MAKOLE
JF-Expert Member
- Feb 5, 2012
- 618
- 280
Jana, siku ya kwanza ya mgomo wa walimu, bwana mrisho Gambo alifundisha Hisabati darasa la saba katika Shule ya Msingi Mazoezi-Manundu. Leo, siku ya pili ya mgomo wa walimu Mh. huyo ameendelea kushusha namba katika shule pacha za Mazoezi Manundu na Mazoezi Mbeza. Amepiga somo la namba lakini kwa bahati mbaya sana aliitwa ofisini akiwa amefundisha maumbo mawili tu katika shule ya Mazoezi-mbeza. Nimejaribu kumuomba Chalii anipe daftari lake nikague lakini amesema kuwa mwalimu- mkuu anafundisha tu lakini wao hawaandiki.
My take: jamaa anajitahidi ila ningemshauri sana aende kufundisha katika shule zilizoko chaka kwani hapa mjini wanafunzi hawana tatizo, wanazo tuition. lakini huko vijijini hakuna tuition hivyo wanafunzi wanaathirika zaidi.