Mkuu kama unaamini mkeo ni mwaminifu kwako basi tambua humtendei haki hata kidogo, wewe ni zaidi ya katili kwake, na ulimuoa ili umkatili. Hivi unajisikiaje unapokuwa na mchepuko wako faragha? mnafanya tendo la ndoa wakati si mwanandoa mwenzio??? hata mkeo huwa humkumbuki? fikiria ungekuwa wewe ndio mke!
Pia tambua huyo mchepuko yupo na wewe lakini huko Arusha ana michepuko mingine zaidi, we jisifie tu kuwa anakupenda na hana haja ya wanaume wengine??, imekula kwako, yeye akiwa Arusha akae tu bila ya kukutana na mwanaume eti kisa wewe upo, na hali anajua wewe upo na mkeo huku, hakuna ana michepuko mingine ya kutosha. Usipoangalia utakuja kumletea mkeo magonjwa na kumuumiza moyo wake.
Pia kuhusu msaada wa kimahitaji, unaona sifa kwa jinsi unavyosaidiwa, je asingekuwepo huyo mwanamke usingeihudumia familia mwenyewe? acha kubweteka akili kwa kuwa yupo mtu anakusaidia malezi ya familia, tafuta njia mbadala ya kupata kipato, na njia moja wapo ni kama ulivyoshauriwa hapo juu mfungulie mkeo biashara yoyote afanye. Sio kuchukua hela za watu tu ipo siku hizo hela zitakugharimu sana.
Pia acha kumsema mkeo vibaya, eti mama wa nyumbani, ulishindwa nini kumfungulia hata genge auze matunda tangu umemuoa, leo ndo umuone mama wa nyumbani?. Acha bwana huyo mchepuko atakufikisha pabaya japo leo unamuona mwema. Kuhusu ndugu chukua hatua ya busara tu wewe si ndio kichwa cha family.