Lema adai Gambo anaficha ukweli kuhusu Tsh. Mil 400 za Bodaboda, Kingai aingilia

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Siku moja baada Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo kutoa madai ya kuwepo njama za kuuawa baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa Serikali aliosema anawajua, Godbless Lema, mbunge wa zamani wa jimbo hilo amemshukia akisema analenga kuhamisha goli huku Jeshi la Polisi likianza kufuatilia madai hayo.

Gambo alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara alioufanya juzi katika Soko la Kilombero jijini Arusha ili kusikiliza kero za wananchi.

Alisema yamefanyika majaribio mawili ya kuvamia nyumbani kwake huko eneo la Murieti ili kumuua lakini yameshindikana. “Mimi najiamini, wanakwambia ukirusha mawe hakikisha hukai kwenye nyumba ya vioo, hawa jamaa siku wakinikamata hakuna rangi nitaacha ona, maana wamejaribu sababu nyingine zote wameshindwa,” alisema.

Alisema nyumbani kwake kumeshavamiwa mara mbili na waliomvamia anawafahamu kwani wengine ni watu wa chama tawala na Serikali.

“Mara ya kwanza walinikosa, na mimi si nimekulia humohumo. Mimi sio fala eti, wao wakikaa kule wakipanga mipango tumuibukie leo, wakaja wakashangaa nimechoropoka. Wakaenda mara ya pili wakafanya kituko cha ajabu kweli, wameingia mle ndani wakapekuapekua, ashakum si matusi walikuwa wamekwenda na kondomu wakaweka lotion ili mke wangu akienda kule ajue nakula mzigo akiwa hayupo,” alisema Gambo.

Wakati hayo yakiendelea, Mbunge wa zamani wa Arusha, Godbless Lema alisema tuhuma za Gambo ni kuhamisha goli la mjadala wa Sh400 milioni za Chama cha Waendesha Bodaboda Jiji la Arusha (Uboja). Lema anayeishi uhamishoni nchini Canada, alisisitiza kinachofanywa na Gambo ni kuzima mjadala huo ndio maana anaibua tuhuma kwa viongozi.

Mwezi uliopita Aboja ilibaini zaidi ya Sh400 milioni zimetolewa kwenye akaunti yao na baadhi ya fedha hizo kutumika kisiasa. Fedha hizo zinadaiwa kutolewa kuanzia mwaka 2018 hadi 2021 katika mazingira ya kutatanisha na Gambo alishauri waliokuwa viongozi wa umoja huo watafutwe ili wazirejeshe fedha hizo.

“Nina wajua viongozi wa Serikali wa Arusha kuanzia Mongela (John- Mkuu wa mkoa) na Said Mtanda (Mkuu wa wilaya ), wana UCCM lakini si kupanga mauaji dhidi ya Gambo, mbunge huyu anataka kuzima mjadala wake,” alisema.

Wakati Lema akisema hayo, jana Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai alisema tuhuma hizo ni za jinai hivyo zitachunguzwa kwa mujibu wa sheria.

“Kwa kuwa jambo jili limetokea Arusha, naomba uzungumze na kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, kama jana alisema alikuwa hana taarifa inawezekana leo anazo,” alisema Kingai. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo jana hakupatikana lakini alipozungumza na gazeti hili juzi alisema hana taarifa za Gambo kutishiwa kuuawa.

Hata hivyo, gazeti hili lina taarifa kuwa uongozi wa Mkoa wa Arusha umeanza uchunguzi wa tuhuma hizo ikiwamo kumtafuta Gambo mwenyewe ili kupata maelezo ya kina na kuwataja watuhumiwa anaodai anawafahamu.

Kwa upande wao, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha, Dk Wilfred Ole Soileli na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda walisema watalizungumzia suala hilo leo. Kutokana na kuwa katika majukumu mengine yasiyomruhusu kuzungumza kwa kina, Soileli alisema “naomba tuonane kesho (leo) saa tano.”

Wakati CCM na Serikali wakitarajia kuzungumza leo, Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alisema wameanza kuzifanyia kazi tuhuma hizo kuhakikisha mbunge anakuwa salama.

“Mimi sina hizo taarifa za Mheshimiwa Gambo kutaka kuuawa ila tunafatilia,” alisema Nenelwa.

Gambo amekuwa mbunge Arusha Mjini baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Kabla ya ubunge, alikuwa mkuu wa mkoa huo akipanda kutoka kuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Tuhuma hizo, Gambo amezitoa kipindi ambacho ana msuguano na baadhi ya viongozi wa CCM na Serikali tangu alipoeleza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mei 24 kuwa baadhi yao wanakula fedha za jiji.

Kutokana na tuhuma hizo, baadhi ya viongozi wa jiji walifunguliwa mashtaka na sasa wanaendelea na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha huku yeye akisisitiza kuwa ataendelea kukemea ufujaji wa fedha za umma.

MWANANCHI
 
Tuhuma za Lissu enzi zile zilipuuzwa na bunge la Ndugai mpaka aliposhambuliwa kwa risasi.....ila Mungu ni mwema hakupuuza kumlinda.
 
Uhai wa mwaccm una thamani kuliko mpinzani japo wote ni Watanzania swali Gambo kaenda kulalamika polis? Maana Sirro alitwambia kuwa Lissu hakutoa taarifa polis?
 
Gambo anyooshe maelezo tu, hao jamaa walikuja wakamnaniliu yeye akiwa kalala usingizi wa pono kastuka asubuhi kukuta condom zilizotumika zikiwa zimejaa wazungu kibao.
 
Uhai wa mwaccm una thamani kuliko mpinzani japo wote ni Watanzania swali Gambo kaenda kulalamika polis? Maana Sirro alitwambia kuwa Lissu hakutoa taarifa polis?

ili jambo mpala leo nilizarau serikali yangu pande zote
 
Siku moja baada Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo kutoa madai ya kuwepo njama za kuuawa baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa Serikali aliosema anawajua, Godbless Lema, mbunge wa zamani wa jimbo hilo amemshukia akisema analenga kuhamisha goli huku Jeshi la Polisi likianza kufuatilia madai hayo.

Gambo alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara alioufanya juzi katika Soko la Kilombero jijini Arusha ili kusikiliza kero za wananchi.

Alisema yamefanyika majaribio mawili ya kuvamia nyumbani kwake huko eneo la Murieti ili kumuua lakini yameshindikana. “Mimi najiamini, wanakwambia ukirusha mawe hakikisha hukai kwenye nyumba ya vioo, hawa jamaa siku wakinikamata hakuna rangi nitaacha ona, maana wamejaribu sababu nyingine zote wameshindwa,” alisema.

Alisema nyumbani kwake kumeshavamiwa mara mbili na waliomvamia anawafahamu kwani wengine ni watu wa chama tawala na Serikali.

“Mara ya kwanza walinikosa, na mimi si nimekulia humohumo. Mimi sio fala eti, wao wakikaa kule wakipanga mipango tumuibukie leo, wakaja wakashangaa nimechoropoka. Wakaenda mara ya pili wakafanya kituko cha ajabu kweli, wameingia mle ndani wakapekuapekua, ashakum si matusi walikuwa wamekwenda na kondomu wakaweka lotion ili mke wangu akienda kule ajue nakula mzigo akiwa hayupo,” alisema Gambo.

Wakati hayo yakiendelea, Mbunge wa zamani wa Arusha, Godbless Lema alisema tuhuma za Gambo ni kuhamisha goli la mjadala wa Sh400 milioni za Chama cha Waendesha Bodaboda Jiji la Arusha (Uboja). Lema anayeishi uhamishoni nchini Canada, alisisitiza kinachofanywa na Gambo ni kuzima mjadala huo ndio maana anaibua tuhuma kwa viongozi.

Mwezi uliopita Aboja ilibaini zaidi ya Sh400 milioni zimetolewa kwenye akaunti yao na baadhi ya fedha hizo kutumika kisiasa. Fedha hizo zinadaiwa kutolewa kuanzia mwaka 2018 hadi 2021 katika mazingira ya kutatanisha na Gambo alishauri waliokuwa viongozi wa umoja huo watafutwe ili wazirejeshe fedha hizo.

“Nina wajua viongozi wa Serikali wa Arusha kuanzia Mongela (John- Mkuu wa mkoa) na Said Mtanda (Mkuu wa wilaya ), wana UCCM lakini si kupanga mauaji dhidi ya Gambo, mbunge huyu anataka kuzima mjadala wake,” alisema.

Wakati Lema akisema hayo, jana Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai alisema tuhuma hizo ni za jinai hivyo zitachunguzwa kwa mujibu wa sheria.

“Kwa kuwa jambo jili limetokea Arusha, naomba uzungumze na kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, kama jana alisema alikuwa hana taarifa inawezekana leo anazo,” alisema Kingai. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo jana hakupatikana lakini alipozungumza na gazeti hili juzi alisema hana taarifa za Gambo kutishiwa kuuawa.

Hata hivyo, gazeti hili lina taarifa kuwa uongozi wa Mkoa wa Arusha umeanza uchunguzi wa tuhuma hizo ikiwamo kumtafuta Gambo mwenyewe ili kupata maelezo ya kina na kuwataja watuhumiwa anaodai anawafahamu.

Kwa upande wao, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha, Dk Wilfred Ole Soileli na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda walisema watalizungumzia suala hilo leo. Kutokana na kuwa katika majukumu mengine yasiyomruhusu kuzungumza kwa kina, Soileli alisema “naomba tuonane kesho (leo) saa tano.”

Wakati CCM na Serikali wakitarajia kuzungumza leo, Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alisema wameanza kuzifanyia kazi tuhuma hizo kuhakikisha mbunge anakuwa salama.

“Mimi sina hizo taarifa za Mheshimiwa Gambo kutaka kuuawa ila tunafatilia,” alisema Nenelwa.

Gambo amekuwa mbunge Arusha Mjini baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Kabla ya ubunge, alikuwa mkuu wa mkoa huo akipanda kutoka kuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Tuhuma hizo, Gambo amezitoa kipindi ambacho ana msuguano na baadhi ya viongozi wa CCM na Serikali tangu alipoeleza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mei 24 kuwa baadhi yao wanakula fedha za jiji.

Kutokana na tuhuma hizo, baadhi ya viongozi wa jiji walifunguliwa mashtaka na sasa wanaendelea na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha huku yeye akisisitiza kuwa ataendelea kukemea ufujaji wa fedha za umma.

MWANANCHI
wakati fulani kuna mtu nje ya ccm alisema wakiwamaliza wa nje ya chama chao watamalizana wao kwa wao.
 
makubaliano ya boda boda watatumia vilainishi vinavotumika kwenye injini.picha wametuma
IMG_0311.jpg
 
Kama mihimili inalalamika inaishi kwa mashaka sisi akina kajamba nani itakuwaje
 
anaogopa kijambio chake kuzurika.

nasikia watu wanafanyiwa hivo si rahisi kushtaki kutokana na aibu na mwisho wa siku kujiua wenyewe kwa mawazo na aibu
 
Kupigwa proncher siyo jambo dogo
 
Siku moja baada Mbunge wa Arusha Mjini (CCM), Mrisho Gambo kutoa madai ya kuwepo njama za kuuawa baadhi ya makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na viongozi wa Serikali aliosema anawajua, Godbless Lema, mbunge wa zamani wa jimbo hilo amemshukia akisema analenga kuhamisha goli huku Jeshi la Polisi likianza kufuatilia madai hayo.

Gambo alitoa tuhuma hizo kwenye mkutano wa hadhara alioufanya juzi katika Soko la Kilombero jijini Arusha ili kusikiliza kero za wananchi.

Alisema yamefanyika majaribio mawili ya kuvamia nyumbani kwake huko eneo la Murieti ili kumuua lakini yameshindikana. “Mimi najiamini, wanakwambia ukirusha mawe hakikisha hukai kwenye nyumba ya vioo, hawa jamaa siku wakinikamata hakuna rangi nitaacha ona, maana wamejaribu sababu nyingine zote wameshindwa,” alisema.

Alisema nyumbani kwake kumeshavamiwa mara mbili na waliomvamia anawafahamu kwani wengine ni watu wa chama tawala na Serikali.

“Mara ya kwanza walinikosa, na mimi si nimekulia humohumo. Mimi sio fala eti, wao wakikaa kule wakipanga mipango tumuibukie leo, wakaja wakashangaa nimechoropoka. Wakaenda mara ya pili wakafanya kituko cha ajabu kweli, wameingia mle ndani wakapekuapekua, ashakum si matusi walikuwa wamekwenda na kondomu wakaweka lotion ili mke wangu akienda kule ajue nakula mzigo akiwa hayupo,” alisema Gambo.

Wakati hayo yakiendelea, Mbunge wa zamani wa Arusha, Godbless Lema alisema tuhuma za Gambo ni kuhamisha goli la mjadala wa Sh400 milioni za Chama cha Waendesha Bodaboda Jiji la Arusha (Uboja). Lema anayeishi uhamishoni nchini Canada, alisisitiza kinachofanywa na Gambo ni kuzima mjadala huo ndio maana anaibua tuhuma kwa viongozi.

Mwezi uliopita Aboja ilibaini zaidi ya Sh400 milioni zimetolewa kwenye akaunti yao na baadhi ya fedha hizo kutumika kisiasa. Fedha hizo zinadaiwa kutolewa kuanzia mwaka 2018 hadi 2021 katika mazingira ya kutatanisha na Gambo alishauri waliokuwa viongozi wa umoja huo watafutwe ili wazirejeshe fedha hizo.

“Nina wajua viongozi wa Serikali wa Arusha kuanzia Mongela (John- Mkuu wa mkoa) na Said Mtanda (Mkuu wa wilaya ), wana UCCM lakini si kupanga mauaji dhidi ya Gambo, mbunge huyu anataka kuzima mjadala wake,” alisema.

Wakati Lema akisema hayo, jana Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhan Kingai alisema tuhuma hizo ni za jinai hivyo zitachunguzwa kwa mujibu wa sheria.

“Kwa kuwa jambo jili limetokea Arusha, naomba uzungumze na kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha, kama jana alisema alikuwa hana taarifa inawezekana leo anazo,” alisema Kingai. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Justine Masejo jana hakupatikana lakini alipozungumza na gazeti hili juzi alisema hana taarifa za Gambo kutishiwa kuuawa.

Hata hivyo, gazeti hili lina taarifa kuwa uongozi wa Mkoa wa Arusha umeanza uchunguzi wa tuhuma hizo ikiwamo kumtafuta Gambo mwenyewe ili kupata maelezo ya kina na kuwataja watuhumiwa anaodai anawafahamu.

Kwa upande wao, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Arusha, Dk Wilfred Ole Soileli na Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Said Mtanda walisema watalizungumzia suala hilo leo. Kutokana na kuwa katika majukumu mengine yasiyomruhusu kuzungumza kwa kina, Soileli alisema “naomba tuonane kesho (leo) saa tano.”

Wakati CCM na Serikali wakitarajia kuzungumza leo, Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alisema wameanza kuzifanyia kazi tuhuma hizo kuhakikisha mbunge anakuwa salama.

“Mimi sina hizo taarifa za Mheshimiwa Gambo kutaka kuuawa ila tunafatilia,” alisema Nenelwa.

Gambo amekuwa mbunge Arusha Mjini baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Kabla ya ubunge, alikuwa mkuu wa mkoa huo akipanda kutoka kuwa mkuu wa Wilaya ya Arusha.

Tuhuma hizo, Gambo amezitoa kipindi ambacho ana msuguano na baadhi ya viongozi wa CCM na Serikali tangu alipoeleza mbele ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mei 24 kuwa baadhi yao wanakula fedha za jiji.

Kutokana na tuhuma hizo, baadhi ya viongozi wa jiji walifunguliwa mashtaka na sasa wanaendelea na kesi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha huku yeye akisisitiza kuwa ataendelea kukemea ufujaji wa fedha za umma.

MWANANCHI
Karma
 
Hiyo lotion na ndomu walitaka kufanzia kazi gani humo? Teh teh.....
 
Back
Top Bottom