Tatizo la mtoa hoja amesahau kuwa watz ni "wavivu" wa kusoma, ameandika gazeti zima!
Nimesoma sociology....ninaelewa kuwa mwanadamu anaweza kuchange attitude towards jambo fulani lakini anapobadilika kuna mambo mawili ...kwanza kabisa kuna sababu iliyosababisha aamini jambo hilo na anapobadilika kuna jambo pia limetokea na kusababisha aamini kuwa alichokuwa anaamini awali kilikuwa na mapungufu kwaiyo haoni sababu ya kuendelea kuamini jambo hil katika mtazamo huo kwa iyo anaamua kubadilika.
Nikiwa kama mwanafunzi wa 'human geography' ninaamini pia katika role ya time and space katika maisha binadamu...kwa maana ya kuwa wakati fulani unaweza kukubaliana na jambo fulani na kundi fulani....lakini wakati mwingine unaweza kutokubaliana na watu wale wale hata ukiwa mahali palepale ila utategemea kwenye jambo gani...kama ni AJENDA ILE ILE uliyokubaliana nao awali then tunaweza kukuhoji sababu ya wewe kubadilisha mtazamo wako na itabidi uwe na majibu ya kutomung'unya ili tuelewe mwenzetu una ajenda gani.....kama utamung'unya mung'unya huwezi kuzuia watu kukuadhibu kwa kukupa label yaulichoonyesha .....
Nipo naangalia bunge hapa... Dr Augustine Mrema amepewa nafasi ya kuchangia katika hoja ya ujenzi...Mh mrema ametumia muda mwingi kuwalaumu watu wanaomuona kama kibaraka wa serikali....ametumia muda pia kujastifayi kwanini ana iunga mkono serikali and more specific JK...akitaja mazuri aliyotendewa katika jimbo lake nk. amesema pia si lazima awaunge mkono watu wa chama fulani na ajenda yao kuandamana kwa sababu yeye kwa uzoefu wake wa uwaziri/naibu waziri mkuu anajua athari ya uvunjifu wa amani....tena ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hakutumwa na jimbo lake kutaka nchi isitawalike!!
Mh. Mrema ninaamini kuwa watanzania wanaokuita au kukuhisi kuwa kibaraka wa serikali hawafanyi hivyo from no where! wamekupima maneno na utendaji wako toka umekuwa kiongozi wa umma wa watanzania. Ukiwa kiongozi wetu ndani ya ccm uliweza kutetea watanzania kwa nguvu zako zote, bila woga wala TAHADHARI....ulisimama kidete kutetea rasilimali zetu mfano loliondo...ulileta msamiati wa WALAHOI kuonyeshwa kukerwa na gap ya umaskini kati ya walionacho na wasio nacho....ukiwa upinzani miaka ya mwanzoni pia uliendelea na mapambano...hukuchoka kusuta serikali na sisi hatukuchoka KUSUKUMA GARI LAKO KUKUUNGA MKONO....
Ni sisi wale wale tulikuwa tunakuona kama kimbilio ndio tunafikiri au zaidi ya yote kuamini kuwa umekuwa kibaraka kwani mtazamo wako juu yaleyale uliyokuwa unayakataa / SERIKALI ILIYO LIKIZO ISIYOTEKELEZA MAJUKUMU YAKE HATA RASILIMALI ZAKE KUIBIWA NA WANANCHI KUWA WALALAHOI UMEBADILIKA.......... LEO SOKOINE ANGEKUWEPO NA ANGEKUWA ANAWATETEA WAHUJUMU UCHUMI ALIOKUWA ANAWASAKAMA........AU LEO HII MWALIMU ANGEKUWEPO AKATETEA UBEPARI.. NA KUANZA KUELEZEA SEHEMU YA UZURI WAKE TUNGEHOJI...kwaninini...kwa sababu jambo lilelile waliokuwa wanalikataa na kubuni mbinu za kupambanana nalo usiku na mchana ...sasa wanalizungumza kwa kulitetea NA KUJARIBU KUTUONYESHA UPANDE WAKE MZURI BILA KUGUSA KABISA UPANDE WA HASARA YAKE.
Hata wanachama wa magamba wanasema hali si shwari (rejea, warioba, kitine)...hata mwl nyerere foundation wenye ccm yao wanatumambia si shwari...so haiwezi kuwa shwari kwa sababu ya vijineno vyako ...endelea kula ulichopewa kama vita ya mafisadi imekushinda waache wenye uwezo nao waitekeleze huna haja ya kuwasakama waache na sera zao ..
KWAME NKURUMA, MWALIMU NYERERE, SOKOINE, LUMUMBA,WARIOBA WATAENDELEA KUHESHIMIKA KAMA VIELELEZO VYA UZALENDO KWA MATAIFA YAO...HAKUNA KILICHOWATENGANISHA NA UPENDO WA MATATIFA YAO, IWE NJAA, IWE SHIBE, IWE NI WAKATI WAKIWA MADARAKAI AU LA, HAWAKUYUMBA WALICHOKIAMINI WALIKITETEA hata baadhi yao kuuawa
kwani walijua mwanadamu kula matapishi yake ni dalili ya uendawazimu hakuna jina lingine
UMEANDIKA HISTORIA KATIKA TAIFA LETU MREMA na ITAKUHUKUMU
Wakati wa uchaguzi aliwaomba wapiga kura wake wampigie kura AKAFIE BUNGENI- anadhihirisha kifo chake hapo alipo anaandaa utitili wa watu kutoka CCM wa kumzika.Chadema wakichukua madaraka inaonekana ni wengi watajinyonga! Wa kwanza ni Zombe, na huyu bwana naona kama anataka kufuata mkumbo!
Tatizo la mtoa hoja amesahau kuwa watz ni "wavivu" wa kusoma, ameandika gazeti zima!