Uchaguzi 2020 Mchuano wa ubunge Vunjo ni kati ya Mrema na Kimei

Majasho

JF-Expert Member
Aug 4, 2009
413
220
Katika majimbo yenye mchuano mkali ni Vunjo yupo Dkt. Charles Kimei wa CCM, Augustino Mrema wa TLP, James Mbatia wa NCCR- Mageuzi na Grace Kiwelu wa Chadema. Mwazoni ilionekana mchuano ulikuwa kati ya Mbatia na Kimei lakini hali ni tofauti Vunjo sasa. Mchuano umekuwa kati ya Mrema na Kimei. Sababu kubwa ni madhaifu ya wagombea wenyewe

1. Charles Kimei hajulikani jimbo la vunjo na Kitendo cha halmashauri Kuu ya Kamati kuu ya CCM kukata Jina la inock koola zadock mtoto wa Tajiri wa kimarangu Mzee Koola(Mmiliki wa makampuni ya Zadock A1outdoor Africa), ambaye alishinda kura Za maoni imeigawanyisha CCM jimboni vunjo pande mbili, wanao muunga mkono kimei na wale walichukizwa na kitendo cha koola kukatwa.

Pili, kwenye majimbo mengine mshindi wa kura Za Maoni alisindikizwa na walioshindwa kwenda kuchukua fomu na hata kumpigia kampeni mshindi, lakini hali ni tofauti vunjo ambapo Koola amegoma kumpigia kampeni Kimei na kuondoka zake kwenda Dar es Salaam.
Tatu, Palikuwa hakuna shamrashara kimei alivyotangazwa kama mgombea wa ubunge CCM vunjo.

Nne, kulazimishwa kustaafu CRDB, wananchi wa vunjo wanajua Magufuli alishauri astaafu kuliko kutumbuliwa kwa kashfa ya kulipwa mil 45 kwa mwezi. Hawa ndio wale waliomchukiza magufuli kwa kulipwa zaidi ya mil 40 kwa mwezi na alisema hadharani.

Tano, kuna bango lilisimikwa njia panda himo na wana CCM, upande mmoja picha ya magufuli na upande wa pili picha ya Mrema (angalia picha ya chini) ikileta tafsiri kwamba wana CCM watampigia Mrema kura.

Sita, kitendo cha Waziri mkuu Kassim majaliwa kutompigia kampeni Kimei, alifanya mikutano moshi mjini na vijijini akaenda kufanya mkutano Rombo wakati kwenda rombo unapitia Vunjo, hata Kimei alipojaribu kuusimamisha msafara wake haukusimama, wakati 2015 wakati Magufuli alivyokuja vunjo kwa ajili ya kampeni aligeuza msafara wake kuelekea Mwanga ili kumpa heshima na kumsalimia Mrema. Hivyo majaliwa kumtosa Kimei haijaleta picha nzuri vunjo.

1. James Mbatia alivyoshinda ubunge 2015 alilikacha jimbo na hakufanya kitu na alikuwa anaonekana kwa nadra sana jimboni humo. Alichangisha kila kaya 20,000 Za kuchonga barabara Jambo ambalo halikulitekeleza na limewaudhi wananchi jimboni humo. Madiwani wake wengi kumkimbia ndani ya jimbo hilo, kata kama Za Marangu magharibi diwani wake alijitoa na anagombea kwa tiketi ya CCM, hata mbadala wake waliomuweka kugombea kata hiyo amejiondoa, katika kata nyingi amepoteza wanachama kwa hali hiyo. Jambo jingine ni kwamba mbatia ushindi wake wa 2015 ulibebwa na ukawa na dhana kwamba lowassa angekuwa Rais na mbatia kuwa waziri wa elimu lakini hicho kitu hakipo kwa sasa kila chama kinajigemea hata Chadema ilimsaidia ashinde 2015, mwaka huu wameweka mgombea grace kiwelo. Mbatia mpaka sasa hajafanya kampeni anazindua kampeni zake tarehe 19.9.2020

3. Grace kiwelu hawezi kupata ubunge maana ukweli wachaga wao kutawaliwa na mwanamke inakuwa ngumu. Mbili, kuolewa na mwanaume wa old moshi na si wa vunjo. Tatu, kawa mbunge wa viti maalum miaka 10 hakuna alichosaidia wana vunjo na ameteuliwa na chama chake ubunge wa Viti maalum Chadema tafsiri yake si kwamba hayupo kwenye ushindani ni kwamba ameweka tu jina.

4. Augustino Mrema anafanya kampeni zake chini kwa chini na kura zote Za mbatia zitarudi Kwake, Vilio vingi ni kwamba wanajuta kumchagua Mbatia na mbadala ni Mrema.

Mbili, Mrema ana historia ya uchapa kazi nzuri vunjo na kitendo chake cha kuwa karibu na kumuunga mkono Rais, Dkt. Magufuli kitampa kura kwa sababu ya imani kubwa wananchi walionayo kwa Mhe. Rais kwamba anafanya kazi nzuri.

Tatu, Mrema kuteuliwa tena kuwa mwenyekiti wa bodi ya parole kwa kipindi cha pili 2020 - 2023 ni heshima kubwa aliyopewa na magufuli na yeye pekee yake kaingia kugombea ubunge bado kashikilia cheo alichopewa na Rais wengine wote wenye tamaa walitumbuliwa, wana vunjo wanajiuliza kama rais ana imani kubwa hivyo na Mrema kwa nini wasimpe ubunge.View attachment 1567986View attachment 1567988
 
Mrema si kazeeka sana aisee,,,watu wa vunjo hamlioni hili?.
Mpeni kimei au kiwelu acheni wenge...
 
Mrema si kazeeka sana aisee,,,watu wa vunjo hamlioni hili?.
Mpeni kimei au kiwelu acheni wenge...
Mbona Kimei na Mrema umri wao unalingana. Mrema kachoka tu kwa sababu ya njaa. Wanavunjo mkipa ubunge Mrema naye atanawili kuwa sawa na Kimei. Jaribuni kuwa na huruma wana Vunjo ili mzee wetu Mrema naye anawili.
i
 
Kimei mshahara wake mil 45 alikuwa anapewa na serikali au crdb ...unaandika upumbavu tu..magufuli yuko na power kiasi gani kwenye kampuni au taasisi binafsi Crdb


Huyo mrema anaumwa magonjwa mengi pia age yake ni 80+ kimei 60+ mbatia 50+ hapo dawa tunampa Kimei au mama Tanzania.
 
Back
Top Bottom