Mrema lyatonga hawezi ubunge

Mrema lyatonga hawezi ubunge

Status
Not open for further replies.
Bwana mateso, acha Mzee wa kararacha aje awatese kwa kipindi kingine. CCM wamezidi unafiki. After all Mrema ameonyesha uzalendo wa kweli kwa kukataa unafiki wa ccm hata kama imebidi ateseke. Well come back mh mrema.



Hiyo sio hoja. Unachotaka kuwaambia wapiga kura wa Vunjo ni kwamba wakichagua upinzani hawataletewa maendeleo na serikali ya ccm sio? Kama ni hilo ni uoga hata hivyo walishazoea na usiwatishe.

Heshima kwako Mchili.

Leo wako wengi kweli sijui wametumwa na nani ?.Ukiona hivyo ujue Mzee wa Kiraracha anawatesa uko Vunjo.
 
MATESO,Bora ujiendee mamba club maana uajibishana na watu usiowajua , na wanajua kuliko wewe , kuweka taarifa za uongo hapa utaumbuliwa ndugu.

Kimaro, hafai kupewa nafasi nyingine tena ,kwani hakuna lolote alilolifanya ,na ni majuzi tuu wakati wa kampeni za serikali za mitaa alitafuta Ambulance mbili akawa anatembea nazo kwenye mikutano ya hadhara na kuwaambia wananchi wakiichagua CCM atawapa , na baada ya uchaguzi tarehe 26/10/2009 alitoa moja eneo la KILACHA-HIMO, na ile ya pili kumbe aliiazima kwa rafiki yake mmoja aliyepo Arusha , sasa huyu anafaa kuwa Mbunge wa Jimbo lenye shule nyingi za Sekondari Tanzania kweli?
 
MATESO,Bora ujiendee mamba club maana uajibishana na watu usiowajua , na wanajua kuliko wewe , kuweka taarifa za uongo hapa utaumbuliwa ndugu.

Kimaro, hafai kupewa nafasi nyingine tena ,kwani hakuna lolote alilolifanya ,na ni majuzi tuu wakati wa kampeni za serikali za mitaa alitafuta Ambulance mbili akawa anatembea nazo kwenye mikutano ya hadhara na kuwaambia wananchi wakiichagua CCM atawapa , na baada ya uchaguzi tarehe 26/10/2009 alitoa moja eneo la KILACHA-HIMO, na ile ya pili kumbe aliiazima kwa rafiki yake mmoja aliyepo Arusha , sasa huyu anafaa kuwa Mbunge wa Jimbo lenye shule nyingi za Sekondari Tanzania kweli?

Tunamhitaji Mzee wa Kiraracha Mjengoni full stop.
 
mimi ni mmoja kati ya apiga kura wa mzee wa kiraracha, tuna kila sababu ya kumrudisha mzee madarakani, maana hata huyo wa ccm amaejifanya mpambanaji ni usanii tu ndani ya nyumba ya sanaa, hata hotelini, ni muda wa kimaro kwenda kuuza chai hotelini kwake, full force mzee wa kiraracha ndani ya mjengo,
 
nashangaa sana kusoma thread nyingine, watu wanaamka na kupost upuuzi. mateso hizo data zako uezipata wapi, huko vunjo watu wanampenda kwasababu ya historia yake na mambo aliyoyafanya akiwa kama mbunge wao miaka kumi, takwimu za uchaguzi wa serikali za vijiji mrema amepata wenyeviti 20 na vitongoji 48, mbowe huko Hai amepat wenyeviti 4, lipumba nae patupu, sasa yupi mwenye nguvu ndani ya jimbo lake na ukizingtia TLP hawana ruzuku maana hawana tena mbunge. wakati chadema na mbowe wanapokea zaidi ya million 70 za ruzuku kwa mwezi. mrema ni tishio kwa ccm huko vunjo mpaka wanaanza kununua wenyeviti wa TLP.kimaro wanamzomea pande zote za vunjo maana hajaleta maendeleo yoyote jimboni kwake.
 
Kwa hali hiyo basi nasema Mrema hana tena nafasi ya kupewa ubunge kwenye jimbo la Vunjo kwani anaweza kuja kuharibu mpango ulioko wa kujenga barabara zilizotajwa.
..Nasema hivyo kwa sababu yeye sasa hivi hawezi tena mikikimiki ya ubunge kwani amezeeka na anasumbuliwa sana na Kisukari.
Mkuu Mateso, una umri gani? Hoja yako ni ipi sasa, Mrema ataharibu mpango wa kujenga barabara, au Mrema amezeeka na ni mgonjwa? Nataka nijue umesimamia wapi hasa ili nikujibu.
 
MBUNGE wa Vunjo, Aloyce Kimaro jana alikuwa na wakati mgumu baada ya kuzomewa na kundi la wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika mji mdogo wa Himo ulio kwenye jimbo la Vunjo, Moshi Vijijini.
....
Kadhia hiyo ilianza wakati Mbunge Kimaro alipozungumza na kuelezea kuwa yuko katika hatua za mwisho za kutatua kero ya muda mrefu ya maji katika eneo hilo lenye uhaba mkubwa wa huduma hiyo.

Baada ya kugusia tu suala hilo, Kimaro alishtukia sauti zikitoka kwenye kundi hilo zikidai kwa kelele kuwa mbunge huyo ni mwongo na kwamba hawamtaki, lakini Kimaro akaendelea kusisitiza kuwa kero ya maji itakuwa historia muda mfupi ujao.
.....
 
Mmemjibu vya kutosha, ila naongezea yafuatalo juu ya maendeleo na serikali:
Wananchi wanapaswa kutimiza wajibu wao na wakishafanya hivyo serikali lazima nayo itimize wajibu wake. Mbunge hatakiwi kuibembeleza serikali iwapo wananchi wameshatimiza wajibu wao; anapaswa kudai na si kuomba. Huyu Mateso anataka kutueleza kuwa ukichagua upinzani basi serikali inaacha kutimiza wajibu wake kwako!- la hasha, kwani nikichagua upinzani naacha kulipa kodi? kama nalipa na serikali inaniacha, je itawezaje kudai nami nitimize wajibu wangu?
Mateso anatudanganya - maendeleo yaliyo Kilimanjaro ni kwa sababu ya wao kuwa wapinzani wa muda mrefu. Kumbuka chief Marealle alishaenda kuomba uhuru wa kaskazini kabla Nyerere hajaenda kuomba uhuru wa Tanganyika! Ilibidi Nyerere amuombe Marealle waungane- hii ni sababu ya kwanza eneo hilo kupewa maendeleo -Nyerere aliogopa kuwa watajitenga.
Kilimanjaro walipochagua upinzani 1995 na 2000 ilibidi serikali ya CCM iwaulize sababu za kuchagua upinzani na kuichukia - waliipa CCM matakwa yao na ndipo wakaichagua kwa makubaliano maalum. Utaona basi kama si Kilimanjaro kuwa pinzani basi maendeleo yake yasingekuwa makubwa hivi!
Wananchi chagueni upinzani kama hamridhiki, na mkishafanya hivyo, msirudi nyuma mkifanyiwa hayo anayofikiria Mateso. Mkirudi nyuma mtapigwa nyundo kweli - msikubali hadi pawepo makubaliano juu ya kutekelezewa matakwa yenu; Na hii isiwe kwa CCM tu bali kwa yeyote mtakayemweka madarakani.
 
Sasa Mrema kavunja ukimwa katangaza rasmi kuwa anagombea ubunge Vunjo, kazi kwenu. Mwenye ubavu wa kupambana nae, ajipange kweli.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom