Mrisho Gambo: Familia ya Lisu ilishafeli somo la unafiki

Frank Wanjiru

Platinum Member
Joined
Apr 12, 2012
Posts
25,794
Reaction score
47,250
Mwanasiasa Mrisho Gambo ameisifia familia ya marehemu Wakili Alute Simon Mughwai Lissu kwa kuwa na misimamo thabiti katika kusimamia haki na ukweli, akisema misimamo hiyo si ya kuigiza bali ni matokeo ya misingi imara ya malezi iliyoanzia ngazi ya familia.

Akitoa salamu za rambirambi wakati wa kumuaga marehemu Alute, Gambo amesema tofauti za itikadi za kisiasa kati ya Alute na mdogo wake Tundu Lissu hazikuwazuia kusimamia kile wanachokiamini.

Gambo amesema familia hiyo imeonesha mfano wa watu wanaothamini ukweli kuliko unafiki, akieleza kuwa ni muhimu kwa Watanzania kujifunza kutoka katika misingi ya malezi ya familia hiyo.

Ameongeza kuwa taifa linahitaji kujenga vizazi vyenye misimamo na uadilifu, ambavyo hata baada ya kuondoka duniani vitaacha historia ya mchango wao katika jamii.

Aidha, Gambo amesisitiza umuhimu wa kusimamia haki bila upendeleo wala kuangalia itikadi za kisiasa, akionya kuwa kushindwa kufanya hivyo kutakuwa na madhara kwa taifa zima.

Amehitimisha kwa kumuombea marehemu Alute apumzike kwa amani na kuitaka jamii kuendelea kuthamini misingi ya haki, ukweli na uzalendo.
 
nadhani huyo wa gerezani kubebwa ufala wa kifikra na kukubali kua kibaraka wa mabwenyenye ya magharibi ametia aibu sana watu wa Singida aise 🐒
 
Tatizo la nchi za Kiafrika ukiwa mzalendo na mkweli maisha yako yapo hatarini. Ukifichua ufisadi wa mtu hupumui!! Ila ndugu yetu Lissu hajali na Mungu anamlinda. Kitendo cha kupona na zile risasi ni mpango wa Mungu, huenda ni kiongozi mtarajiwa wa taifa letu la Tz.
 
Mwanasiasa Mrisho Gambo ameisifia familia ya marehemu Wakili Alute Simon Mughwai Lissu kwa kuwa na misimamo thabiti katika kusimamia haki na ukweli, akisema misimamo hiyo si ya kuigiza bali ni matokeo ya misingi imara ya malezi iliyoanzia ngazi ya familia.

Akitoa salamu za rambirambi wakati wa kumuaga marehemu Alute, Gambo amesema tofauti za itikadi za kisiasa kati ya Alute na mdogo wake Tundu Lissu hazikuwazuia kusimamia kile wanachokiamini.

Gambo amesema familia hiyo imeonesha mfano wa watu wanaothamini ukweli kuliko unafiki, akieleza kuwa ni muhimu kwa Watanzania kujifunza kutoka katika misingi ya malezi ya familia hiyo.

Ameongeza kuwa taifa linahitaji kujenga vizazi vyenye misimamo na uadilifu, ambavyo hata baada ya kuondoka duniani vitaacha historia ya mchango wao katika jamii.

Aidha, Gambo amesisitiza umuhimu wa kusimamia haki bila upendeleo wala kuangalia itikadi za kisiasa, akionya kuwa kushindwa kufanya hivyo kutakuwa na madhara kwa taifa zima.

Amehitimisha kwa kumuombea marehemu Alute apumzike kwa amani na kuitaka jamii kuendelea kuthamini misingi ya haki, ukweli na uzalendo.

Hivi kwa nini MaCCM wengi wameukwepa huu msiba. Wanaogopa nini au ndiyo aibu inawasumbua....!!
 
Familia ya Lisu kwa kweli imebarikiwa. Maana ni wazi kuwa ni familia inayosimama kwenye ukweli, haki na upendo daima. Hii ni familia ya kuigwa. Ni familia iliyobarikiwa, siyo kama zile familia za laana za akina Mwashambwa na akina Tlaatlaah. Tunaomba Mungu wa haki azidi kuibariki familia hii, naye huyu alitetangulia mbele za haki, tunaomba akajaliwe makao mema, akawe mmojawapo wa watakatifu wake wenye kuozunguka meza yake kwani aliishi haki yake YEYE BWANA WA HAKI.
 
Back
Top Bottom