Mrejesho: Uso kwa uso na shemeji gesti

Mrejesho: Uso kwa uso na shemeji gesti

chief punguza kamba basi, mbona unanena uongo sanaaaaaaaaaaaa, mara demu wako mliajiliwa wote, mara uume ukashindwa kusimama, mara wazazi wamekuoza kwa lazima demu wako hana kazi....
sijui unazinyofoa wapi hizi hadithi...tupe link na sisi tuzamie huko
 
Pata picha mkeo akija kujua itakuaje kwasabu ipo siku atajua tu. Tafakari chukua hatua
 
Mmh hii ni story au ni kweli? maana mbna kila mara unakuja na story tofauti
 
Mkuu wewe una CHAI nyingi sana.... Soma hii story yako kidogo hapo chini.
Basi kama vipi uwe na ID nyingi !!!!

-----------------------------------
Sijawahi kumtafuta tena Mwarabu kwa hofu

Nilisamehe na mtoto maxima. Sasa nina watoto wawili namheshimu sana huyu mwanamke ameshinda mitihani yote.

Ni mkasa wa kweli ulionipata mimi mwenyewe nime share na nyinyi kama fundisho
 
Wife akijua hawezi kumpiga chini maana ukoo mzima wa wife wanamtegemea yeye, apigwe chini halafu waishije mjini na usukumani wamekimbia. Ila huyo mkeo ni zoba... mimi hata nilishasahau kama bado watu wanaishi na ndugu... hawajui ugumu wa maisha!!! Na mchepuko atakusaidia hadi lini? kwa hiyo umekua mtumwa kwa mchepuko maana unalelewa.
Siku wife akijua unapigwa chini aisee...hebu vaa viatu vya wife afu jitathmini


Baada ya hlo NATOA ushauri wa buree maana stori yako inafanana na brother angu
 
Angalia maisha yako yaweza kua mafupi sana!
 
Wasukuma ni noma sana
Kuna jamaa jirani yangu kwenye sehemu ya biashara yeye huwa saa 12 ameshafika kufungua wakati maduka yanafunguliwa saa mbili hadi tatu hapa mwanza mjini
Na yeye tukishafunga saa 12 jioni anatafuta vijiwe vya kupoteza muda hadi saa sita usiku nikaja siku moja kumuuliza kwanini hupendi kukaa na family yako?
Akaniambia mke wake ni msukuma ameleta ndugu zake watano wamejazana huko home kwa hiyo hana hamu ya kuwahi na walikuja na mchele gunia wamekaa hadi limeisha na hawaondoki eti wamekuja tu kusalimia

Hebu acha kuwasema wasukuma buana,nimekufa na kuoza hapo ati!
 
Wakuu habari za ujenzi Wa taifa
Mtakumbuka 2 weeks ago nilikuja kuwaomba Ushauri baada ya kugongana uso kwa uso na mke Wa Rafiki yangu guest akitoka room na zee moja hivi huku na mm nikiwa na mchepuko ambao yy hakuuona .
Hivyo akaniomba nimfichie siri bado anaipenda ndoa yake
Rejea post hiyo kwa Maelezo zaidi.

Mazungumzo
Alikua amependekeza tumalizane kiutu uzima ili nikae kimya forever, nilimuita sehemu iliyotulia kwa mazungumzo nikamwambia nimekusamehe sitatembea na wewe na pia sitamwambia mumeo
Kwa sharti la kuacha tabia hiyo
Akakiri na kujutia tabia hiyo na kuahidi kuiacha kabisa
Kwa kweli alifurahi sana akanishukuru kupita Maelezo
Ila bahati mbaya laki tano yake niliila
Pia nimemsisitiza sana mumewe kwa simu afanye awezavyo atafute kazi nyingine hapa dar kama uhamisho ukishindikana

Kuhusu mchepuko wangu
Mlinishauri mm pia niache uzinzi niachane na huo mchepuko wangu Wa arusha ambao nilikua nao siku tumegongana na shemeji guest

Ushauri huu umenishinda kwa kweli maana mchepuko huu ni asset kubwa kwangu
Mke nilie nae ni mama Wa nyumbani ambae nililetewa na wazazi kutoka nyumbani nikawatii wazazi na kumuoa

Mchepuko wangu nilisoma nao chuo na tulikua na ndoto za kuoana bahati mbaya destiny haikutaka hivyo ndipo yakatokea hayo ya baba kuniletea mke
Huu mchepuko unanipenda sana ukasema hata kama mm naoa tuendeleze tu uhusiano wetu, basi nikawa nimeoa,
Bahati mbaya mchepuko ulienda nje ya nchi kwa masters program na ulikaa huko karibu miaka 5 na ndipo ukarudi hapa na kupata kazi arusha

Kiuchumi
Kutokana na gharama za maisha kupanda na familia yangu kupanuka mchepuko huu umekua Msaada mkubwa kwangu
Hii ni kutokana na ukweli kuwa nimekopa mikopo mingi kazini na hivyo napokea mshahara kidogo sana uliobaki
Mchanganuo Wa makato au marejesho upo hivi:-

(1)salaried workers loan=250,000
(2)Credit union loan=
250,000
(3)departmental loan=250
(4)blue financial services=250
Total=1,000,000/=

Salary. Loans. Difference 1,500,000-1,000,000=500,000

Baada ya makato ya mikopo yote inabaki laki tano tu
Kiasi hiki ni kidogo mno kwa mahitaji ya familia yangu ambayo ni extended, wife ni Msukuma hivyo ana ndugu nane ninaokaa nao kwangu maana Wali ukipikwa ni kilo 3 kila siku
Kila ninapofanya jaribio la kuwaondoa ndugu hao wife hununa wiki mbili na hulala na suruali tatu za jeans, na skin tight na kufuli hivyo mm husalim amri na kuacha kuwaondoa
Hivyo Nina majukum mazito sana na mikopo yote imeshafanya maendeleo ikiwemo ujenzi

Kwa hali hiyo mchepuko wangu unakua na maana kubwa sana kusaidia gurudum pale ninapokwama
Mathalan January sikua na ada za watoto hata senti tano na kazini sikopesheki tena
Mchepuko wangu ulinisaidia kulipa ada ya watoto wote watatu ya shs 4,200,000
Kwa ahadi ya kuzirudisha ingawa sijarudisha hadi sasa

Mchepuko huu umeshiriki shughuli nyingi za kifamilia I.e harusi na misiba kwa hali na Mali kwa kuchangia pesa nyingi tu ingawa wife huwa anakutana nao katika hizo shughuli bila kuufahamu

Nikimpigia simu kuna jambo lolote lile yy huondoka fasta arusha na kufika haraka
Dar
Hivyo wakuu Nina upenda sana mchepuko huu ambao umenizalia mtoto mmoja kwa sasa na hauna mpango Wa kuolewa na mtu mwingine

Mlinishauri niuache mchepuko lakin nadhan hiyo ni suicide mission kwangu
Ndo maana huwa naupenda uislam kwenye hili la wake wengi basi tu kwa kuwa mm ni mkristo sina jinsi ngoja niende wote wawili ilimradi tu wife asifaham

Huenda kama kuna mtu ana idea nifanyeje au yeyote mwenye mchepuko Wa namna hii anidaidie alifanyaje akaachana nao
nifah pitia hapa
 
Last edited by a moderator:
Unajitetea kwa upuuzi, acha misimamo ya kijinga, tupa kule huo mchepuko
 
kila mtu jf analipwa mshahara wa milion na ushee, sisi walinzi dah!

Bora umeliona hilo.. Hapa wanazungumza wenye digriii.. Mwanzilishi wa Jf yuko wapi atutengee madaraja. La saba kwao.. Form four kwao, six kwao, certificate kwao, diploma pia nakuendelea....
 
habari rafiki yangu,
kwa uzoefu wangu katika ndoa yangu sijawahi kuwa na mchepuko wowote maana nimetosheka na mahaba ninayopewa na mke wangu, je ungekuwa wewe ndio mke ungevumilia upuuzi kama huo unao ueleza hapa?????? sh.500,000/= ni kubwa kama ukiweka matumizi yako vizuri kwani makosa umeyafanya mwenyewe
1.kukubali kutafutiwa mke wa kuoa
2.kuendelea na mahusiano na mchepuko wako wakati umepewa mke
3.kuhudumia kundi la watu wengi akati huna uwezo nalo

ushauri wangu achan na mchepuko kisha utulie na mkeo ulee watoto ulio nao pia nenda kakae na mkeo ukatathimini maisha yenu kulingana na kipato chenu kisha aamue kuendelea kukaa na ndugu au kuwarudisha kwao ili uwahudumie wakiwa kwao angalau tumia utaratibu huu ili uzione baraka
katika mshahara wako unao baki baada ya madeni yako tenga 30%-ya akiba, 40%-weka matumizi yako,10%-dharula, 5%-weka fungu la misaada kwa hao ndugu n.k ukitaka maelekezo ya namna ya kuijenga familia yako nitafute kwenye 0753954715
 
Wadau kwa jinsi nilivyosoma kisa hiki nina tend kuamini kwamba hii scenario ni ya kweli si hadithi tu,haya mbona yako sana kwa wasukuma? wana tabia ya kufunga tela na kukaa kwa ndugu hadi kumi.Iinavyoelekea huu mchepuko wake umeshajiona kwamba ni mke wa pili she seems to be committed kwa mtu wake na hivyo hana wazo la kuwa na bwana mwingine.Ila sasa mr Mchepuko kwa vile wewe umejitanabahisha kwamba ni mkristo hapo vitabu vitakatifu vinakubainisha kwamba kwa kuwa na mchepuko huo unazini hapo sasa ni wewe na Mungu wako kusuka au kunyoa chaguo la njia nyembamba na njia pana,kukaa kundi la mbuzi au la kondoo,kuwa mkono wa kuume au wa kushoto-the choice is yours.
 
chief punguza kamba basi, mbona unanena uongo sanaaaaaaaaaaaa, mara demu wako mliajiliwa wote, mara uume ukashindwa kusimama, mara wazazi wamekuoza kwa lazima demu wako hana kazi....
sijui unazinyofoa wapi hizi hadithi...tupe link na sisi tuzamie huko

ukiwa na mawazo hakika log in jamii forum

mawazo upungua ha ha ha mkuu umenichekesha
 
Mkopo wa milioni 1, unapata mshahara milioni na nusu, unakatwa hadi unabakiza laki 5? Kwani hizo laki 2 na nusu zote unamaliza baada ya miaka mingapi maana mbona kama huna mkopo wa kutisha its just an excuse?

Siku ukibambwa na mkeo utajua vizuri jinsi ya kuuacha mchepuka, sasa hivi haupo tayari,
 
Ata km ni muhongo kuna watu watajifunza na mawili matatu km si kuburudika.
big up kaka uko safi
 
Back
Top Bottom