Mwaka 2020 utakumbukwa kama mwaka ulioshuhudia kampeni zenye ushindani mkubwa na msisimko wa aina yake katika jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjaro. Jimbo la Vunjo limekuwa kama jimbo la North East London huko Uingereza ambalo kila mwaka wa uchaguzi linabadilisha chama.
Kinyang'anyiro hiki ambacho ni vigumu kumtabiri mshindi wake hadi sasa kinawajumuisha vigogo wakubwa ambao ni James Mbatia (M/kiti wa NCCR) ambaye anatetea kiti chake, Augustine Mrema (M/kiti wa TLP) anayetaka kurusha karata ya mwisho kabla ya kustaafu siasa, Dr. Charles Kimei (CCM) aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa CRDB na Grace Kiwelu (CDM) aliyekuwa mbunge wa viti maalumu kwa miaka 15.
Utamu wa demokrasia umenoga katika jimbo la Vunjo kutokana na ushindani mkali unaolifanya jimbo hili la uchaguzi kuwa lenye msisimuko na ushindani mkubwa sana pengne kuliko jimbo jingine katika uchaguzi wa wabunge mwaka 2020. Hizi ndio siasa za ushindani tunazozitaka sio mambo hovyo ya kupita bila kupingwa.