carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 280
- 648
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Chamwino, mkoani Dodoma, Godfrey Mnyamale, amemtangaza Dkt. Netho Ndijina Ndilito wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa mshindi wa uchaguzi wa ubunge katika jimbo hilo baada ya kupata kura 70,974, sawa na asilimia 81.9 ya kura zote halali.
Mnyamale ametangaza matokeo hayo usiku wa kuamkia leo Novemba 5, 2026, baada ya kukamilika kwa zoezi la upigaji na kuhesabu kura. Uchaguzi huo ulihusisha wagombea 16 kutoka vyama mbalimbali vya siasa.
Kwa mujibu wa matokeo hayo, wapiga kura walioandikishwa walikuwa 133,864, ambapo 87,329 walijitokeza kupiga kura, sawa na asilimia 65.24. Kura zilizokataliwa zilikuwa 739, huku kura halali zikiwa 86,590.
Mgombea aliyefuatia kwa wingi wa kura ni Philemon Nyakapala wa CHAUMMA aliyepata kura 10,315, akifuatiwa na Exavery Mapunda wa AAFP (1,042), Shabani Kirita wa SAU (843), Mohamed Mnyalape wa NLD (562), Christina Denis Sembuche wa NCCR-MAGEUZI (483), Samwel Mazengo wa UMD (476), Rahel George wa NRA (418), Jeremia Alexander wa ADC (351), Judith Ngolola wa ADA-TADEA (213), Lailath Mbuta wa TLP (197), Karunde Juma wa CCK (196), Baraka Machumu wa MAKINI (182), Nasma Hamisi wa UDP (173), Runna Karya wa UPDP (104) na Damaly Richard wa DP (61).
Baada ya kutangaza matokeo, Mnyamale amemkabidhi Dkt. Netho cheti cha ushindi wa ubunge. Sasa anasubiri kuapishwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Chamwino na kuanza kuwatumikia wananchi, akirithi nafasi iliyoachwa na Deogratius Ndejembi aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Tanzania.