Mrejesho: Sina hata pesa ya nauli kesho

Mrejesho: Sina hata pesa ya nauli kesho

mkandumbwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Posts
424
Reaction score
371
Wakuu nimekwama.

Sina hata pesa ya kuendea kzini kesho.

Nauza memory card ya simu 32gb. Ni original imekuja na simu. Bei 30,000/=

Karibuni kokote uliko Dar nitakufikishia.

Mrejesho:

Kuna muungwana wendetta amenitumia 40000 bila hata ya kuchukua memory card. Shukrani nyingi sana zifike kwake kwa kunisaidia katika mkwamo huu.

Naahidi kurejesha haraka iwezekanavyo.

My take.....
Usife na tai shingoni yanapokushinda weka wazi waweza saidiwa.

Shukrani kwenu nyote pia.
 
swali hatarishi!! we ni mmoja kati ya wachochezi au wapiga dili..?😱
 
swali hatarishi!! we ni mmoja kati ya wachochezi au wapiga dili..?😱
Sifungamani na pande hizo zote mbili mkuu. Nina memory card nauza elfu thelathini ama tubadilishane kwa lita 15 za peteol. Karibu mkuu. Popote ulipo Dar nitakuletea.
 
Duuuh pole mkuu ndio maisha yalivyo no wayout kikubwa tu upate wateja mimi niko mkoa ningeichukua hiyo kitu

Sent from mTalk using microsoft lumia 950xl
 
Sasa popote utafikaje wakati huna nauli wala petroli???
Kama nikiwa na uhakika wa biashara ya kuuza memory card nitaweza hata kuazima 5000 kwa mangi nikawa na uhakika wa kumlipa jioni. Karibu memory card ni shilingi 30000 tu ni 32 gb original. Popote Dar nakuletea.
 
Mbona mpya ni 25000
Nafahamu mkuu tena kkoo unaweza kupata mpya hata kwa elfu 15 tu. Lakini mm hii ninauza kwa 30. Kama unatazama bei nakushauri nenda kkoo, kama unatazama ubora karibu tufanye biashara.
 
Kadagalani aina gani na i class ipi

Sent from mTalk using microsoft lumia 950xl
 
Wakuu nimekwama.

Sina hata pesa ya kuendea kzini kesho.

Nauza memory card ya simu 32gb. Ni original imekuja na simu. Bei 30,000/=

Karibuni kokote uliko Dar nitakufikishia.
Haaaaaaaahh haaaahhhh...Pole sana
 
Kama hata nauli ipo huo mzigo utaufikisha vipi kwa mteja?
 
Pole sana mkuu.

Umenikumbusha nilivyokuwa kijana. Nilikuwa napata hela naitumia bila mpangilio.

Ikiisha tu, napigiwa simu na ndugu akiomba msaada wa kiasi fulani cha hela. Matokeo yake najutia sana matumizi niliyofanya.
 
  • Thanks
Reactions: 911
Back
Top Bottom