Mrema aitolea uvivu CHADEMA

Mrema aitolea uvivu CHADEMA

Unajua Kisukari ni ugonjwa wa Ki Sugar ni cronic so si tatizo lake maana una tatizo la kumfanya mtu akapoteza kumbukumbu na akakata tamaa, namshauri atafute huduma ya ushauri nasaha asubiri siku za zake aende kwa amani badala ya kuendelea kujichafua kama popo.

tumekusoma ila angalia tu usije tangulia wewe mbele ya haki kabla yake. kufa ni kufa mbaya ukitangulia

Ninakuunga mkono Kapwani, inawezekana ule ni mzimu wake tu upo bungeni unaongea, ila bado hatujagudua EBU TUFANYE UCHUNGUZI WA KINA!!

tatizo lako ni dogo, baba yako kuwa haiwezekani ndio maang unamuonea wivu mrema. poor thing

zhu.jpg

gongsi.jpg

ht.jpg
thank you for sharing

du ndugu yangu kama wewe ni mvivu kusoma hustahili kuwa hata huku kwenye great thinkers, kwa sababu utakuwa unatuletea kahawa za vijiweni tu. kusoma ndio source ya kuchanganua mambo. jirekebishe baba hilo sio gazeti

mbunge wa vunjo (TLP) Agustine mrema ameilipua chadema kwamba inaanzisha maandamano ya kutaka nchi isitawalike. mrema alitoa kauli hiyo jana wakati akichangia bajeti ya wizara ya ujenzi, huku akitumia nafasi hiyo kukanusha kuwa kibaraka wa ccm, bali ataendelea kushirikiana kwa kila jambo. Akizungumza kwa jazba mrema alisema kitendo cha mbunge wa chadema kumwita kuwa ni kibaraka ,kimemfedhehesha kumdhalilisha yeye na watanzania wengine. mwishoni mwa wiki iliyopita, mbunge wa viti maalum chadema, chiku Abwao, alisema mrema ni kibaraka anayetumiwa na ccm kuvuruga upinzani. Akichangia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani, Abwao alipinga na kulaani kitendo cha wabunge wa upinzani wanaohamia ccm au wanaosimama na kuitetea serikali, huku akiwaita wabunge maslahi. jana, mrema katika mchango wake alisema yeye ataendelea kuungana na ccm, ambacho kimekamata dola kwa sababu wanainchi wake wanahitaji maendeleo kutoka serikali hiyo. Alisema chadema imekuwa ikifanya maandamano ambayo haijui maana yake, lakini akawataka wakumbuke kuwa hata misri kulikuwa na maandamano ya hiari kama hayo, mwisho wake yaliondoa serikali madarakani. chanzo gazeti la mwanainchi

article 18(b) ya CURT inampa uhuru mtu yoyote kutoa maoni yake,mwacheni mzee wa watu,tatizo lenu watanzania hamwangali nyuma mnaogopa kugeuka jiwe la chumvi?

pole saana.............umekurupuka na hiyo Article na hujaitafakari............really sorry for you!

ni kupitia hiyohiyo Article tunapata uhuru wa kuuchambua mchango wa Mrema bungeni.

Mzee wa udenda ashie huko.
Kisha zeeka kazi kusinzia bungeni na kungoja posho
Ni kibaraka hatari tangu upinzani umeanza yeye ni kuvuruga tu.
Anajikanyaga wakati anakubaliana kuwa maandamano yaweza ondoa serikali madarakani halafu anasema hajui kuhusu mandamano.

Yeye si ndiye aliye anzisha maandamano na kuwataka wafuasi wake wambembe juu na alikuwa anasababisha usumbufu sana dar.
Hana lolote thamani yake ilikwisha zamani akae huko kando. Ubunge wenyewe kapigiwa chepuo na ccmagamba.
Na yeye ni gamba wa ufisadi wa kupotosha watu .

Tatizo la mtoa hoja amesahau kuwa watz ni "wavivu" wa kusoma, ameandika gazeti zima!

Jisemee wewe peke yako! Kwa niini unawatukana Watz? Great Thinkers wanatumia data kutoa maamuzi. Wewe umepata wapi hizo data kwamba watz ni wavivu wa kusoma? Nimekasirika maana mimi nimesoma yote na nyingi tu ninaendelea kuzisoma na mim ni Mtz.

Nadhani kila mtu anajua kuwa huyu mzee yupo kimaslahi zaidi, alikuwa anajisafisha tu kwa lawama anazopewa za kutumikia ccm.

mrema huna ishu na hufagiliw na m2.. kwani wewe nan asiyekujua ni kibalaka wa magamba mpaka kadi yao unayo. na hasira na wewe nyambafuu..

Kwa Lyatonga hamna la ajabu hapa,alishapoteza mwelekeo kitambo.

Tatizo la mtoa hoja amesahau kuwa watz ni "wavivu" wa kusoma, ameandika gazeti zima!

"Watanzania" siyo kundi lisilo na tofauti.Ndani ya hilikundi kuna watu wa aina nyingi. Wewe umeweza kusoma na kugundua kaandika gazeti. tUSIWE WAVIVU KUFIKIRI....

Mtoa mada ana hadhira yake iliyoiandikia kwa kirefu - waliozoea kuzamia na kuibuka na mambo.

MBUNGE wa Vunjo, Augustino Mrema (TLP), ameliambia Bunge kwamba hakutumwa na wananchi wake kwenda bungeni kuchochea nchi isitawalike, na kwamba hoja za kuwa yeye ni kibaraka wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hazina ukweli.

Alifafanua kuwa uamuzi wake wa kutounga mkono baadhi ya uamuzi wa Chadema ni utashi wake binafsi.

Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Ujenzi jana, Mrema alisema, amesikitishwa sana na kauli ya Mbunge wa Viti Maalumu Iringa, Chiku Abwao (Chadema), aliyoitoa ndani ya bunge hilo hivi karibuni.

Mbunge huyo alipokuwa akichangia mjadala wa Wizara ya Mambo ya Ndani, alisema Mrema ni kibaraka wa CCM.

Mrema alisema, hoja hiyo haina ukweli wowote na kwamba hawezi kuacha kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete na Serikali yake, kwa kuwa ndiye mwenye mamlaka na madaraka ya nchi hii, na mengi ameyafanya kwa maendeleo ya wananchi wa Jimbo la Vunjo.

“Lazima nimuunge mkono Rais wangu, siwezi pingana naye ndiyo mtu mwenye madaraka na yote nitakayo kanifanyia jimboni, wengine wasio na madaraka siwezi waunga mkono,” alisema Mrema.

Alisema, suala la yeye kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa si upendeleo, na kwamba hata wao Chadema katika Bunge la tisa, walipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya hiyo anayoishikilia yeye.

“Mbona Bunge la tisa hao Chadema walipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa chini ya kiongozi wao Dk. Willibrod Slaa, ina maana nao walikuwa vibaraka wa CCM? Alihoji Mrema.

Alisema, hawezi kukataa anapoitwa na rais wake, na kwamba suala la kuwaunga mkono chama fulani ni utashi wa Mbunge na hakuna anayelazimishwa, akawataka wabunge wasigeuze Bunge kuwa sehemu ya uchochezi na kuvuruga amani, bali wafanye yale waliyotumwa na wananchi wao.

“Najua athari za maandamano nimewahi kuwa kiongozi wa juu serikalini, ni lazima tuwe na utaratibu mzuri, natoa tahadhari kuhusu maandamano ili yasitokee kama ya Libya, kwani nao walianza kwa maandamano ya amani lakini umeona mwisho wake,” alisema Mrema.

Usimseme mtu kwa ugonjwa anaougua kumbuka kuna kesho ndugu..au ndo umevuka mto?think thrice frend..

kweli kamanda.

ila afya yake ni choka mbaya, labda akapate kikombe kwa bibi wa tabora!

Similar Discussions

Back
Top Bottom