Mimi huwa sipendi stori za kutunga, kwani ni wapi walipoandika kwamba Mrema au Mtanzania yeyote mwenye sifa haruhusiwi kuomba nafasi ya UKURUGENZI TPA, bahati mbaya sikuona tangazo la post hiyo ninge apply. Hivi wenye mamlaka ya mwisho ya kutehua Mkurugenzi wa TPA ni AKINA NANI? Sasa kama Mrema amejipima akaona atupe ndoana yake i.e ajaribu bahati yake kwani tatizo liko wapi - kama ana some issues za ku-sort out, wanao mfanyisha usahili ndio wanajua jinsi ya ku-deal na vitu kama hivyo, sisi watu baki yanatuhusu NINI? Hii tabia iliyo jengeka siku za karibuni za kutaka kupre-empty au kushikiza Serikali kwa masuala ambayo hayatuhusu sijui inatokana na nini? mara Dk.Dau anataka kufanya hivi, mara Ridhiwani amejipanga kufanya vile, si hilo tu - tuhuma zinakwenda mbali kwa kuwagusa akina Marwa, Walwa - hata members wa Board hawakuwa spared nao ni Mamilo na Ulanga yaani tuhuma left, right and centre! Nilisha uliza humu siku za nyuma - hivi huyu Ridhiwani ana madaraka/mamlaka gani katika Taifa letu, lini alipewa Uwaziri usio na Wizara au ni Roving Balozi nini? Manake mambo mengine ukiyasikiliza utavunjika mbavu kwa vicheko - tamthilia zimezidi mno. Kwa nini atutaki kutulizana akili mpaka zoezi zima la kumchagua/appoint Mkurugenzi wa TPA litakapo kamilika, baada ya hapo kama kuna tatizo katika uteuzi si litajulikana tu, lakini watu wanakuja humu na wild madai/tuhuma, jumping guns wakiwa na madhumuni ya kuwakomoa au kuwaribia sifa binadamu wenzao. Mtu unabaki unajiuliza maswali mengi - je, haya madai/tuhuma yanatokana na an inside job ya baadhi ya wafanyakazi wa TPA walio apply post hii ambao wana ogopa ushindani, je madai/tuhuma hizi ni from without kwa wale walio leta maombi ya post ya Mkurugenzi wa TPA wanatafuta mbinu za kuwa-eliminated kiana watu wanao waona ni tishio kwao, baadhi yetu Watanzania tuna hila za ajabu sana.