Mrembo mjasiriamali bongo amshauri Rais Magufuli mambo makuu matatu

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
MREMBO mjasiriamali Bongo aitwaye Babra Kalugira ameibuka na kumshauri Rais Dk. John Pombe Magufuli 'JPM' mambo makubwa matatu.

Kalugira ni mjasiriamali lakini pia ni mfanyakazi kwenye taasisi binafsi nchini.
Msikilize mwenyewe.

"MHESHIMIWA rais, mawaziri, wabunge na Watanzania wenzangu, shikamoni. Mimi naitwa Barbra Kalugira, nina miaka 31. Kubwa lililonileta hapa ni kumshauri Rais na serikali yake. Nataka nitoe wazo ambalo ninaamini linaweza likasaidia kujenga uchumi wa Tanzania."

KUHUSU KOROSHO
"Naomba niongelee suala la Korosho. Korosho tumekuwa tukiiangalia kwa kuiuza tu, Korosho kama korosho. Lakini mimi ninaiangalia kwa jicho lingine. Kivipi? Korosho ukiangalia vizuri ina product (bidhaa) nyingi sana ambazo zinaweza kutoka.

"Kuna product inaitwa vegetable oil (mafuta ya mboga). Tukiiangalia kiafya, vegetable oil it is very good. Haina cholesterol.

"Korosho inatoa maziwa. Lakini pia Korosho ukiangalia vizuri, watu ambao wameshatumia ile peanut butter (siagi ya karanga), inatoa ile paste. Korosho inaweza ikatengenezewa cake. Mambo ya bakery (uokaji).

"At the same time, Korosho ukiitumia kama maziwa, ukiitumia kama vegetable oil, yale makapi yake yanatengenezwa chakula cha mifugo. Tukiachana na chakula, Korosho inaweza kutengeneza mafuta ya ngozi mazuri sana ambayo hayaathiri ngozi zetu sisi Waafrika.

"Lakini pia ukiifanya Korosho kama ya kutolea bidhaa nyingi, watu wengi watafaidika, watapata ajira. Hebu tuangalie, hapa pana viwanda saba. Lakini pia kwenye hivyo viwanda saba, kuna wakurugenzi na wasaidizi.

Kuna receptionist (mtu wa mapokezi), kuna wapishi, wahasibu, watu wa masoko. Kuna thinkers (wafikiriaji), jinsi gani product iwe, branding yake. Hawa wote watakuwa wamepata ajira.
"Lakini pia hizo bidhaa zote zikitengenezwa kwa ubora mzuri na branding ikawa nzuri tunaweza kushindana na watu wa nje kwa kupeleka bidhaa zetu.

"Kwa hiyo mheshimiwa rais, kwa kuangalia Korosho kwa upande wa bidhaa, kwanza exportation (usafirishaji bidhaa nje) kwenye nchi itaongeza thamani ya shilingi ya Tanzania. Lakini pia hawa watu wote ambao watakuwa wanafanya kazi kwenye hivi viwanda watakuwa wanatoa kodi.

"Jinsi gani ya kupata investors (wawekezaji) mimi najua. Mheshimiwa rais, najua wewe unaipenda sana Tanzania na unawapenda sana Waafrika ndiyo maana unakuwa mkali. Kwa hiyo napenda niishie hapa kwenye hii ishu ya Korosho na viwanda."

KUHUSU VIPAJI
"Kuwekeza katika vipaji, angalia matajiri wa dunia hii. Ni wale watu ambao wanatumia vipaji vyao. Mimi naamini tunaweza kuchezesha michezo. Tunaweza kutumia talents (vipaji) kuitajirisha Tanzania.
"Angalia ma-bodyguard (walinzi) wa wasanii, watu wanaofanya gym, wama miili mizuri ya mazoezi.

Mheshimiwa rais, mimi najua jinsi ya kuwaleta wawekezaji. WW ikaja hapa. Ukawaambia lengo letu ni kuweka ajira kwa vijana na kuwasaidia Watanzania kuwa na maisha mazuri bila kutegemea mikopo.

"Kwa makabila zaidi ya mia moja tuliyonayo Tanzania, vuta picha umeweka kabila moja watu kama hamsini kwenye stage (jukwaa) wanapiga ngoma kwa zile beats (midundo), unafikiri watalii wangapi wataongezeka hapa nchini?

"Tufanyeje kuhusu hili? Mheshimiwa rais tenga eneo kubwa sana. Kwa mfano, nje ya nchi, kuna sehemu inaitwa Las Vegas. Ni sehemu ya 'kula maisha.' Wewe tenga kijiji, hatutasema ni sehemu ya kula maisha, tenga kijiji ambacho kitakuwa Latest Beautiful Alena in Africa au in the world.

"Mheshimiwa rais, boxing around. Hebu mwangalie Mayweather (Floyd) anavyosumbua. Ni ngozi nyeusi. Maana yake sisi tumebarikiwa mheshimiwa rais. Swimming pool. Ukienda Zanzibar, Mwanza, kuna watoto wanapiga mbizi kupindukia. Hivi vipaji vyote tuviweke katika kutafuta pesa. Watu waje kuangalia pale, wanalipa pesa.

'Kwenye hicho kijiji kuwepo na sehemu za burudani, kama mashindano. Tuwape Watanzania vitu vya kufanya. Tanzania, Afrika zipewe hadhi yake. Wazungu wamechoka na tamaduni zao ndiyo maana wanatamani kwenda kuishi kwenye mwezi. Mheshimiwa rais, mimi naamini tukifanya hivi tutakuwa tumefika."

KUHUSU UTAMADUNI

"Kuhusu utamaduni mheshimiwa rais, ninayo ya kuongea. Nchi ambayo haina utamaduni inadharaulika. Na mtu yeyote ambaye hana utamaduni hahesabiwi kama mtu. Kwa kupitia tamaduni zetu, tunaweza kuajiri vijana wengi.

"Mfano, nizungumzie tiba asili ambayo pia ni sehemu ya utamaduni. Mheshimiwa rais, wewe unaweza kuwa na namna ya kutangaza dawa za asili. Tiba za asili zipo na zinafanya kazi sahihi. Zinaponya kweli. Mimi Babra nimekulia (dawa) Kanyigo, nikiumwa nimekulia Nkaka ambayo ni Alovera. Nimetwangiwa Mshana. Tulikuwa hatujui hospitali.

"Mimi nafanya kazi kwenye tiba za asili. Dawa zetu zilikuwa zinafanya kazi vizuri kabisa. Lakini wenzetu wajanja walipokuja wakaharibu. Sisi tulijua jinsi gani ya kusaidia tiba asili ifike mahali ambapo tulikuwa tunataka kufika. Tulikuwa tunataka tufike hatua badala ya kuletewa dawa za Nutrition Products supplements tufike levo ya kutengeneza supplements zetu na sisi tuwauzie wao.

"Mimi naamini unaipenda Tanzania. Lakini ukweli ni kwamba kuna watu wetu walikwama. Badala ya kusaidia Watanzania ambao wanajihusisha na tiba asili wasonge mbele, wao wakawa wanarudisha nyuma. Wanaweka vikwazo, wanasema msifanye chochote, mara wauza madawa ya kulevya.

"Nyie ni government (serikali), kwa nini msichunguze. Lakini pia ni waganga wangapi ambao wazazi wao walifariki dunia wamewaachia ile mitishamba? Sasa unapowasumbua au huwaelekezi, unawawekea masharti magumu lengo ni nini hasa?

"Mheshimiwa rais, naomba uwe rais wa kufufua vya kwako. Kwenye tiba asili zipo dawa za kutibu malaria ukapona kabisa. Zipo dawa za kutibu fangasi. Hata nguvu za kiume. Wachukuliwe Watanzania kumi, wapewe hizo dawa, muone kama hawatapona. Wakipona tisa maana yake hiyo dawa inafanya kazi.

"Una sera nzuri mheshimiwa rais. Lakini je, huko tunakokwenda wanaelewa? Ambacho tulitakiwa kufanya ni kuweka bajeti kuhakikisha miti ya tiba asili inalimwa kwa wingi. Tungekuwa hatuhitaji hizo dawa zao. Na ndiyo maana wanachukua magogo yetu kwa sababu wanajua kuna dawa. Tulipangiwa matangazo,eti tusiseme tunatibu, lakini kwenye dawa za Kizungu wao wanaandika zinatibu. Mheshimiwa rais, liangalie hili. Nashukuru sana."

IMG-20200205-WA0003.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ana ndoto Fulani Lakini hiyo ndoto inatakiwa ifanywe na sekta binafsi yeye anabwagia serikali!! Hizo kataja Ni fursa kwa sekta binafsi kutajirika

Dubai kwa mfano yote ile mijengo ya ajabu imejengwa na kampuni moja binafsi sio serikali

Tanzania hatuna venture capitalist wanunua mawazo ya biashara. Otherwise namshauri hayo mawazo yake aliyonayo na mengine atafute mfanyabiashara mkubwa waingie ubia wayafanye .

Mimi wahaya watani zangu naogopa kutapeliwa .Waweza pewa mchongo ukajua huu natengebeza bilioni Sasa hivi ukiingia kichwa kichwa unaliwa mzima mzima
 
Hayo sio Mambo ya kushauriwa Raisi wa nchi. Kwa vile wewe ni Mjasiri mali changamkia tu hizo fursa. Itafika pahali mpaka masuala ya Ukunga mpaka upate ushauri wa Raisi?
 
Back
Top Bottom