Mrema na Cheyo waomba CHADEMA ifutwe

Naona kila anayetaka kusikika siku hizi lazima azungumzie CDM. Sasa Cheyo na Mrema wakizungumzia mambo ya vyama vyao kuna mwandishi atakayeandika?

Cheyo kasema tunataka mambo ya Misri. Kwani mambo ya Misri ni mabaya? Kuondoa utawala wa kifisadi madarakani ni vibaya? Has Cheyo lost his marbles?

 
Wadau jana mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema na mwenyekiti wa UDP John Cheyo waliishambulia CHADEMA kwa maneno unayoweza kufananisha na matusi. Eti Mrema ameshauri CHADEMA ifutwe kwa sababu wanataka kuleta vita. Cheyo naye amesema CHADEMA wanataka kuleta mambo ya Libya na Misri.

Hivi kweli hawa ni wapinzani? Na kwanini wote wazungumze lugha moja kwa wakati mmoja. Imetokea kwa bahati mbaya? Eti Mrema anadai CHADEMA hawana uchungu na taifa hili na wanatumiwa na mataifa ya nje...


Huyu Mzee Mrema kwa vile hataki kustaafu siasa pamoja na uzee wake sijui mungu atatusaidia vipi waTZ kuondikana na kero hii!! Mungu Saidia TZ!!
 
Wadau jana mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema na mwenyekiti wa UDP John Cheyo waliishambulia CHADEMA kwa maneno unayoweza kufananisha na matusi. Eti Mrema ameshauri CHADEMA ifutwe kwa sababu wanataka kuleta vita. Cheyo naye amesema CHADEMA wanataka kuleta mambo ya Libya na Misri.

Hivi kweli hawa ni wapinzani? Na kwanini wote wazungumze lugha moja kwa wakati mmoja. Imetokea kwa bahati mbaya? Eti Mrema anadai CHADEMA hawana uchungu na taifa hili na wanatumiwa na mataifa ya nje...

Lisemwalo lipo na kama halipo laja.

hata Mbuyu ulianza kama mchicha. Chadema mpo hapoooooooo
 
Inawezekana hao watu ni Mamluki. Hatahivyo, ikumbukwe kuwa Rais ndiye aliwakumbusha CDM kuhusu kuzunguka nchi nzima pale aliposema vyama vya upinzani ni vya msimu.

Ingawa mimi sio mwanachama wa chama chochote, lakini hawa CDM wanaonyesha ukweli na hali halisi ya maisha ambayo kila mtu wa maisha ya kawaida inamgusa. Nani asiyeona tatizo la mago wa umeme? Hebu niambie maisha bora yatakuja nama gani kama kijana sitaweza kusaga sembe, kukuoboa mpunga au kuchomelea vyuma (welding), kunyoa watu saloon n.k kutaja machache, achilia mbali kuuza maji, soda na juice baridi. Na hizo 94 bilioni za kulipa Kampuni yenye utata? Haina hata anwani ya makazi!!!!!
 
wengine ugonjwa umewamaliza hizo bongo. Nashangaa kwa nini hawajaenda Loliondo au wanasubiri lift ya Jk? Mrema iko soku tutakutandika mbogo huku kiraracha subiri uone
 
Hii ni kutokana na ukweli kwamba kwa sasa watu tunataka kufanya mabadiliko ya kweli, hasa kwa njia ya mapinduzi ya nguvu za umma, hatuwezi tena kusubiri kura mpaka 2015.

Kikwazo kinakuja kwamba, tukitaka kufanya maandamano, serikali/CCM, itasingizia kwamba hawa ni CHADEMA, hata mimi nashawishika kwamba chama kikiongoza mapinduzi ya aina hii itaonekana kama ni uhaini/kupindua serikali, (treason) hata viongozi wake wanaweza kushitakiwa tukishindwa (hata kama watakua wameonewa).

Naomba sana serikali ya JK iifute CHADEMA kama ambavyo wameanza kutishia, tukishafanya mapinduzi, tukatengeneza katiba mpya chini ya jeshi then CHADEMA inaweza kuomba kusajiliwa tena upya, na viongozi walewale, ukombozi wa nchi uendelee, watakua wamekwepa lawama.

PEOPLESSSSSSSS..............
 
Wana JF hawa Cheyo na Mrema nashindwa kuwaelewa ni wapinzani au ni wachumia tumbo. Utashangaa kwanza wamechaguliwa na CCM kwenye maulaji yao halafu wanaiponda CHADEMA badala ya kuikosoa CCM(chama cha majambazi) huu ni uhuni na usaliti mkubwa.Baada ya kuona hawaukubaliki na Watanzania wanatafuta mbunu za kumwangamiza Dr Slaa mkombozi wetu wa kweli. Nawaambia mtakufa kifo cha mende msipojirekebisha kama JK wenu mnaemtetea. Wewe cheyo si uliseme bungeni kuwa baada ya DR wa kweli kukosa urais hana cha kufanya yule ni mbunifu angalia mnavyolialia sasa na mwaka huu mtalijua jiji mpaka kieleweke hakuna kulala mpaka 2015.
 
Hao huenda ni mamluki, kuweni makini na huo ushauri wao.Hatahivyo, huo ni ushauri tu wao sio watoa maamuzi. Ushauri ukitolewa, wenye maamuzi wataupima na kuufanyia kazi, na hapa wenye maamuzi ni wananchi.
 
Wadau jana mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema na mwenyekiti wa UDP John Cheyo waliishambulia CHADEMA kwa maneno unayoweza kufananisha na matusi. Eti Mrema ameshauri CHADEMA ifutwe kwa sababu wanataka kuleta vita. Cheyo naye amesema CHADEMA wanataka kuleta mambo ya Libya na Misri.

Hivi kweli hawa ni wapinzani? Na kwanini wote wazungumze lugha moja kwa wakati mmoja. Imetokea kwa bahati mbaya? Eti Mrema anadai CHADEMA hawana uchungu na taifa hili na wanatumiwa na mataifa ya nje...

Kaka kwani hilo la kutumiwa hulijui? na kama kweli hulijui basi inaonekana unafata mkumbo. Mrema na cheyo ni wakongwe katika siasa ya hapa TZ kwahiyo wanahaki kikatiba kutahadhalisha wanachama wao na watanzania kwa ujumla kwa mienendo ya aina yoyote inayoweza kuipelekea nchi pabaya.

Halafu kwa kuonesha wewe ni mwepesi wa kukulili mambo na sio kuyapambanua unadhani maana ya upinzani ni kupinga kila jambo au wewe in all aspect unakuwa againist gov. upinzani wa kweli ni wakuyafanya kwa vitendo mambo ambayo serikali inakuwa imeonekana kushindwa ili nyinyi mpendwe na sio kufanya vurugu. Hilo limesha onekana ni kama kijiwe cha wahuni ambao wanatumia udhaifu wa wananchi kusaka madaraka kwa nguvu. it will never happen
 
Akili za tope ni kama hii. Tanzania ina mahakama na unafuta utawala wa sheria mtu kama akifanya kosa si anafikishwa kwenye mkondo wa sheria wacha kutekwa na propaganda za chama cha majambazi. Huu ni utoto wa kufikiri.
 
CCM imekuwa kwenye "fungate la kisiasa" miaka yote tangu kuanza kwa siasa za vyama vingi mwaka 1992. Hata wenyewe, kwa kujua au kutojua, wamekuwa wakivikebehi vyama vya upinzani kuwa ni vyama vya msimu na vyama vya uchaguzi. Sasa kimejitokeza chama ambacho kinafanya kazi "full time" na kimejionesha kuwa si "chama cha uchaguzi", CCM hao hao wanaanza kupiga kelele! Jambo hili linashangaza sana. CCM mlipokuwa mkivikebehi vyama kuwa ni vya msimu na vya uchaguzi tu mjue kuna watu walikuwa wanazifanyia kazi kauli zenu ati!

Sasa CCM ijue kuwa fungate la kisiasa limekwisha na inatakiwa kifanye kazi na si kulalama kila siku eti amani inahatarishwa. Hadi sasa hakuna tukio hata moja katika mikutano na maandamano yaliyofanyika linaloashiria kuwa amani imewekwa hatarini, ukiacha lile la Arusha ambalo mfululizo wa matukio unaonesha kuwa jeshi la polisi ndo alikuwa kinara wa kuvuruga amani. Hali ikiwa hiyvo, ni nani basi mwenye kupata moyo wa ujasiri wa kusema Chadema wanavuruga amani?

CCM iache woga! Iache kutojiamini. Maandamano na mikutano ya Chadema, ndo sisa zenyewe! Na inatakiwa ziendelee hadi 2015. CCM mjue kuwa mna mzigo mkubwa wa kutekeleza ahadi zenu za kwenye ilani ya uchaguzi na za mgombea wenu. Kitengo chenu cha propaganda kimekufa baada ya uchaguzi? Kwa nini sasa hivi CCM inajisimika nyuma ya serikali na kuifanya serikali iwe ndo msemaji wake? Jamani CCM na serikali ni vitu viwili tofauti, tunatarajia tuone CCM ikipambana na Chadema kwenye majukwaa ya siasa! Hili la CCM kuwatumia watendaji wa serikali kuisaidia kujibu mapigo kunazidi kuifanya CCM ionekane chama dola, chama cha Kikoministi ambacho hakitenganishiki na dola. Hivi CCM hiyo "hangover" bado tu haijaisha?

CCM amkeni, muwasimamisheni viongozi wenu wa propaganda, waende wakaitetee serikali yenu kule kwa wananchi! Wakapambane na hoja za Chadema kuitetea serikali yake. Kwa mfano wakaseme jinsi ambavyo mkataba wa Dowans ulivyo halali na wakaseme jinsi ambavyo haiwezekani kuiondoa Tanzania kwenye mgao wa umeme!

Halafu tutawaachia wananchi kuamua mbivu na mbovu ni zipi! CCM kuendelea kuamini katika nguvu ya dola na kutumia marungu ya nguvu hizo za kidola kupambana na upinzani ni vitu vilivyopitwa na wakati na havitawasaidia mbali ya kuzidi kuwafarakanisha na wananchi! CCM iwe tayari kushindwa kwa hoja bila kuamsha matumizi ya maguvu. Mpaka hapo, maandamano yote yamekuwa ya amani na hakuna tatizo. CCM kama haiwezi kushindana na hoja zinazotolewa kwenye majukwaa hayo, basi ukubali kupigwa ngumi za usoni na ijue 2015 itakuwa kiyama yake.

Lakini ikianza kutumia nguvu ya dola kupambana na wapinzani wanaofanya kazi za siasa (ambazo CCM muda mrefu imekuwa ikiwakejeli kwa kutozifanya) itakuwa ndo kuvuruga amani kwenyewe. Hili litasababisha nchi yote ianguke pamoja na CCM!
 
Kuifuta CDM ni kuwapa sifa za bure tu. Watanzania wenzangu wapenda amani, Ivumayo huwa haidumu, wananchi watawachoka tu,, nani asiyependa amani,, nani anataka maisha ya ukimbizi? Na tayari watu wameshaanza kuwashtukia. Waacheni kama Mwalimu alivyosema juu ya Mrema wakati ule polisi wanamsumbua. Naomba waachiwe uhuru wooote, waende kote, na polisi wawape ushirikiano mzuri tu, tusiwabague ni wenzetu hao, watasema na maneno yatakwisha, watu tunawaangalia tu.
Maji ya moto hayo, yatapoa tu.
 
Kaka kwani hilo la kutumiwa hulijui? na kama kweli hulijui basi inaonekana unafata mkumbo. Mrema na cheyo ni wakongwe katika siasa ya hapa TZ kwahiyo wanahaki kikatiba kutahadhalisha wanachama wao na watanzania kwa ujumla kwa mienendo ya aina yoyote inayoweza kuipelekea nchi pabaya.

Halafu kwa kuonesha wewe ni mwepesi wa kukulili mambo na sio kuyapambanua unadhani maana ya upinzani ni kupinga kila jambo au wewe in all aspect unakuwa againist gov. upinzani wa kweli ni wakuyafanya kwa vitendo mambo ambayo serikali inakuwa imeonekana kushindwa ili nyinyi mpendwe na sio kufanya vurugu. Hilo limesha onekana ni kama kijiwe cha wahuni ambao wanatumia udhaifu wa wananchi kusaka madaraka kwa nguvu. it will never happen
Mwaka huu mtaweweseka sana, katika sehemu zote walikopita Chadema ni wapi wamefanya fujo? kwanini serikali isitekeleze madai ya wananchi badala ya kutumia mbinu chafu kujaribu kuzoofisha maadandamano ya CDM....if it will never happen, mnachachawa nini sasa tulieni!!
 
Mkuu nimekuelewa saana tuu!

nikweli cdm kifutwe ili kuondoa visingizio na wanachi tuitoe ccm kwa nguvu!

Kikwete USIJARIBU KABISAA KUFANYA HAYA NI HATARI SAANA!
 
kuifuta cdm ni kuwapa sifa za bure tu. Watanzania wenzangu wapenda amani, ivumayo huwa haidumu, wananchi watawachoka tu,, nani asiyependa amani,, nani anataka maisha ya ukimbizi? Na tayari watu wameshaanza kuwashtukia. Waacheni kama mwalimu alivyosema juu ya mrema wakati ule polisi wanamsumbua. Naomba waachiwe uhuru wooote, waende kote, na polisi wawape ushirikiano mzuri tu, tusiwabague ni wenzetu hao, watasema na maneno yatakwisha, watu tunawaangalia tu.
Maji ya moto hayo, yatapoa tu.
wewe ndo kilaza wakufa mtu hata upepo huoni, mkuu ccm mnakazi kubwa saana ya kuleta mapinduzi kiuchumi acheni mbwembwe!!
 
Hata kama CDM wata kaa kimya kuna maandamano mengine yana kuja wanafunzi wanadai kulipwa kila siku angalau 10,000 kwa mahesabu ya haraka haraka ni takibani mil 4 kwa mwanafunzi kwa mwaka...wafanya kazi ambao ndiyo wenye familia na majukumu mbali mbali zaidi ya wanafunzi hawapati kiasi hicho kwa mwaka...JK kashaunda tume ya kushugulikia tatizo hilo mziki utakuja akikubaliana na mtakwa ya wanafunzi......
 
CHEYO NA MREMA hawanao mafisadi tu..!!.Usually
when people are sad they don't do anything they just CRY over their
condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)
.
 
jamani msipoteze muda,mrema anaumwa mpaka kichwani..cheyo ana frustrations za chama chake kushindwa hata kuchukua udiwani..si saizi yetu wale..tugange na CDM yetu wanatupotezea muda!
 
Back
Top Bottom