Mateso
JF-Expert Member
- Aug 6, 2008
- 259
- 19
Wana JF waliokwishatembelea Moshi au wanaotokea Moshi wanakumbuka ama wameambiwa mengi kuhusu maendeleo ya Jimbo la Vunjo tangu Mrema alipohama CCM na kuingia upinzani. Kwa wale wasiojua naona niwajuze kidogo. Mrema alipokuwa Waziri wa mambo ya Ndani alikuwa mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini. Kwa wakati huo alijitahidi sana kulitetea jimbo lake na wapiga kura walifurahia na kupenda jitihada zake kiasi cha kuamini kuwa angekuwa mbunge wao wa kudumu. Mapipa mengi ya lami yalinunuliwa kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutoka marangu mtoni kwenda kilema na kiraracha kwake.
Wakati uongozi wa awamu ya pili unajianda kumaliza kipindi chake Mrema akaanza kufichua mambo ya ufisadi likiwemo la mashamba ya mkonge akashindwa kutunza siri za Baraza la mawaziri na hivi akawajibishwa na kujiuzulu. Baada ya hapo akaingia NCCR na akaleta upinzani mkubwa sana kwa CCM mwaka 1995.
Wananchi wengi wa Kilimanjaro walijiunga na NCCR na jimbo la Moshi Vijijini likachukuliwa na NCCR. Baada ya hapo mipango yote ya maendeleo kwa jimbo hilo ilisimama na Serikali ya BM haikutupia jicho jimbo hilo kabisa kwa sababu lilikuwa chini ya upinzani. Kwa hali hiyo ile barabara ya marangu kilema haikujengwa tena na mapipa yote ya lami yaliibiwa.
Barabara hiyo kwa sasa hivi ni mbovu sana ijapokuwa inapitisha magari mengi sana, Yaani magari ya abiria toka kilema kwenda moshi mjini yanapita kila baada ya dk 5-10. Sasa hivi baada ya CCM kuchukua jimbo la Vunjo kuna mpango wa kujenga barabara kutoka marangu mtoni kwenda kilema hadi mlima kilimanjaro na kupitia kirua hadi kawawa road.
Kwa hali hiyo basi nasema Mrema hana tena nafasi ya kupewa ubunge kwenye jimbo la Vunjo kwani anaweza kuja kuharibu mpango ulioko wa kujenga barabara zilizotajwa. Ni kwa hali hiyo basi namshauri Mrema aache tamaa zake za Ubunge apumzike kama Mwenyekiti.
Nasema hivyo kwa sababu yeye sasa hivi hawezi tena mikikimiki ya ubunge kwani amezeeka na anasumbuliwa sana na Kisukari. Kwa ujumla wake nisingependa wanajimbo wa Vunjo kudanganyika na kumwendekeza Mrema ambaye sasa hivi ameshahamasisha vijana wake kufanya fujo hata kwenye mikutano ya hadhara ya Mbunge wa sasa hivi.
Je kama anafanya hivyo sasa hivi mwakani iwakati wa kampeni takuwaje? TAHADHARI CHUKUENI HATUA.