yamewafikisha hapo. Hakuna anayependa kupanga vitu vyake barabarani apigwe na jua au anyeshewe na mvua au agongwe na gari.

Changamoto kubwa ni ukosefu wa ajira na Kazi ya Machinga imekuwa ni sehemu ya kupumulia.

Hili si suala la mchezo ni kuhusu maisha ya watu tena watu wanyonge kabisa. Hapa tusisukumwe na Wafanyabiasha Wakubwa wakati tunashughulikia suala la MACHINGA.

Ni jambo linalohitaji utulivu na kuangalia mustakabali wa maisha ya watu.

Mrisho Gambo
Mbunge-Arusha Mjini

View attachment 1932006
Nimependa sana alivyojivua uwajibikaji..kwamba wafanyabiashara wakubwa ndio wachawi wa mamachinga....kwahiyo lawama ziende kwa wafanyabiashara wakubwa sio kwao wanasiasa na serikali.

Kweli chama kizee kimekosa mvuto..inamaana hawakua na longtime plan kuhusiana na ongezeko la watu..na namna ya kukabiliana na ukosefu wa ajira.

Wasubiri siku wamachinga wakianza kupanga kwenye vibaraza vya nyumba zao ndio sijui watamlaumu nani.

#MaendeleoHayanaChama
 
Wabunge wote waliopo bungeni hawatarudi bungeni 2025 wacha waendelee tu kucheza.

Waache kujificha kwenye kichaka Cha wamachinga

Ila swala la machinga ni la kisheria fremu zipo wazi waingie hata watatu watatu wafanye biashara walipe Kodi.
 
Huyu dogo...ana Wivu na wafanyabiadhara wakubwa. Wanasiasa wa namna hii hawawezi kuwa solution ya matatizo ya jamii yetu.badala ya kuleta mbinu ya kuwasaidia machinga wawe na permanent places za biashara yeye analaume group lingine. Hopeless kabsaa huyu...
Machinga tatizo ni serikali hasa kuwa na mipango madhubuti ya wapi wafanyie biashara zao.
Mfano:serikali inashindwaje kuchukua maeneo strategic kibiashara na kuwadia wananch wenye maeneo hayo na kubadili use of land?
 
Inasikitisha kuwa na viongozi wenye mawazo dhaifu kila upande. Kunapotokea tatizo badala ya kufikiria na kufanya utafiti wa kina namna ya kulitatua la kwanza wanalowaza ni kumtafuta mchawi. Ni ujinga uliopitiliza na inaonyesha wazi huu udhaifu umo ndani ya siasa zetu na mfumo wake. Mfano kila uchumi unapoyumba la kwanza utasikia "mabeberu ndiyo wamesababisha". Wakati huo huo hao hao mabeberu ndiyo wanaojazia bajeti ya nchi kila mwaka hadi miaka 60 ya Uhuru. ILI TUTOKE HAPA KAMA TAIFA HATUNA BUDI KUUKATAA, KUUPINGA NA KUUANGAMIZA KABISA MWENDO HUU WA FIKRA DHAIFU!
 
Suala la Machinga si jambo jepesi hata kidogo. Hakuna mtu anayependa kuwa mmachinga bali maisha ndio yamewafikisha hapo. Hakuna anayependa kupanga vitu vyake barabarani apigwe na jua au anyeshewe na mvua au agongwe na gari.

Changamoto kubwa ni ukosefu wa ajira na Kazi ya Machinga imekuwa ni sehemu ya kupumulia.

Hili si suala la mchezo ni kuhusu maisha ya watu tena watu wanyonge kabisa. Hapa tusisukumwe na Wafanyabiasha Wakubwa wakati tunashughulikia suala la MACHINGA.

Ni jambo linalohitaji utulivu na kuangalia mustakabali wa maisha ya watu.

Mrisho Gambo
Mbunge-Arusha Mjini

View attachment 1932006
Mrisho Gambo usitafute sifa za kijinga.
Miji imechafuka utafikiri erikali imeenda likizo.
Kama una uchungu na machinga wakaribishe upenuni mwako na uone.
 
Nimeona jamaa jana alivua nguo akabski uchi watu badala ya kuumizwa na zile ngumi pale Kariakoo wakawa wanaushangaa Mtwangiso wenye uko unabembea dah maskini Magu atakumbukwa.

Alizitaka serikali za mitaa kutenga maeneo kwa ajili ya Wafanyabiashara wao lakini RCs,RASs,DCs, DEDs, DAS, MDs, Mameya, Madiwani,DOs,WEO,WENYEGITI,MEOs/VEOs walikosa plan ya kuwapanga watu hawa ndipo akaamua kuwa wafanye biashara popote tu wasiguswe!!

Sasa naona vita ya wenyewe kwa wenyewe inanukia..Samia watch it mama!!!
 
Huyu mjinga sana hakuna nchi duniani ikaendelea kwa wamachinga barabarani ataje nchi moja duniani. Nchi inaendeshwa na wafanya biashara wenye kulipa kodi sio fujo barabarani hata risiti hawatoi kuharibu mazingira na kuuwa biashara. Soko la kariakoo ni hazina na lazima liwe la kimataifa hata wafanya biashara wa nchi jirani wakija wajisikie hali ya usalama na kufanya biashara kwa kufuata sheria na kulipa stahiki zote. wamachinga ni lazima waondoke barabarani hilo halina mjadala.
 
Suala la Machinga si jambo jepesi hata kidogo. Hakuna mtu anayependa kuwa mmachinga bali maisha ndio yamewafikisha hapo. Hakuna anayependa kupanga vitu vyake barabarani apigwe na jua au anyeshewe na mvua au agongwe na gari.

Changamoto kubwa ni ukosefu wa ajira na Kazi ya Machinga imekuwa ni sehemu ya kupumulia.

Hili si suala la mchezo ni kuhusu maisha ya watu tena watu wanyonge kabisa. Hapa tusisukumwe na Wafanyabiasha Wakubwa wakati tunashughulikia suala la MACHINGA.

Ni jambo linalohitaji utulivu na kuangalia mustakabali wa maisha ya watu.

Mrisho Gambo
Mbunge-Arusha Mjini

View attachment 1932006

Wamachinga watoke kwenye sehemu za kutembea. Huwezi kuendesha nchi bila mpangilio! wengine wanatafuta umashuhuri tu
 
Suala la Machinga si jambo jepesi hata kidogo. Hakuna mtu anayependa kuwa mmachinga bali maisha ndio yamewafikisha hapo. Hakuna anayependa kupanga vitu vyake barabarani apigwe na jua au anyeshewe na mvua au agongwe na gari.

Changamoto kubwa ni ukosefu wa ajira na Kazi ya Machinga imekuwa ni sehemu ya kupumulia.

Hili si suala la mchezo ni kuhusu maisha ya watu tena watu wanyonge kabisa. Hapa tusisukumwe na Wafanyabiasha Wakubwa wakati tunashughulikia suala la MACHINGA.

Ni jambo linalohitaji utulivu na kuangalia mustakabali wa maisha ya watu.

Mrisho Gambo
Mbunge-Arusha Mjini

View attachment 1932006
Msameheni bure ndio upeo wake wa kufiri umeishia hapo. Nilitegemea aje na njia mbadala ya namna ya kuwa accommodate hawa Machinga lkn kwa kutetea uwepo wao katika hali hii mimi binafsi nimemsamehe.
 
Back
Top Bottom